March 26, 2017 kupitia mtandao wa Instagram Meneja wa msanii Diamond Platnumz, Babu Tale aliandika kuhusu Wizara ya Maliasili na Utalii kushindwa kuwatumia watu maarufu nchini kuutangaza utalii wa Tanzania akiwataja mwanasoka Mbwana Samata na mwanamuziki Diamond Platnumz kati ya watu wanaofanya vizuri kimataifa lakini hawapewi dili hizo.
Alipotafutwa Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembealisema>>Wasanii wetu wenye majina makubwa watangaze tu Tanzania. Tanzania ni nchi yao sio lazima mpaka waambiwe waje tukae pamoja tupange mikakati na tuangalie ni kitu gani anaweza kufanya na watusaidie kutangaza utalii wetu.”
Baada ya Babu Tale kusikia majibu ya Waziri Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe ameamua kutumia ukurasa wake wa instagram kuandika anachofikiria au namna alivyomuelewa Waziri.
“Duh hapa sijui mimi mshamba au sijamuelewa vizuri Mh Waziri kuhusu kuitangaza Tanzania mimi kwa akili yangu fupi naona watu wa nchi jirani wanatafuta wasanii watanzania kutangaza nchi zao hapa kwetu tunaambiwa tuombe ili tutoe msaada mh sasa hela ya wizara inaenda wapi????
– Babu Tale.
“Cha ajabu unaweza ukaambiwa uitangaze nchi halafu utapelekwa mbugani bure duh. Ninachojua kila sekta inamfuko sasa hili eneo la utalii mfuko upo wapi mimi naendelea kuuliza mfuko wa kuitangaza Tanzania kwa nia nzuri na mazuri yaliyopo umewekwa wapi??>> – Babu Tale.
“Leo wasanii wengi wanakimbilia hata kufanya video zao nje ya nchi sababu ukitamani kufanya kitu nchini inakuwa kama mtu anakukomoa usifanye. Hvi Samatta anavyofunga magoli wangewaza kumvalisha bendera ya tanzania nguo yake ya ndani pale anapofunga goli avue watu waone duniani kuna nchi inaitwa Tanzania ingekuwa je?>> – Babu Tale.
“Sina nia mbaya ila tuamke kweli kuitangaza nchi yetu na sio wahusika waifuate sekta husika wakati kila sekta inakitengo cha matangazo na wanajua nani wakupewa jukumu #mtazamochanya#Tanzania #” >> – Babu Tale.