BAADA ya hivi karibuni mkewe kujifungua mtoto wa kike aitwaye, Anyagile, msanii wa Bongo Fleva, Naftar Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ amefunguka kuwa, mtoto huyo amempa mzuka zaidi wa kufanya muziki.
Akipiga stori na Showbiz, Nuh alianza kwa kufafanua maana ya jina la Anyagile kuwa linamaanisha amenikuta baada ya kumpokea, nguvu kubwa anaielekeza kwenye muziki ili apate chochote cha kumfanya akue.
“Nimefurahi sana kupata mtoto wa kike, mke wangu alishakuwa kwenye uhusiano na wanaume wengi lakini hajawahi hata kuwabebea mimba lakini kwa muda mfupi amenipatia kijike. Kilichobaki sasa hivi ni toa ngoma weka ngoma,” alisema Nuh anayebamba na Wimbo wa Anameremeta.