SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 5 Machi 2016

T media news

Waziri Mkuu wa Uturuki apokewa rasmi mjini Tehran

Waziri Mkuu wa Uturuki aliyewasili hapa mjini Tehran jana usiku amepokewa rasmi na Makamu wa Kwanza wa Rais.Is'haq Jahangiri, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemlaki na kumkaribisha rasmi Ahmet Davutoglu Waziri Mkuu wa Uturuki katika jengo la kiutamaduni na kihistoria la Ikulu ya Sa'ad Abad mjini Tehran.Baada ya Waziri Mkuu wa Uturuki kulakiwa rasmi, viongozi hao wameanza mazungumzo ya pande mbili ambayo yanahusiana na ushirikiano wa pande mbili, masuala ya kieneo na kimataifa.Akiwa hapa nchini Waziri Mkuu anatarajiwa kufanya mazungumzo na viongozi wengine wa ngazi za juu wa Iran akiwemo Rais hassan Rouhani.Ahmet Davutoglu Waziri Mkuu wa Uturuki jana usiku aliwasili hapa nchini kwa shabaha ya kufanya ziara rasmi akiwa anauongoza ujumbe wa ngazi za juu wa nchi yake wakiwemo mawaziri wa uchumi, forodha na biashara, nishati, usafiri na uchukuzi na mawasiliano na ustawi.Iran na Uturuki zinatarajiwa kutiliana saini mikataba kadhaa ya ushirikiano katika nyanja mbalimbali.Kwa sasa Iran na Uturuki zinafanya juhudi za kuinua kiwango cha uhusiano wao wa kiuchumi na kibiashara.