SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 5 Machi 2016

T media news

Ripoti: Israel inawaua kwa makusudi watoto wa Palestina

Harakati ya Kimataifa ya Kuwalinda Watoto imeripoti kuwa wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wanawauwa kwa makusudi watoto wa Kipalestina.Harakati ya Kimataifa ya Kuwalinda Watoto tawi la Palestina leo imeashiria kitendo cha wanajeshi wa Kizayuni cha kuwauwa shahidi watoto 41 wa Kipalestina tangu kuanza Intifadha ya Quds hadi sasa, na kusisitiza kuwa wanajeshi wa utawala huo wanatekeleza siasa za kuwafyatulia risasi kwa makusudi watoto wa Kipalestina kwa lengo la kuwauwa, hatua ambayo ni kinyume na sheria.Harakati hiyo imeashiria kuuliwa shahidi watoto 16 wa Kipalestina waliopigwa risasi na askari wa Israel katika mwaka huu wa 2016 na kuongeza kuwa, utawala huo umefunga mafaili ya mauaji ya watoto hao bila ya kufanya uchunguzi na umepinga pia ombi la familia za wahanga wa mauaji hayo waliotaka maiti za watoto wao zifanyiwe uchunguzi.Tangu kuanza Intifadha ya Palestina hadi sasa, makumi ya watoto wa Kipalestina wameuawa shahidi kwa kupigwa risasi kwa makusidi na wanajeshi wa Israel katika maeneo mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, Quds na Ukanda wa Ghaza.