Q Chief kuweka kambi Nigeria


Msanii wa muziki Q Chief amesema yupo mbioni kusafiri kuelekea nchini Nigeria kwa ajili ya kukutana na wadau mbalimbali wa muziki.

Muimbaji huyo ambaye anafanya poa na wimbo ‘Mkungu wa Ndizi’, ameiambia Bongo5 Ijumaa hii kuwa safari hiyo itamfungulia connection mpya za muziki wake.

“Unajua tayari nimeshafanya kazi nyingi sana hapa nyumbani, lakini pia nimeona kuna umuhimu wa kutoka kidogo na kujifunza mambo ya watu wengine. Kwa hiyo nipo kwenye mpango ya kwenda Nigeria kwa ajili ya kukutana na wadau mbalimbali ili kupata idea mpya, kwa hiyo nadhani kila kitu kikiwa sawa mutasikia nini kimetokea,” alisema Q Chief.

Q Chief ni miongoni mwa wasanii ambao wanafanya kazi chini ya kampuni ya muziki ya QS Mhonda.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: UTAMU WA MADAM JESCA

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU

SIMULIZI FUPI: UCHI WANGU UMENIPONZA