KILIMO CHA BUSTANI NA MAUA CHA DADA YASINTA...KARIBUNI !!!!!


Habari zenu..kuna wengi wameniuuliza vipi kuhusu bustani pia mapishi nipi na bustani ipi ila pilikapilika ni nyingi na hizi likizo lakini leo nimeona sio mbaya nichukue muda na kuwaonyesha maendeleo ya bustani yangu...Karibuni
 
 
 Nyanya zimeanza kukomaa karibu nitakula
 Kushoto ni mchicha na kulia ni figiri  mnaona ilivyokua
 Njegere zimeanza kuchanua
 Viazi mviringo(matosani)  navyo vimwanza kuchanua
 Mdada huyu ni mpenzi wa maua pia mawe hapa mnaona maua yako yanavyoendelea.
Kwa kuwa mtundu nikajaribu kupandikiza pilipili pia maana pitiku bila pilipili mmmmhh na matokeo ni haya
Sikuchoka nikajaribu kupandikiza dodoki  Nanasi na tangawizi---Dodoki kwenye hicho chombo cha bluu, nanasi chombo cha blauni na tangawizi chombo cheupe. Kwa msingi kwa kweli unaweza kupanda kila kitu na kuvuna. Haya nawatakieni Alhamisi njema na karibuni 

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: UTAMU WA MADAM JESCA|T MEDIA NEWS

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU|T MEDIA NEWS

SIMULIZI FUPI: UCHI WANGU UMENIPONZA|T MEDIA NEWS