SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 5 Machi 2016

T media news

Israel yakiri kuhusu nguvu ya Hizbullah ya Lebanon

Utawala wa Kizayuni wa Israel umekiri kuhusu uwezo wa kijeshi wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon.Jeshi la utawala wa Kizayuni jana Ijumaa lilikiri kuwa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon si kundi la msituni tena, bali kwa uhalisia wa mambo kundi hilo limegeuka na kuwa jeshi. Maafisa wa kijeshi wa utawala wa Kizayuni wametabiri kuwa, katika vita vyovyote vijavyo, Hizbullah ya Lebanon itaisababishia Israel hasara, vita ambavyo Wazayuni hawana uwezo wa kukabiliana navyo.Wakati huo huo vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni jana Ijumaa vilitangaza kuwa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon ina wapiganaji zaidi ya elfu nne ambao wana uwezo wa hali ya juu wa kivita na kiintelijinsia.Harakati ya Hizbullah ya Lebanon ilitoa pigo kubwa kwa utawala wa Kizayuni katika vita vya siku 33 ulivyoanzisha mwaka 2006 huko kusini mwa Lebanon ambapo hatimaye ulilazimika kurudi nyuma na hivyo kuipa Hizbullah ushindi mkubwa.