Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2016

VIGEZO SITA (6) MUHIMU VYA KUMPATA MUME/MKE BORA

Picha
Na Zuhura Simba Watu wengi wamejikuta kwenye kashfa za kuitwa wahuni kwa kubadilisha wanaume/wanawake kwenye maisha yao kwani wataalamu wa masuala ya mapenzi wanasema idadi kubwa ya wapenzi si kigezo sahihi cha kupima tabia ya mtu na kumhusisha na uhuni. “Wanasema msichana/mvulana anayeingia katika uwanja wa mapenzi kwa kuwa na hisia za kufanya mapenzi, hukosa umakini wa nani anafaa kuwa mpenzi wake kutokana na kukosa elimu ya uhusiano kutoka kwa wazazi wake”. Kama kawaida yetu  mtembezi.com  ni kukupa kile unachotakiwa kukijua ili uweze kupata muelekeo ulio makini kwenye maisha yetu hasa kwenye upande wa malidavi. kutambua vigezo vya mwenza wako unaye muhitaji; kwa kila mwenye mwenza wake inabidi ujue mahitaji ya nafsi yako kwa kujua nini unataka kwenye mahusiano yako kwani watu wengi hawana elimu ya kutosha kuhusu mahusiano ndo mana unaambulia kuhangaika mara kwa bwana Juma mara kwa hasani au kwa upande wa wanaume ndo wanabadilisha sketi kam misemo ya...
Picha
Mahakama ya Kikatiba nchini Afrika ya Kusini imemuamuru Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma ndani ya siku105 awe amerejesha serikalini dola milioni 16 fedha za walipakodi ambazo alizitumia kukarabati makazi yake binafsi. Mahakama hiyo imesema Rais Zuma mwenye umri wa miaka 73 alikataa kutii agizo kutoka kwa ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu mwaka 2014 la kumtaka alipe fedha hizo zilizotumika kuifanyia ukarabati nyumba yake ya kibinafsi. Jopo la Majaji 11 wa Mahakama hiyo ya Kikatiba ya nchini Afrika ya Kusini limesema Rais Zuma alikiuka Katiba ya nchi hiyo kwa kutumia fedha hizo katika ukarabati wa nyumba yake hiyo ambayo ipo eneo la nkandla -kwazulu-natal na kuhitimisha miaka 6 ya sakata hilo. Chama cha siasa cha Democratic Alliance cha nchini humo  kimeanzisha kampeni ya kumuondoa Rais zuma madarakani baada ya mahakama ya kikatiba kutoa uamuzi kuwa alikiuka Katiba. Vyama viwili vya upinzani viliwasilisha kesi hiyo mahakamani ili kumlazimisha Rais Zuma kuzingatia matokeo ya u...

Za Mwizi ni Arobaini..Wezi wa Nyaya za Kampuni ya TTCL Wakamatwa

Picha
WANANCHI  wa Mtaa  wa soko la sovya Wilayani Kasulu usiku wa kuamkia leo wamewakamata wezi waliokuwa wamekata nyaya za mawasiliano za kampuni ya TTCL.  Akiongea juu ya tukio hilo Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya simu TTCL nchi Dk Kamugisha Kazaura alisema kuwa tukio hilo limetokea katika eneo la soko la sovya majura ya saa kumi na moja alfajiri. Alisema kuwa wananchi  wanaoishi karibu na eneo lililokatwa nyaya hizo ndiyo waliowakamata vijana hao baada ya kufanya uhslifu huo. Mkurugenzi huyo alisema kuwa hasara waliyoipatia kampuni kwa kukata nyaya hizo inakadiliwa ni zaidi ya milioni 20. "Hasara waliyoingizia serekali ni kubwa sana hizo nyaya walizokata zinagharimu milioni 20,lakini kuitengeneza upya line hiyo inaweza kugharimu zaidi ya hiyo fedha''alisema Kazaura Alisema kutokana na wezi huo umepelekea baadhi ya ofisi za serekali kukosa mawasiliano ikiwemo ofisi ya polisi Wilaya,Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Bank na Takukuru. Naye Waziri wa Ujenzi, Uchuk...

Sakata la Wastara Kutoroshwa Hospitalini...Ndugu Wakwama Kumpata Alipo

Picha
Hali bado tete! Baada ya Gazeti la Ijumaa Wikienda ambalo ni dugu wa damu na hili toleo la Jumatatu iliyopita kutoka na habari yenye kichwa kisemacho; WASTARA ATOROSHWA HOSPITALINI, habari mpya ni kwamba, nduguze wameshindwa kujua wapi alipo mpaka sasa. Kwa mujibu wa chanzo chetu, Ijumaa iliyopita, baadhi ya ndugu wa Wastara, wakiwemo dada zake, waishio jijini Dar walikodi gari ndogo ili kwenda Morogoro kumfuata Wastara na kumrejesha Dar ambako ndiko kwenye makazi yake, lakini walidunda dakika za mwisho wakiwa Mwenge, tayari kwa safari. HIKI HAPA CHANZO “Jamani Wastara amezua balaa. Mnajua kwamba ndugu hatujui alipo mpaka sasa. Baada ya kuondoka nyumbani kwa mumewe (Mbunge wa Jimbo la Donge, Zanzibar, Sadifa Juma) hapa Dar, alikwenda Morogoro kwa huyo mtu aliyesema ni babu yake, Abdulaaziz Babu kwa lengo la kupumzisha akili. “Sasa baada ya kusikia ameugua ghafla maradhi ya kisukari na moyo na amelazwa Hospitali ya St. Herry Health Centre , sisi ndugu tuliamua kumfuata. ...

Soma Nafasi za Kazi Mbali Mbali Zilizotangazwa Magazetini Siku ya Leo...

Picha
Hapa nimekuwelea link ambayo unaweza kusoma nafasi za ajira zilizotangazwa katika magazeti ya leo tarehe 31 March 2016... Bonyeza  HAPA   Au Tembelea   www.ajirayako.com

Nape Nhauye Atema Cheche..TFF Inao Uwezo wa Kumlipa Kocha Mkuu wa Taifa Boniface Mkwasa...

Picha
Serikali ya awamu ya tano kupitia Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye imesema kwamba Shirikisho la Mpira wa miguu nchini TFF linapaswa kumlipa mshahara kocha wa timu ya taifa (Taifa Stars,) kwa sababu uwezo wa kubeba majukumu hayo wanayo. Charles Boniface Mkwasa alichukua nafasi ya M-holland, Marti Nooij, Juni 21 mwaka uliopita na ilisemwa kwamba serikali itaendelea kuisaidia TFF kumlipa kocha wa timu ya Taifa na Mkwasa (kocha wa kwanza mzawa tangu 2006) angeendelea kulipwa mshahara kama ule ambao makocha wa kigeni walikuwa wakilipwa. Mbrazil, Marcio Maximo aliifundisha Stars kwa miaka minne kati ya 2006 hadi mwaka 2010, Mdenmark, Jan Borge Poulsen alichukua nafasi hadi mwaka 2012 tinu hiyo ilipochukuliwa na Mdenmark mwingine Kim Poulsen ambaye naye aliisimamia hadi mapema mwaka 2014 alipopewa majukumu hayo Nooij. Makocha wote hao walikuwa wakilipwa mishahara yao na serikali iliyopita ya awamu ya nne chini ya rais mstaafu, Mh. Jakaya Mrisho Kikw...

Magufuli amponza 'Mlevi', Apandishwa kizimbani kwa tuhuma za kumtishia kifo Rais Magufuli

Picha
HAMIMU Seif, mkazi wa Mwananyamala Ujiji, Dar es Salaam, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu akituhumiwa kumtishia kifo Rais John Magufuli, anaandika Faki Sosi. Mbele ya Hakimu Mkazi Helleni Liwa, Keneth Sekwao, Wakili wa Serikali, aliiambia mahakama kuwa kijana huyo alitishia kumuua rais Machi 10 mwaka huu, alipokuwa katika baa ya Soweto maeneo ya Makumbusho, Jijini Dar es Salaam. Sekwao ameeleza mahakama kuwa kijana huyo alitamka kuwa amechoshwa na mambo anayofanya rais, na kwamba yupo tayari kujitoa mhanga kwa kujilipua na bomu. Mshitakiwa amekana mashitaka, na mahakama imeweka wazi dhamana yake. Kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo tarehe 14 Aprili mwaka huu.

Taarifa Rasmi ya TAKUKURU Kuhusu Kuwafikisha Wabunge Watatu Mahakamani Kwa Rushwa

Picha
WABUNGE WATATU WAJUMBE WA KAMATI YA HESABU ZA SERIKALI ZA MITAA WAMEFIKISHWA MAHAKAMANI KWA RUSHWA --   Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) leo tarehe 31/3/2016 imewafikisha Mahakamani wabunge watatu ambao ni wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa kwa kosa la kushawishi na kuomba rushwa ya Shilingi Milioni thelathini (30,000,000/-) kinyume na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007 kifungu cha 15 (i)(a).  Wabunge hao ni  Mheshimiwa Suleiman Ahmed Saddiq Mbunge wa Mvomero;Mheshimiwa Victor Mwambalaswa Mbunge wa Lupa na Mheshimiwa Kangi Lugola Mbunge wa Mwibara. Wabunge hao wamesomewa shitaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mfawidhi, Mh.Thomas Simba.  Akisoma mashtaka hayo wakili wa TAKUKURU, Maghera Ndimbo akishirikiana na Emmanuel Jacob alisema kuwa mnamo Machi 3, 2016 majira ya saa 2 - 4 usiku, katika Hotel ya Golden Tulip iliyopo jijini Dar es Salaam washtakiw...

Tetesi: Kikwete Kumrith Ban Ki-Moon Umoja wa Mataifa

Picha
Dr. Jakaya Mrisho Kikwete Rais mstaafu wa Tanzania kwa awamu ya nne (2005 – 2015) ni miongoni mwa wanadiplomasia wakubwa duniani wenye ushawishi na uwezo wa utatuzi wa matatizo mbalimbali duniani, sio tu kwa sababu viongozi wa mataifa mbalimbali duniani wanamkubali bali kwa uwezo wake katika masuala ya kidiplomasia. Alizaliwa mwaka 1950 Oct katika mkoa wa Pwani Wilaya ya Bagamoyo katika kijiji cha Msoga katika familia ya kisiasa na kilimo. Baba yake Mzee Mrisho Kikwete alikuwa ni Mkuu wa Wilaya (DC) ya Pangani na babu yake naye ambaye alikuwa ni Chief wa Wakwere, Chief Kikwete. Alipata elimu ya Msingi Msoga kabla ya kujiunga na shule ya sekondari Kibaha akiwa pia ni mwenyekiti serikali ya wanafunzi na vijana wa TANU 1966 na Baadaye Tanga school. Ambapo alijiunga na chuo kikuu Dar es salaam, ambapo pia alikuwa mwenyekiti wa serikali ya wanafunzi na kuhitimu Shahada ya uchumi 1975 alipojiunga na Jeshi. Aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa ...

Faiza Ally Awatukana Team Wema.."Team Wema Wengi Wapumbavu - Mimi Siwezi Kupenda Kuwa na Team za Kipumbavu"

Picha
Mrembo wenye Vituko vya kila leo Faiza Ally ameamua kuwafungukia team Wema Sepetu kwa Kuandika Haya: Faizaally_  Team Wema wengi wapumbavu - mimi siwezi kupenda kuwa na team za kipumbavu ! Pumbavu zenu wote ....... Mnaponda watu bila mnazalilisha huyo Malkia wenu nae anaonekana Kama nyinyi ! Kweli mshamba mshamba - mshamba belongs uswahilini bora mngekuwaga hata mna point basi #ujinga mtupu..... Hivi account za kina Malkia Malkia wote wajinga sijui wanatafuta followers kutumia picha za Wema ? But i swear to god nisinge penda kuwa na stupid team at all - Ndio Maana mnafanya anatukanwa - mmeanza kuchokonoa matako ya zari sasa mwisho wameanza na watu kuchunguza yake and u know why ? Because of the stupid team that she has - Kama mm ningewaambia yoyote ana taka kuwa team yangu awe na adabu za kuheshimu wengine Na maisha Yao ! Na yoyote mwenye account ya kutukana watu asitumie picha zangu ! And there for kidogo ange kuwa hata na watu wa manna kabisa hata wa kumwambia ya...

James Lembeli (Chadema ) Aangukia Pua Kesi ya Kupinga Ushindi wa Mbunge wa CCM Kahama

Picha
Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga leo imetupilia mbali maombi ya James Lembeli wa CHADEMA ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini wa Oktoba 25 2015, kwa madai kwamba taratibu zilikiukwa. Akisoma hukumu iliyochukua saa tatu Jaji wa Mahakama hiyo Moses Mzuna amesema ushahidi uliotolewa na upande wa Lembeli haukuwa na nguvu za kutosha kuishawishi mahakama hiyo kutengua matokeo ya uchaguzi kwani sehemu kubwa ni wa maneno. Jaji Mzuna amesema kitendo cha Lembeli kulalamikia vitendo vya rushwa vidavyodaiwa kufanywa na mgombe wa kiti hicho kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jumanne Kishimba kushindwa kuvitolea taarifa kwenye vyombo vya dola kimedhoofisha ushahidi na kuuwekea mashaka.  Kwa upande wa mashahidi waliounga mkono kuwepo kwa vitendo vya rushwa Jaji Mzuna amesema wameshindwa kujenga hoja kwa mlolongo unaofanana kiasi kwamba wameonekana kana kwamba walikuwa na ushahidi wa kutengenezwa. Akitoa hukumu hiyo, Ja...

Mange Amjibu Faiza Ally 'Mimi Mpumbavu Inapokuja Issue ya Wema Ila Nadhani Nilionekana Mpumbavu Mara Mia Wakati Nakutetea Wewe'

Picha
Mangekimambi _ Sawa nakuwa mpumbavu kwenye swala la Wema Ila kumbuka hata wakati nakupigania wewe niliitwa mpumbavu vile vile.Nilitukanwa kona zote kwanini namtetea mwanamke anaevaa pampers na kutembea matako Wazi. Ila sikujali niliacha waniite mpumbavu Kwa ajili yako Na huku sikujui hata kukuona sikuwahi Ila Kwa sababu niliamini in my heart unaonewa niliacha waniite mpumbavu. Leo Na wewe unaniita mpumbavu sababu namtetea Wema Kwa kitu ambacho hata wewe unajua sio sawa? Na ukisoma sijamtetea nimekurekebisha tu kuwa hujakosea ni sawa team Wema ni wapumbavu je kwanini huwasemi hizo team zingine Kwa upumbavu huu? Umemsema Wema hawakanyi team yake je Mbona hujamsema Dai Au Zari kwanini hawakanyi team zao?Lazma tuwe watu wa haki. Hizi team zoooote ni ushuzi mtupu Na ni majipu. Sasa unapochagua team ya kutupia lawama unakosea.. . . Mimi mpumbavu inapokuja issue ya Wema Ila nadhani nilionekana mpumbavu Mara Mia wakati nakutetea wewe na sikujali so kaa ukijua huwa sijalimatusi,...

BAADA YA KILIO CHA MUDA MREFU BARABARA YA KIGOMA-NYAKANAZI KUKAMILIKA MWEZI MEI.

Picha
Makandarasi wanaojenga barabara ya Kidahwe-Kasulu Km 50 na Kibondo-Nyakanazi Km 50 wametakiwa kukamilisha ujenzi huo mwezi Mei mwakani badala ya Novemba ili kuharakisha mkakati wa Serikali wa kuufungua mkoa wa Kigoma kwa barabara za lami. Waziri   hayo mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara hiyo uliyogawanywa sehemu mbili, Kidahwe-Kasulu inayojengwa na China Railway 50 Group na Kibondo-Nyakanazi inayojengwa na Nyanza Road Works. Prof. Mbarawa amewataka makandarasi hao kuongeza kasi ya ujenzi, vifaa na  wafanyakazi wenye sifa ili barabara hizo zikamilike kwa wakati na ubora unaotakiwa. “Tutahakikisha ifikapo Juni mwaka huu tutakuwa tumelipa madeni yote mnayoidai Serikali hivyo fanyeni kazi kwa uhakika kwa kuwa katika kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya Tano tayari tumeshawalipa makandarasi zaidi ya shilingi bilioni 725”, amesema Prof. Mbarawa. Prof. Mbarawa amesisitiza kwamba nia ya Serikali ni kuifungua mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi na Rukw...

PROFESSA J: NAHAMISHIA STUDIO YANGU MIKUMI

Picha
Na Amin Nyaungo Joseph Haule a.k.a profesor Jay amesema atahamisha studio yake ya Mwanalizombe iliyopo Dar es salaam hadi jimboni kwake Mikumi mkoani Morogoro. Akiongea hayo kupitia Clouds fm mbunge huyo wa Mikumi katoa sababu ya kuhamisha jimboni kwake lengo kuu kusaidia wananchi wa jimbo hilo kwani yawezekana kuna vipaji ili wajipatie ajira kupitia studio yake. Amewaomba  watengenezaji wa muziki(producer) waje kutengeneza ngoma kupitia studio hiyo ili kutoa mchango wao kwa wananchi wa mkoa huo. Profesor Jay amesema pia ataongeza na video shooting kwa ajili ya kutengeneza wigo mpana kwa wana kwaya au sherehe na shughuli zote zinazo husu video.

CCM Yatoa Tamko Baada ya Wabunge Wake Kufikishwa Mahakamani Leo Kwa Tuhuma za Rushwa

Picha
Kwa kipindi cha hivi karibunin kumekuwepo na tuhuma za baadhi ya wabunge kujihusisha na masuala ya rushwa. Tuhuma hizo zimekuwa zikifanyiwa kazi na vyombo vya dola na kwamba tayari baadhi ya wabunge wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma hizo. Chama cha Mapinduzi (CCM) kinasikitishwa sana na tuhuma hizo, hasa pale zinapowahusisha wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi  na kinaunga mkono jitihada za vyombo vya dola katika kutafuta ukweli wa tuhuma hizo. Lazima ifahamike kuwa vitendo vya rushwa havina itikadi,dini, wala kabila na kwamba havikubaliki kwa namna yoyote kwani vina madhara makubwa kwa taifa. CCM inavishauri vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa kina na kuwachukulia hatua stahiki wabunge wote watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo vya rushwa. Chama cha mapinduzi kwa upande wake hakitasita kuwachukulia hatua kali za kinidhamu wabunge wake watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo vya rushwa.

ZANZIBAR YAZIDI KUUADHIBU UCHUMI WA TANZANIA, WENGNE WASUSIA KUTOA MISAADA

Picha
Kundi la watoa misaada 10 kutoka nchi za magharibi wametangaza kusitisha ufadhili wao kwa bajeti ya serikali ya Tanzania. Hii inafuatia uamuzi wa shirika la utoaji misaada la serikali ya Marekani kuondoa msaada wa dola 472 wa kufadhili miradi ya maendeleo kutokana na jinsi uchaguzi wa kisiwa cha Zanzibar ulivyoendeshwa. Karibu theluthi moja ya bajeti ya Tanzania ilitegemea msaada mwaka uliopita, kwa hivyo hatua hizo za hivi punde ni pigo kwa mipango ya maendeleo ya serikali mpya.

ZITTO KUWATAJA WATUMISHI HEWA WIZARA YA UJENZI

Picha
Mbunge wa Kigoma mjini kupitia ACT Wazalendo Zitto Kabwe, aitaka Serikali kuwabainisha wafanyakazi hewa kwenye Wizara, baada ya agizo la Rais la kuhakiki watumishi hewa kwenye Halmashauri kutekelezwa. Zitto Kabwe ameandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Facebook, na kuonesha kushangazwa kwa Wizara kutoweka wazi wafanyakazi hewa waliomo humo, huku akijitolea kubainisha wale wa kwenye wizara ya ujenzi. “Watumishi hewa kwenye wizara mbona hatusikii? Wakuu wa mikoa wameagizwa kutambua watumishi hewa. Mawaziri hawakuagizwa. Ok ngoja nijitolee kutambua watumishi hewa wizara ya ujenzi kupitia ripoti za CAG 2010/2011 mpaka 2014/2015”, aliandika Zitto Kabwe. Jana mikoa yote nchini imetekeleza agizo la kuhakiki wafanyakazi hewa walioko kwenye halmashauri zao, huku mkoa wa Mwanza ukiongoza kwa kuwa na wafanyakazi hewa 334.

Waongozaji Video wa nje Wanavyozidi Kuingiza Pesa Kutoka Bongo..Wakina Adamu Juma Wanakosea Nini?

Picha
Muziki wa Tanzania kwa sasa umefanikiwa kuchukua nafasi kubwa Afrika na tayari umeanza kupenya kwenye nchi nyingine duniani. Wasanii wengi wenye menejimenti nzuri yenye uwezo wa kifedha wanaonekana kukimbilia nchi za jirani kufanya video na madirector wa huko, pamoja na kuzitumia location za huko kwenye video zao. Madirector wa bongo kwa sasa wanaonekana kuzikosa fedha nyingi za wasanii. Alianza AY na Jaydee kwenye safari hizo za nje kabla ya Diamond kuunga msafara huo na wengine kufanya msururu huo kuwa mkubwa. Mafanikio ya kwenda huko yameonekana, rangi za video zimekuwa nzuri na baadhi ya video zimeshaanza kupigwa kwenye TV kubwa za nje na kutengeneza connection kubwa. Zipo video zinazopigwa kwenye TV hizo za nje lakini zimetengezezwa na madirector wa ndani kama Hanscana, GQ na wengine. Godfather na Justine Compus ndiyo madirector wanaoongoza kuchukua fedha za wasanii wa bongo kama; Diamond, Navy Kenzo, Joh Makini, Vanessa Mdee, Jux, Shettah na wengi...