Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2018

Mambo ya Kuzingatia Katika Kuchagua Mchumba Mwenzi wa Maisha

Picha
Ikiwa wale wanaokusudia kuoana hawataki kuwa na mashaka mengi wala kuwa na mambo kadha wa kadha ya kuwanyima furaha baada ya kufunga ndoa, imewalazimu kufikiria vyema na kwa moyo wote juu ya jambo hili na kwa wakati huu kabla ya kuoana. Ikiwa hatua hii itafanywa kipumbavu, itakuwa mojawapo ya mambo makuu mno yawezayo kuharibu mafao ya mvulana ama msichana wawapo wamekwisha kuoana. Kwao maisha yataonekana kuwa kama mzigo wa laana. Kaitka ulimwengu huu hakuna awezaye kumnyima mwanamke furaha, ama kumharibia maisha na kufanya yamuelemee na kumchoma moyo zaidi ya mumewe; na hali kadhalika hakuna mwenye uwezo wa kupooza matumaini na jitihada za mwanaume na kuposha nguvu zake, kuharibu mvuto wake na maendeleo yake zaidi ya mkewe. Mara nyingi ni tangu dakika ile baada ya harusi ambapo maisha huanza kuwaelemea wanawake na wanaume wengi. Ndoa ni jambo ambalo lina mvuto katika ulimwengu huu, na litakuwa na mvuto katika ulimwengu ujao pia. Wengi hawaelewi vyema muungano huu wa ndoa. Wengi wao h...

Jina la Ngoma Mpya ya Roma Mkatoliki Lazua Gumzo, Mkewe Ahofia Kumpoteza

Picha
Kila mdau wa muziki nchini Tanzania kwa sasa anahamu ya kusubiri wimbo mpya wa rapa Roma Mkatoliki hii baada ya mkali huyo wa Hip Hop kupitia katika kipindi kigumu cha kufungiwa wimbo wake na yeye mwenyewe kupigwa marufuku ya kutojihusisha na muziki. Sasa habari nzuri ni kwamba jina la wimbo wake mpya ambao unatarajiwa kuachiwa limeshavuja na sio lingine ni  “NIKIFA CHIMBENI MAKABURI MATATU” jina ambalo limevujishwa na mkewe. Mkewe na Roma Mkatoliki, Nancy amesema anajua magumu anayopitia mumewe na anawaza endapo ataachia wimbo huo wa “NIKIFA CHIMBENI MAKABURI MATATU” maisha yake yatakuwaje? kwani ugumu wa mashairi yaliyomo kwenye wimbo huo yanamtia hofu. “Dah Nawazaa Sijui Baba Ataimba Nini Sasa Round hii! Kila Angle Wanakukazia!! Nawaza Ukiachia Ile “NIKIFA CHIMBENI MAKABURI MATATU.“ameandika Mke wa Roma kwenye ukurasa wake wa Instagram. Hata hivyo, Nancy amemshauri Roma asiuachie wimbo huo kwani bado anampenda na anahofia kumpoteza. “Lakini Daaah Bora Ukae Kimya Tu!! Bado...

Hivi Mawakala wa Mabwanyenye Waliosababisha Ndege Yetu Ikamatwe Canada ni Akina Nani?- Tundu Lissu

Picha
Mbunge wa Singida, Tundu Lissu amesema ameona taarifa ya Msemaji wa Ikulu, Gerson Msigwa, kwamba ndege aina Bombardier iliyokuwa imezuiliwa Canada inakuja nchini. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Lissu ameandika baadhi ya mambo ambayo angependa baadhi ya watu wanaodai kuwa alitumwa kipindi cha nyuma alipokuwa anazungumzia kushikiliwa kwa ndege hiyo Canada wafahamu.  ==>>Hii ni kauli yake Nimeona taarifa ya Msemaji wa Ikulu, Gerson Msigwa, kwamba Bombardier yetu iliyokuwa imezuiliwa Canada inakuja. . Kufuatia taarifa hiyo, baadhi ya watu wamedai mitandaoni kwamba kuletwa kwa ndege hiyo ni pigo na aibu kwa mawakala wa mabwanyenye waliosababisha ndege yetu kushikiliwa Canada. Mimi nauliza: Hivi 'mawakala wa mabwanyenye' waliosababisha ndege yetu ikamatwe Canada ni akina nani hasa??? . Here are some basic facts: . 1) Mwaka 2003, kampuni ya Sterling Construction and Engineering Ltd. (SCEL), ilivunjiwa mkataba wake wa ujenzi wa Barabara ya Bagamoyo. Mkataba huo ulivunj...

“Ni Vita Yetu Sote, Tukipata Viongozi Wabaya Tunaumia Wote” -Askofu Chengula

Picha
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mbeya, Evaristo Marc Chengula, amewataka waumini wa kanisa hilo nchini Tanzania kuchagua viongozi sahihi na watakaokidhi mahitaji yao badala ya kufanya makosa kwa kuchagua viongozi wasiofaa na kuanza kulalamika baada ya uchaguzi. Askofu Chengula ametoa ujumbe huo katika mahubiri aliyotoa kwenye ibada ya Ijumaa Kuu inayofanyika katika Kanisa la Bikira Maria wa Fatima Parokia ya Mtakifu Francisco wa Asizi, Mwanjelwa mkoani Mbeya. Amesema imekuwa ni kawaida kwa maaskofu na wadau wengine kuanza kukosoa viongozi baada ya uchaguzi, jambo ambalo halina faida, hivyo wao kama maaskofu mwaka huu wameamua kuwataka waumini wao kuwapima kwa umakini watu wote watakaojitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi zijazo. “Ni vita yetu sote, tukipata viongozi wabaya tunaumia wote, tukipata viongozi wazuri tutafurahi wote, kila mmoja aone kiu ya Tanzania hii kuwa nchi ya upendo,” -Askofu Chengula

Mama Aliyejifungua Mapacha wa Baba Wawili Tofauti Azua Gumzo

Picha
Mama mmoja aliyefahamika kwa jina la Bi, Rashida Nakabugo nchini Uganda, amejikuta akiingia kwenye gumzo kubwa baada ya kutoka kwa vipimo vya vinasaba (DNA) vinavyoonesha kuwa watoto wake mapacha waliyokuwa wakigombaniwa na wanaume wawili kwa zaidi ya miaka mitatu toka kujifungua kwake kila mmoja ana baba tofauti badala ya kuwa wa mtu mmoja kama ilivyozoeleka. Miaka mitatu ya mgogoro wa wanaume hao ambao waliyokuwa wana wapigania mapacha hao waliyofahamika kwa jina la Babirye na Leticia Nakato umemalizwa kwa kila mmoja kupata mtoto mmoja kufuatia matokeo hayo ya vinasaba yaliyotolewa na kituo cha Health Viber Diagnostics huko Kampala nchini Uganda. Vipimo hivyo vya DNA vimeonyesha kuwa, Babirye ni mtoto wa Baseka Sengendo mwenye umri wa miaka 25 mkazi wa Mpigi na Leticia Nakato ni wa Patrick Ssegane mwenye umri wa miaka 30 licha ya kuzaliwa siku moja na mama mmoja. Kwa mujibu wa chombo cha habari cha New Vision kimeeleza kuwa wanaume wote wawili wanaamini kila mmoja ndiye mzazi sah...

Zlatan Ibrahimovic akubali kulipwa mshahara mdogo

Picha
MARA baada ya Zlatan Ibrahimovic kutangaza kusajiliwa na LA Galaxy ya Marekani, wengi wakawa wanajiuliza juu ya malipo ambayo atakuwa akilipwa, lakini imebainika kuwa ni pungufu ya yale aliyokuwa akilipwa alipokuwa Manchester United. Zlatan alikuwa akilipwa euro 21.8m (Sh bilioni 60.5) kwa mwaka lakini sasa atalipwa euro 1.2m (Sh bilioni 3) ikiwa ni pungufu ya asilimia 95 ya kiwango cha mshahara aliokuwa akilipwa, hiyo inamaanisha kuwa atakuwa akilipwa pauni 16,000 (Sh milioni 44) kwa wiki. Kutokana na kanuni za Marekani kuweka kiwango maalum kwa malipo ya mchezaji imelazimika Zlatan akubali kupokea mshahara mdogo lakini utakuwa na posho nyingi.

Utafiti Unaonyesha Jinsi ‘Smartphone’ Zinavyoua Kumbukumbu za Binadamu

Picha
Utafiti mpya kutoka nchini Uingereza unaonesha kwamba ongezeko la simu aina ya smartphone na mitandao ya kijamii linalosababisha tabia wa watu kupiga picha mara kwa mara linasababisha watu kupoteza kumbukumbu. Utafiti huo unaeleza kuwa kupiga picha muda wote kunasbabisha watu kupoteza kumbukumbu ya vitu ambavyo wanaviona na hii ni athari kubwa kwa ustawi wa mtu. Wanasayansi hao ambao wamechapisha utafiti huo kwenye jarida la Journal of Experimental Social Psychology wameeleza kuwa ongezeko la mitandao ya kijamii halijawa tu athari kwa afya za watumiaji bali hata maisha yao ya kawaida.

Mtibwa Sugar: Tunatafuta Matokeo na Tutaitumia Azam Kama Njia ya Kusonga Mbele

Picha
Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila amesema wamejiandaa vilivyo kuhakikisha wanaitumia Azam FC kama njia na kusonga mbele katika mechi yao ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports. Mtibwa Sugar inacheza mechi ya robo fainali ya Kombe la FA kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam na Katwila anaamini wamejiandaa hasa. "Azam wana timu nzuri lakini kweli tumejiandaa sana na tuko Dar es Salaam kutafuta matokeo ya mechi hiyo," alisema. Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na uwezo wa wachezaji wa timu hizo ambao wamekuwa wakiuonyesha katika mchuano hiyo na Ligi Kuu Bara msimu huu. Mshindi katika mechi hiyo ataingia nusu fainali ya michuano hiyo ambayo bingwa wake atapata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika

ROMA, ITALIA: Papa Francis amesema Jehanamu hakuna moto na roho za wasiotubu zitatoweka

Picha
Papa Francis amesema Jahananu haipo! Alipoulizwa wanaokufa na dhambi wanakwenda wapi, akajibu: Wanapotea angani na hakuna adhabu wanayopewa. Does Hell Exist? Pope Francis Says No In New Interview That Could Change Catholic Church Forever Catholic Pope Francis made a startling revelation Thursday by stating that hell did not exist, in an interview with a leading liberal Italian newspaper. In an article entitled "It is an honor to be called a revolutionary,"  La Repubblica  editor Eugenio Scalfari acknowledged the pontiff's previous remarks about how "good souls" who sought repentance from God would receive it and then asked: "What about the bad souls?". Seemingly going against centuries of core Christian belief, Pope Francis said the souls of sinners simply vanished after death, and were not subject to an eternity of punishment. "They are not punished, those who repent obtain the forgiveness of God and enter the rank of souls who con...

Katibu wa Bunge Azungumzia Ajali ya Wabunge 6

Picha
Katibu wa Bunge, Steven Kagaigai amesema chombo hicho cha dola kinafuatilia kwa ukaribu ajali ya wabunge sita iliyotokea jana usiku, Machi 29, 2018 mkoani Morogoro. Kagaigai amesema baada ya kupokea taarifa hizo wamefanya mawasiliano na uongozi wa Hospitali ya Morogoro na walishauriwa kuwahamishia Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya uchunguzi zaidi. “Ndiyo taarifa hizo ninazo, wamepata ajali huko Morogoro, tayari tumeshafanya taratibu za kuwapeleka Muhimbili kwa huduma zaidi na ofisi yetu inawajibika kwa kila hatua,” amesema Kagaigai. Wabunge hao ambao wote ni kutoka Zanzibar ni Haji Ameir Haji (Makunduchi), Khamis Ali Vuai (Mkwajuni), Bhagwanji Maganlal Meisuria (Chwaka), Makame Mashaka Foum (Kijini), Juma Othman Hija (Tumbatu).

Wabunge Sita Walazwa Muhimbili...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya March 31

Picha
Wabunge Sita Walazwa Muhimbili...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya March 31

Mama ajifungua mapacha wenye baba tofauti

Picha
Katika hali ya kushangaza huko nchini Uganda, wanaume wawili na watu wengine wamejikuta kwenye mshangao baada ya kukuta wote wawili ni baba wazazi wa watoto wawili mapacha. Inaelezwa kuwa wanaume hao waliingia kwenye mgogoro siku za hivi karibuni kila mtu aking’ang’ania kuwa baba mzazi wa mapacha hao, na ndipo walipoamua kwenda hospitali ili kupima kipimo cha DNA. Hatahivyo matokea ya daktari yalionesha kuwa wanaume hao wote wawili ni baba halali wa mtoto mmoja wa mapacha hao, yaani kila mmoja ana mtoto mmoja kati ya mapacha hao. Inaeelezwa kuwa wanaume hao Joseph Baseka Sengendo, 25, na Patrick Ssegane, 30, wamezaa na Rashida Nakabugo, ambapo Sengendo anatajwa kuwa mume wa ndoa wa mwanamke huyo. Wanaume hao wanasemekana kuwa ni ndugu.

Musiba Awashambulia Viongozi wa Dini Wanaomshambulia Rais Magufuli

Picha
MWANASIASA aliyekuwa ACT Wazalendo na hivi karibuni kutimkia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Cyprian Musiba ameujibu baadhi ya viongozi wa dini akisema walikuwa wakijipatia pesa kupitia mafisadi na wengine walikuwa wanauza madawa ya kulevya. Musiba amesema kutokana na jitihada za serikali kuwabana mafisadi na wauza unga waliokuwa wakiwapa pesa hizo, baadhi ya vioongozi hao wanaongea maneno ya hovyo kuhusu Rais Dkt. John Magufuli na kutoa matamko ambayo yamekosa tija.

Operesheni Kumg'oa Mugabe Yaibua Mambo Mazito

Picha
Matokeo ya uchunguzi wa Baraza la Taifa la Ukimwi (NAC) na Jeshi la Polisi la Zimbabwe (ZRP), unaonyesha kuwa maofisa wa jeshi la Wananchi wa Zimbabwe wanadai huduma ya ngono bure kutoka kwa wanawake wanaojiuza kama shukrani kwao kwa kusimamia 'Operesheni Rejesha Heshima', Novemba mwaka jana. Uchunguzi huo uliofanywa mwezi uliopita baada ya operesheni hiyo iliyomuweka madarakani, Emmerson Mnangagwa ulilenga kupima uelewa wa maofisa wa polisi, tabia zao na ushiriki wao katika ngono, ushoga na matumizi ya dawa za kulevya. Wakati wa utafiti huo, wanawake hao wanaojiuza waliwalalamikia wanajeshi kwamba baadhi yao wamekuwa wakitumia bunduki kuwatisha, ili wafanye nao ngono bure. "Wanajeshi wamekuwa wasumbufu katika baadhi ya maeneo kwani wanataka ngono bure hasa baada ya kushiriki katika Operesheni ya Kurejesha Heshima,” inasema taarifa ya utafiti huo huku ikitaja matukio kuwa mengi zaidi kutokea katika eneo la Chiredzi.

Duma Aingia Ndani ya Gari la Watalii Serengeti

Picha
Britton Hayes na mjomba wake, wote kutoka Seattle, Washington, walikuwa safarini kujionea wanyama katika mbuga ya taifa ya Serengeti nchini Tanzania pale duma huyu alipoamza kuwa mtalii ndani ya gari lao. Mgeni huyo wasiyemtarajia alikaa ndani ya gari hilo kwa dakika 10 katika eneo la Gol Kopjes la mbuga hiyo, kabla ya mwishowe kuondoka kwenda kuwinda swara. Britton Hayes anasema walikuwa wamemuangazia duma mmoja aliyekuwa ameruka sehemu ya mbele ya gari lao pale mwingine aliporuka na kuingia kupitia sehemu ya nyuma bila wao kumuona. “Tulianza kugundua duma hao walikuwa wameanza kuvutiwa na gari letu; lakini hatukuwa na muda wa kuondoka au kutoroka kwa sababu hutaki kuwashtua wanyama hao, ukifanya hivyo ndivyo mambo huenda mrama,” Hayes aliambia jarida la Komo News. “Nilikuwa nimejawa na wasiwasi sana. Lakini wakati wote nilikuwa nauhisi uhai wangu,” anasema.

Msemaji wa Serikali: Hatujazuia Serikali Kukosolewa, Bali Misingi ya Maadili Ifuatwe

Picha
SERIKALI imesema haijazuia vyombo vya habari kukosoa utekelezaji wa sera, mikakati na programu zake na badala yake imewataka kuzingatia miiko na maadili ya taaluma hiyo yaliyoanishwa na sheria za kimataifa. Hayo yamesemwa jana Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi wakati wa uzinduzi wa Awamu ya 25 ya utafiti wa sauti ya wananchi iliyotolewa na taasisi ya Twaweza. Dkt. Abbasi alisema kumekuwepo na mkanganyiko mkubwa kuhusu dhana  ya uhuru wa habari, hatua inayosababisha baadhi ya vyombo vya habari kuandika na kutangaza taarifa mbalimbali ambazo zimekuwa zikikiuka misingi ya sheria za nchi. “Wapo baadhi ya watu wamekuwa wakifikiri dhana ya uhuru ni kusema chochote na kutumia lugha ya kejeli, hivyo ripoti hii ya utafiti tumeweza kuwa na wataalamu mbalimbali waliokuwa wakitoa mada na kujadili kwa kina misingi na miiko ya uhuru wa habari” alisema Dkt. Abbasi. Alisema kuwa dhana ya uhuru wa habari ...

Kajala Masanja Akana Kutoka Kimapenzi na Chege

Picha
Msanii wa filamu nchini Kajala Masanja amefunguka na kuweka wazi kuhusu tetesi zinazosambaa kuwa sasa anatoka kimapenzi na msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka kiumeni Chege Chigunda. Kajala akiomgea kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio amekana kuhusu kutoka kimapenzi na msanii huyo na kudai kuwa hakuna jambo kama hilo na "Mama yangu mzazi hakuna kitu kama hicho si mmeona Chege kapata mtoto juzi tu hapa, yaani mimi sina hata namba yake ya simu na haiwezi kutokea kitu kama hicho"alisisitiza Kajala Mbali na hilo Kajala amewatakia kheri wanawake wote maarufu ambao wanakaribia kuolewa siku za karibuni na kusema kwake yeye badobado kwani anaamini mume mwema anatoka kwa Mungu hivyo atakapompata huenda na yeye ndiyo akafanya maamuzi hayo ya kuolewa sasa.

Mkuu wa Jeshi, Waziri wa Mambo ya Ndani Kenya Wahukumiwa Kwa Kuidharau Mahakama Sakata la Miguna

Picha
Mahakam nchini Kenya imewapiga faini waziri wa mambo wa mambo ya ndani Fred Matiang'i na mkuu wa jeshi la polisi Joseph Boinnet baada ya wawili hao kudharau amri yake kuhusu kumuachia mwanasiasa wa upinzani Miguna Miguna Waziri wa mambo ya ndani wa Kenya na Inspekta Janerali Mkuu wa Polisi wamepigwa faini kwa kuidharau mahakam siku ya Alhamisi, kwa kushindwa kutii agizo la jaji kumuachia mwanasiasa wa upinzani, katika hukumu iliochochea zaidi mgogoro kati ya mihimili miwili ya dola. Jaji wa mahakama Kuu George Odunga amesema maafisa hao wawili waandamizi serikalini "walidhihirsha tabia isiyotarajiwa katika zama hizi za kikatiba," - katika ukaripiaji usiokifani kwa maafisa wa juu serikalini. Waziri wa mambo ya ndani Fred Matiang'i, na inspekta Jenerali Mkuu wa Polisi Joseph Boinet wametozwa kila mmoja shilingi za Kenya 200,000, sawa na dola za Marekani 1,985, kutokana na ushiriki wao katika kumzuwia mwansiasa wa upinzani Miguna Miguna wiki hii. Mahakama nchini Ken...

Jeshi la Polisi latoa onyo kwa Madereva kipindi cha Sikukuu

Picha
JESHI la Polisi mkoani Pwani limewaasa madereva hususani wa mabasi yanayofanya safari za mikoani ,kuacha kufanya mbwembwe wakati wakiwa barabarani na kutumia vileo katika kipindi hiki cha sikukuu za Pasaka ili kuepusha ajali zembe. Aidha jeshi hilo limetoa onyo kali kwa wale wenye nia ya kutenda uhalifu kwenye kipindi hicho . Akizungumza na waandishi wa habari na baadhi ya maofisa wa jeshi hilo ,kuhusiana na operesheni za kaguzi hizo ambazo ni endelevu ,na kutoa salamu za Pasaka ,kaimu kamanda wa polisi ,mkoani Pwani ,(SSP) Abdi Issango ,alisema madereva wafuate sheria za usalama barabarani bila kushurutishwa . Amesema wanafanya operesheni ya kukagua madereva wa mabasi hayo na kufanikiwa kuwakamata madereva 29 kwa makosa ya mwendo kasi na kulipita gari la mbele sehemu isiyoruhusiwa (wrong overtaking). Pamoja na hayo ,Issango alielezea madereva 22 walikamatwa kwa kosa hilo na madereva saba walikamatwa kwa kosa la mwendo kasi . Alibainisha dereva mmoja alipewa onyo kutokana na kosa...

Urusi Nayo Imejibu Mapigo.....Wanadiplomasia 60 wa Marekani Watimuliwa, Ubalozi Wafungwa

Picha
Urusi imewafukuza wanadiplomasia 60 wa Marekani, na kufunga ubalozi uliopo St Petersburg ikiwa ni majibu kwa kitendo cha Marekani kuwafukuza wanadiplomasia wa Urusi juu ya shutuma ya Uingereza kuhusu kuhusika kwa Urusi katika shambulio la jasusi wa zamani wa Urusi Sergei Kripal na binti yake huko Uingereza. Hatua hiyo ilitangazwa na waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov. Zaidi ya nchi ishirini zimewafukuza wanadiplomasia wa urusi nchini mwao katika kuunga mkono Uingereza. Miongoni mwa nchi hizo ni Marekani ambapo mapema wiki hii iliwatimua wanadiplomasia 60 wa urusi kuondoka Marekani. Katika kujibu hilo Urusi imewatimua wanadiplomasia 58 kutoka Moscow na wawili kutoka mji wa Yekaterinburg, chombo cha habari cha Interfax kiliripoti. Lavrov alisema kuwa nchi nyingine zilizowafukuza Warusi wasubiri majibu kwa vitendo. Ameongeza kuwa Ubalozi wa Marekani umepewa taarifa juu ya hatua hiyo kama majibu kwa Marekani kwa kuwatimua wanadiplomasia wake na kusimamisha ubalozi ulioko S...

Fahamu jinsi ya kupata watoto Mapacha kila mwanamke anaweza kupata

Picha
Siku ya leo naomba tujifunze elimu mpya kabisa ya uzazi ambapo mwanamke yeyote anaweza kupata ujauzito wenye watoto mapacha hata kama si asili ya ukoo wake, ambavyo wengi wanavyosema. Nimetumia neno ‘mwanamke yeyote’ kwa sababu kuna imani ya miaka na miaka kwamba, si kila mwanamke anaweza kupata ujauzito bali itategemea na asili yake. Imani ya kale kuhusu ujauzito Baadhi ya mila na desturi, hasa katika nchi za Kiafrika zinaamini kwamba, mwanamke kupata watoto mapacha kunatokana na urithi wa kizazi chake, kuanzia mababu wa upande mmoja kati ya wanandoa hivyo uzao huo hufuata mkondo kwa miaka na miaka. Wengi wakipata mapacha huulizwa kama kwenye kizazi chake, kuna watoto mapacha. Akitokea mama akasema hakuna, basi huaminika kwamba lazima upande wa mwanaume kuna waliowahi kuzaliwa mapacha hata kama si katika miaka ya karibuni. Imani hii ni ya kizamani sana, ukweli ni kwamba mwanamke yeyote mwenye sifa ya kushika mimba na kuzaa, anaweza kupata ujauzito na kuzaa mapacha bila kujali ...

KAMATI YA UTEKELEZAJI YA UVCCM MKOA WA MJINI YAKUTANA NA VIJANA WA VYUO

Picha
Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Mkoa wa Mjini ikiongozwa na Mwenyekiti wake Ndugu Kamaria Suleiman Nassor leo tarehe 29.3.2018 imefanya ziara na kukutana na wanafunzi wa Chuo cha Mwenge Community Center wa kozi za Nursing,Uandishi wa HABARI,Ufundi Umeme na Ushonaji. Katika ziara hiyo wanachuo wameimizwa kuwa Wazalendo kwa nchi yetu na kuwafichua wale wote wanaojihusisha na vitendo vya udharirishaji watoto. Pia wanachuo walikumbushwa historia ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ambayo yaliasisiwa na Hayati Shekhe Abeid Aman Karume na mafanikio yaliyopo chini ya Serikali zinazoongozwa na CCM. Katika ziara hiyo wanachuo walizungumzia changamoto zinawakabili ambazo zilichukuliwa na uongozi wa UVCCM kwa hatua zaidi. Baada ya hotuba kumalizika wanachuo 50 wa MCC wameomba kujiunga na UVCCM na tayari wamelipia gharama za kiingilio na ada. Mipango ya kutoa kadi kwa vijana hao inaendelea kwa kufuata taratibu kwa mujibu wa Kanuni ya UVCCM. #TUKUTANE KAZINI Imetolewa na: Joel L....

Mbowe na Viongozi Wenzake Kula Sikukuu ya Pasaka Gerezani

Picha
Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Wilbard Mashauri amesema baada ya kusikiliza hoja zilizowasilishwa na upande wa Serikali na utetezi katika kesi inayowakabili viongozi wa Chadema, akiwemo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe washtakiwa hao wafikishwe mahakamani hapo Aprili 3, 2018. Amesema siku hiyo washtakiwa watasaini bondi ya Sh20 milioni na wakiwa huru ndipo utaratibu wa kukata rufaa wa upande wa mashtaka utafanyika.     “Nikitoa dhamana wakati washtakiwa hawapo haina maana zoezi zima lisimame.Leo washtakiwa hawajafikishwa mahakamani na nimetoa masharti ya dhamana, hivyo kutoa dhamana na  washtakiwa wakiwa bado hawajasaini ilo zoezi bado halijakamilika. “Hivyo kwenye hatua ya sasa ni mapema mno kwa upande wa mashtaka kuwasilisha hoja za kukata rufaa wakati bado mchakato haujakamilika. “Mahakama inatoa remove order waje mahakamani April 3,2018 na wadhamini wao ili waje kukamilisha masharti ya dhamana.”  A...

Zifahamu Hatari Kuu Zilizojificha Ndani ya Bafu Lako

Picha
Watafiti katika nchini Uingereza wanasema kuwa usafi wa bafuni ni jambo linalofaa kuzingatiwa kuliko wengi wanavyodhania.  "Bafu ni mahali ambapo usafi wake huwa ni mgumu'' "Watu hutumia muda wao katika kusafisha vyoo vyao lakini ingelikuwa vyema kama kila mtu angezingatia zaidi usafi wa bafu kwa kutumia madawa ya kuuwa bakteria." 1.Kuoga kwa kutumia kifaa cha kukumwagia maji mwilini kwenye bafu za manyunyu Wataalamu wanasema unapotumia kifaa hiki kwenye bafu za manyunyu hunabudi kuwa makini sana, kwani kinapotumika baada ya kuzimwa kwa muda mrefu na kutumiwa tena hugeuka kuwa makao ya vimelea vya bakteria. Hatari nyingine kwa watu wazima na watoto itokanayo na kifaa hicho (shower) ni uwezekano wa kuunguzwa na maji yanayotoka kwenye kifaa hiki ambacho kinaweza kuwa moto sana na kuuchoma mwili. Msemaji wa kituo cha utafiti Rospa ameiambia BBC: " Tunawaomba watu kuweka maji baridi kwanza ndani ya beseni/ vidimbwi vya maji ya kuoga kwa ajili ya watoto . ...

Ireland Kuhalalisha ‘Utoaji Mimba’ kwa Kura

Picha
Nchi ya Ireland ambayo ni ya misingi ya kidini hususani kwa dhehebu za Kikatoliki, suala la utoaji mimba kwa miaka mingi limekuwa haramu hata kama ni kwa kesi za kidaktari. Kutokana na marufuku hiyo ya kisheria wanawake wamelazimika kwa kipindi chote kwenda kutibiwa nchi za nje endapo madaktari watasema inabidi watolewe mimba hizo kutokana na kuhatarisha maisha yao . Hali hii imeanza kubadilika ambapo wanaharakati kwa miaka wameshinikiza kufutwa kwa sheria hii na kuhalaisha utoaji wa mimba kwa wanawake, na jana March 28, 2018 Waziri wa Afya nchini humo Simon Harris amezungumza. Waziri huyo ameeleza kuwa May 25, 2018 itapigwa kura ambayo ndiyo itatoa hatima ya kuhalalishwa kwa sheria mpya ya utoaji wa mimba nchini humo baada ya miaka 35 au la.

CAG Aomba Radhi Wananchi Juu ya Taarifa ya Deni la Taifa Aliyompa Rais Magufuli "Yalikuwa Makosa ya Kimatamshi Deni ni Himilivu"

Picha
Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali Profesa. Mussa Assad ameomba radhi wananchi na serikali juu ya taarifa ya deni la taifa na kusema kuwa yalifanyika makosa ya kimatamshi deni hilo ni himilivu. Profesa Assad ametoa taarifa hiyo mjini Dodoma ambapo amesema deni halisi ni shilingi trillion 46.08 na ni himilivu hivyo anaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kwa wananchi na taasisi za serikali. "CAG anapenda kutoa ufafanuzi kuhusu kauli yake aliyotoa kuhusiana na mwenendo wa na ukuaji wa deni la taifa kama alivyonukuliwa wakati akitoa ripoti hizo kwa Mhe. Rais Magufuli taarifa sahihi kuhusu mwenendo wa deni ni kwamba kwa kujibu wa taarifa ya maandishi wa CAG hadi kufikia tarehe 30 Juni 2017 deni la taifa lilikuwa ni trilioni 46.08 katika deni hilo deni la ndani ya trilioni 13.34 sawa na asilimia 16 na deni la nje nu trilioni 37.75 ambayo ni sawa na asilima 71, kwa hivyo utafiti umebaini kuwa deni la taifa kwa sasa ni himilivu" CAG wakati akitoa ripoti hiyo kwa Rais...

Mahakama ya Kenya Yawahukumu Waziri, IGP na Mkuu wa Uhamiaji Kisa Mugina

Picha
Mahakama nchini Kenya imewahukumu Waziri Fred Matiang'i, Mkuu wa Uhamiaji Gordon Kihalangwa na IGP Joseph Boinnet kulipa faini KSh200,000 (Sh4.4m) kwa kosa la kuidharau mahakama Jaji wa Mahakama Kuu George Odunga Jumatano alisema waziri wa usalama nchini humo, mkuu wa polisi na mkuu wa idara ya uhamiaji watakuwa wamekaidi maagizo ya mahakama iwapo wangekataa kumwachilia huru. Alikuwa ametoa ilani kwa watatu hao kufika mahakamani baadaye Jumatano lakini baada yao kukosa kufika akawapata na hatia ya kukaidi agizo la mahakama.

Mahakama Yatoa Masharti ya Dhamana kwa Mbowe na Viongozi Wengine wa CHADEMA

Picha
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa masharti ya dhamana kwa viongozi 6 wa CHADEMA akiwemo Freeman Mbowe kwa kuwa na wadhamini 2 kila mshtakiwa atakayesaini Bondi ya Shilingi Milioni 20. Pia wadhamini hao wawe na barua za utambulisho, ambapo baada ya kutimizwa masharti hayo Mbowe na wenzake wawe wanaripoti Central Police mara moja kwa wiki. Wakili wa serikali, Faraja Nchimbi ameieleza Mahakama ya Kisutu kuwa watakata rufaa kupinga uamuzi wa mahakama hiyo kutoa masharti ya dhamana kwa Mbowe na wenzake

Kimenuka! Dili la Zali Lawagombanisha Shamsa Ford na Faiza

Picha
Baada ya hapo jana aliyekuwa Baby Mama wa Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady kupata dili la kuwa balozi wa bidhaa za Softcare Diapers, mjadala umekuwa mkubwa ni kwanii mastaa wa kike Bongo hawapati fursa kama hizo. Muigizaji Faiza Ally alihoji ni kwa nini mastaa wa Bongo hawajapata dili hilo badala yake akapewa mtu mwingine, Faiza alienda mbali zaidi kwa kusema Wakenya na Waganda hawezi kufanya kitu kama hicho. Sasa Shamsa Ford amepigana na mtazamo wa Faiza kwa kueleza kuwa mastaa wa kike Bongo wamejiharibia wenyewe ingawa wanajulikana lakini si kwa upande ambao unavutia kibiashara. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika; Naona tu watu wanalalamika kwanini madili yanawapita mastar wa bongo na wageni ndo wanapata nafasi hiyo. Mimi nina mtazamo tofauti kabisaa, kabla ya kuanza kumtafuta mchawi ni nani ni bora kwanza tukajikagua wenyewe kwanza, nina uhakika kila biashara ina condition zake na kila biashara inahitaji faida. Hakuna mfanyabiashara atayekubali kumchukua STAR wa bo...

Makonda Atoa Zawadi ya Vifaa vya Kujifungulia kwa Wajawazito Watakaojifungua Pasaka

Picha
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo ametoa zawadi ya vifaa tiba vya Mama mzazi kwaajili ya kujifungulia (Delivery Packs) 200 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi million 20 Kama zawadi yake ya sikukuu ya pasaka kwa kinamama watakaojifungua kwenye msimu huu wa pasaka. Gharama ya mfuko mmoja (package) ya Vifaa hivyo vya kisasa ni Shilingi laki Moja ambapo ndani yake kuna Mashuka, Vitambaa, Dawa, Mabomba ya Sindano, Pamba, Kibanio cha kitovu, Nyuzi, pedi za kinamama, Dawa ya kuzuia upotevu wa damu, Nyembe na Gloves ambapo vitatolewa Bure kwa Mama mzazi atakaejifungua msimu huu wa pasaka kwenye vituo vya Afya na zahanati zilizopo kwenye Wilaya Tano za Mkoa huo. Makonda ametoa vifaa hivyo baada ya kubaini changamoto ya baadhi ya kinamama kushindwa kumudu gharama ya vifaa vya kujifungulia na kujikuta wanatumia kanga au nguo jambo ambalo ni hatari kiafya kwa mama na mtoto. Akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Makonda kwa waganga wakuu wa halmashauri na wasimamizi wa vituo na Zah...

Jux Afunguka Sakata la Ujauzito wa Vannessa

Picha
Msanii wa muziki BongoFleva Juma Jux ambaye yuko kwenye mahusiano ya kimapenzi na Vanessa Mdee, amekanusha taarifa za mpenzi wake huyo kuwa mjamzito na kudai kwa sasa hawajajipanga kufanya hivyo ila endapo watakuwa tayari kwa hilo watasema. Jux ameeleza hayo wakati alipokuwa anahojiwa na moja wapo ya chombo cha habari nchini Tanzania baada ya kuenea picha ya mpenzi wake Vanessa mitandaoni ikiwa inamuonesha tumbo lake limeja jaa mithiri ya ujauzito. "Kiukweli Vanessa hana ujauzito ile ni picha tu, labda siku hiyo alikuwa ametoka kula 'ameshiba' na kupigwa picha vibaya ndio ikatokea hivyo. Lakini hakuna kitu kama hicho, hivyo vitu inabidi viende kwa mipango pia lazima mwenzako umshirikishe endapo unataka kufanya hivyo na mkubaliane ili mambo yaweze kwenda sawa", amesema Jux. Pamoja na hayo, Jux ameendelea kwa kusema "ikifika 'time' watu watajua kwasababu sisi hatuwezi kuficha mambo hata kama sisi hatuto-post lakini inaweza akaja ku-post mtu mwingine kwa...

Haya Hapa Ndio Makosa ya Mwanaume Yanayosababisha Mke au Mchumba Amsaliti

Picha
Kuna sababu anuai zinazomfanya mwanamke amsaliti mumewe. Ni muhimu kutambua kuwa mwanamke ni kiumbe mwenye hisia kali na daima ahisi raha na amani. Baadhi ya nyakati hufanya usaliti ili kuziba pengo la upungufu unaotokea katika maisha yake. Zifuatazo ni sababu kubwa ambazo zinamfanya amsaliti mumewe: 1. KUTOMPA KIPAUMBELE NA KUTOMTHAMINI Tunatambua kuwa mke anafanya kazi kubwa sana ambayo lau kama ingekuwa ni kampuni basi pangehitajika watu zaidi ya 10 kuzifanya. Atamtunza mume, watoto, nyumba na familia kwa ujumla. Wakati fulani mume anaweza akampuuza na asimthamini, licha ya kujitoa kwa moyo wote kumtunza na kuihudumia familia. Hivyo, kutotoa kipaumble kwa mke ni kosa kubwa ambalo linaweza likamgharimu mume, mke akipata mtu anayempa kipaumbele na kumuonesha thamani hakika hataacha kuitumia hiyo fursa. 2. UKOSEFU WA MAHABA Kwa asili mwanamke ana silika ya hitajio la kupendwa, mwanamke anahitaji kupendwa, mwanaume yeye ana silika ya kupenda ngono, ukimpa ngono tu basi anaridhika....

Wafuasi wa Chadema Waliamsha Dude Mahakamani

Picha
IKIWA ni saa 48 zimepita tangu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na viongozi wenzake watano wa chama hicho kupelekwa katika mahabusu ya Segerea baada ya kunyimwa dhamana katika kesi yao waliyosomewa juzi Machi 27, Katika Mahakama ya Kisutu Dar, wafuasi wa chama hicho waliofurika mahakamani hapo wamezua sintofahamu baada ya kufanya vurugu wakipiga makelele na kuimba wakitaka haki. Wafuasi hao waliokuwa nje ya geti la mahakama hiyo wakiwa wamekusanyika baada ya Jeshi la Polisi kuwazuia kuingia mahakamani kusikiliza kesi ya viongozi hao walianza kupiga makelele wakiimba ‘hatupoi hatupoi, tunataka haki tunataka haki’, hali iliyowalazimu polisi kutia kambi eneo hilo na kuimarisha ulinzi kuhakikisha hakuna uvunjifu wowote wa amani unafanyika. Kesi hiyo ilitarajiwa kuendelea tena leo Machi 29, ili kufanya jitihada za kupata dhamani. Viongozi wengine waandamizi wa Chadema wanaoshtakiwa katika kesi hiyo ni: Vicent Mashinji, John Mnyika, Peter...

Kesi ya Kutoa Lugha ya Fedheha Dhidi ya Rais Magufuli Inayomkabili Halima Mdee Yapigwa Kalenda

Picha
Kesi ya kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli inayomkabili mbunge wa Kawe, Halima Mdee leo March 29, 2018 imeshindwa kuendelea baada ya mshtakiwa kuwa mgonjwa. Kesi hiyo imeshindwa kuendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na mshtakiwa huyo kuwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu. Mdee anakabiliwa na shtaka moja la kutoa lugha ya matusi dhidi ya Rais,  kwa kusema, “anaongea hovyo hovyo, anatakiwa afungwe breki” kitendo ambacho kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani. Wakili wa Serikali, Patrick Mwita amedai hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati shauri hilo lilipokuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi. “Kesi hii imekuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi na tayari upande wa mashtaka tunaye shahidi hapa mahakamani, lakini nimepata taarifa kuwa mshtakiwa ni magonjwa na ameshindwa kufika mahakamani hapa,” -Wakili Mwita. Baada ya kueleza hayo, wadhamini wa Mdee, Fares Robison ambaye ni Diwani wa Mbezi Juu na M...

TWAWEZA :zaidi Ya Nusu Ya Watanzania Hawajisikii Huru Kumkosoa Rais,makamu Wa Rais Na Waziri Mkuu

Picha
Idadi kubwa ya wananchi hawajisikii huru kumkosoa Rais (60%), Makamu wa Rais (54%) na Waziri Mkuu (51%).  Karibu nusu ya wananchi pia hawajisikii huru kuwakosoa mawaziri (47%), Wakuu wa Mikoa (46%) na Wakuu wa Wilaya (43%).  Hata hivyo, idadi kubwa ya wananchi (87%) wanasema wanapaswa kuwa huru kuikosoa serikali na Rais kwa kufanya maamuzi mabaya na kutosikiliza ushauri (80%).  Wanaamini kupitia ukosoaji wanaweza kuisaidia serikali kutofanya makosa (81%) na si kuwashushia hadhi watendaji wa umma au kuhatarisha umoja (19%).  Vilevile wananchi hawaungi mkono matumizi ya lugha ya matusi ambapo asilimia 71 ya watanzania hawataki wananchi waruhusiwe kuwaita wafuasi wa chama chochote cha siasa “wapumbavu au malofa”. Matokeo haya yametolewa na Twaweza katika muhtasari wake uitwao Siyo kwa kiasi hicho? Maoni ya wananchi kuhusu taarifa na mijadala. Takwimu za muhtasari huu zinatokana na utafiti wa Sauti za Wananchi ambao huratibiwa na taasisi ya Twaweza....