Zlatan Ibrahimovic akubali kulipwa mshahara mdogo

MARA baada ya Zlatan Ibrahimovic kutangaza kusajiliwa na LA Galaxy ya Marekani, wengi wakawa wanajiuliza juu ya malipo ambayo atakuwa akilipwa, lakini imebainika kuwa ni pungufu ya yale aliyokuwa akilipwa alipokuwa Manchester United.

Zlatan alikuwa akilipwa euro 21.8m (Sh bilioni 60.5) kwa mwaka lakini sasa atalipwa euro 1.2m (Sh bilioni 3) ikiwa ni pungufu ya asilimia 95 ya kiwango cha mshahara aliokuwa akilipwa, hiyo inamaanisha kuwa atakuwa akilipwa pauni 16,000 (Sh milioni 44) kwa wiki.

Kutokana na kanuni za Marekani kuweka kiwango maalum kwa malipo ya mchezaji imelazimika Zlatan akubali kupokea mshahara mdogo lakini utakuwa na posho nyingi.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: UTAMU WA MADAM JESCA

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU

SIMULIZI FUPI: UCHI WANGU UMENIPONZA