Mahakama ya Mwanzo Usambara mkoani Tanga imemhukumu kwenda jela miezi mitatu Swabaha Shosi ambae alishawahi kushika headlines kwa kulia mbele ya Rais Magufuli wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria February 2, 2017.
Hakimu wa Mahakama hiyo Khadija Kitogo amemtia hatiani kwa kuingia eneo lisiloruhusiwa kisheria.
Swahaba alifikishwa Mahakamani hapo August 9, 2017 akikabiliwa na shtaka la kuingia Chongoleani ambako hakuruhusiwi Raia kuingia.
Mahakama ilielezwa kuwa aliingia katika eneo lililokuwa limetengwa kwa ajili ya ujio Rais Magufuli na Yoweri Museveni walipokwenda kuzindua mradi wa bomba la mafuta kutoka Uganda mpaka Hoima.
Swahaba alikana mashtaka hayo na kujitetea kuwa alikanyaga eneo wakati akiandaa eneo kwa ajili ya kuwauzia chakula waliodhuria uzinduzi huo na kwamba hakuwa peke yake walikuwa wengi.
Hakimu Kitogo akitoa hukumu hiyo amesema baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote mahakama imemkuta na hatia ya kuvunja sheria ya Makosa ya jinai.
“Ninampa adhabu ya kwenda jela miezi mitatu ili iwe fundisho kwa wengine wanaovunja sheria kwa kuingia maeneo yasiyoruhusiwa”