Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Mkoa wa Mjini ikiongozwa na Mwenyekiti wake Ndugu Kamaria Suleiman Nassor leo tarehe 29.3.2018 imefanya ziara na kukutana na wanafunzi wa Chuo cha Mwenge Community Center wa kozi za Nursing,Uandishi wa HABARI,Ufundi Umeme na Ushonaji.
Katika ziara hiyo wanachuo wameimizwa kuwa Wazalendo kwa nchi yetu na kuwafichua wale wote wanaojihusisha na vitendo vya udharirishaji watoto.
Pia wanachuo walikumbushwa historia ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ambayo yaliasisiwa na Hayati Shekhe Abeid Aman Karume na mafanikio yaliyopo chini ya Serikali zinazoongozwa na CCM.
Katika ziara hiyo wanachuo walizungumzia changamoto zinawakabili ambazo zilichukuliwa na uongozi wa UVCCM kwa hatua zaidi.
Baada ya hotuba kumalizika wanachuo 50 wa MCC wameomba kujiunga na UVCCM na tayari wamelipia gharama za kiingilio na ada.
Mipango ya kutoa kadi kwa vijana hao inaendelea kwa kufuata taratibu kwa mujibu wa Kanuni ya UVCCM.
#TUKUTANE KAZINI
Imetolewa na:
Joel L.K.Makwaia
Katibu wa UVCCM
MKOA WA MJINI-UNGUJA
29 Machi 2018

