SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 29 Machi 2018

T media news

KATA 33 ZA WILAYA YA BUNDA ZAHITIMISHA ZIARA YA MWENYEKITI WA UVCCM WILAYA KWA KISHINDO JIMBO LA BUNDA MJINI



March 28,2018

Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Bunda *Ndg Gasper Charles* akiambatana na Katiba wa UVCCM Wilaya *Ndg Steven E. Shija* wamehitimisha ziara yao kwa Kata 33 za Wilaya ya Bunda Katika Kata ya Guta na Bunda Mjini

Katika Kata ya Guta Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya alipokutana na Baraza Maalumu la UVCCM Kata, alipokea Vijana wapya 20 kuwa Wanachama wapya wa UVCCM baada ya kuona UVCCM ikishughurika na Changamoto za Vijana

Pia Katika Kata ya Bunda Mjini Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya, akiambatana na Viongozi Mbalimbali walitembelea shughuri ya Ujenzi wa Mitaro kuboresha Barabara za Mjini, ambapo Mwenyekiti na Viongozi wote walishiriki Katika Ujenzi huo kuonesha kuunga Mkono jitihada za Serikali kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM

Vilevile Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya alipokea Wanachama wapya kutoka CHADEMA, walioamua kuungana na Vijana wa CCM kulinda Amani ya Taifa lao na kushirikiana na Serikali katika kuwaletea Wananchi wa Bunda maendeleo

_"Tumeona Juhudi za UVCCM kuwatetea Vijana Wanyonge, kuleta Umoja kwa Vijana wote kujiinua Kiuchumi, kulinda Amani ya Taifa letu na kuhakikisha Serikali inateakeleza Ilani ya CCM kwa vitendo, tumeona tukate Shauri tujiunge kuijenga Bunda yetu pamoja"_ alisema Petro Charles aliyewahi kuwa Red brigade wa CHADEMA na Mwanachama

_"Tunawapongeza Vijana wote mliochukua maamuzi ya kuungana na Jumuiya yetu kuleta Mabadiliko chanya, tunawaahidi ushirikiano wa Karibu ili tufikie mafanikio ya Pamoja kama Vijana"_ alisema Gasper

Kata hizo mbili zimehitimisha ziara ya kwanza na Kihistoria Katika Wilaya ya Bunda yenye Kata 33 na Majimbo Matatu ya Uchaguzi

Mwisho, Katibu aliwakumbusha Viongozi wa Chama kuwapa Ushirikiano Viongozi wa Jumuiya zote maana wao ndiyo Walezi, na aliwasihi kuwalea Vijana wote kwenye Misingi mathubiti ya CCM


        *TUPO KAZINI*

*Imetolewa na :-*
*Ndg S.E.Shija*
*Katibu wa UVCCM Wilaya*
*Bunda, Mara*