Mahakama ya Kenya Yawahukumu Waziri, IGP na Mkuu wa Uhamiaji Kisa Mugina


Mahakama nchini Kenya imewahukumu Waziri Fred Matiang'i, Mkuu wa Uhamiaji Gordon Kihalangwa na IGP Joseph Boinnet kulipa faini KSh200,000 (Sh4.4m) kwa kosa la kuidharau mahakama

Jaji wa Mahakama Kuu George Odunga Jumatano alisema waziri wa usalama nchini humo, mkuu wa polisi na mkuu wa idara ya uhamiaji watakuwa wamekaidi maagizo ya mahakama iwapo wangekataa kumwachilia huru.

Alikuwa ametoa ilani kwa watatu hao kufika mahakamani baadaye Jumatano lakini baada yao kukosa kufika akawapata na hatia ya kukaidi agizo la mahakama.