Viongozi sita wa Chadema wamefikishwa leo saa 2 asubuhi katika Mahakama ya Kisutu kwa ajili ya kusikiliza uamuzi wa dhamana yao, huku ulinzi ukiimarishwa katika eneo hilo.
Kesi hiyo inatajwa leo Machi 29, ambapo Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard, Mashauri atatoa uamuzi kama washtakiwa hao watapata dhamana au hawatapata.
Wakati viongozi hao wakifikishwa mahakamani, Jeshi la Polisi limeimarisha ulinzi kuzunguka viunga vya mahakama ya Kisutu.
Katika lango kuu la kuingia mahakamani hapo, polisi waliovalia kiraia walifanya ukaguzi kwa kila anayeingia na kutoka na kuwazuia