Muigizaji wa Bongo movie Salma Jabu maarufu kama Nisha ameendelea kuwa kwenye Headlines baada ya kuzidi kuonekana kwenye mapozi ya kimahaba na Mwanaume aliyewahi kutoka kimapenzi na muigizaji Wolper.
Wawili hawa wamekuwa wakionekana mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii lakini wanapotafutwa kuzungumzia hilo wamekuwa hawatoi ushirikiano wakutosha, sasa leo March 27, 2018 muigizaji huyo ameendelea kuweka video ikimuonesha waki-kiss na Brown kitu kilicho endelea kuwa Gumzo mtandaoni.
Nisha amepost video hiyo na kuandika ujumbe huu….>>>“kitu pekee tunachohitaji ni FURAHA ila mara nyingi tunaangukia kwny VILIO vya kujitakia. washauri wa mapenzi ni wengi ila unahisi unaweza kunishauri wa kuwa naye wkt tayari moyo wangu upo sehemu fulani.
“Ila kabla hujanihukumu mimi Nishabebe au Brown je USHAWAHI KUUMIZWA? hadi ukayachukia mapenzi na kutamani uwe #BACHELA miaka yote? kama jibu ni ndio USIHUKUMU kitabu kwa cover la nje. kama jibu ni HAPANA endelea kutupa madongo yanatukomaza kiakili. wacha nikwambie siri NASOMA COMMENT zote na yule BUBU BADO HAJAONGEA” – Nisha