Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2016

RAIS MAGUFULI AFUNGA MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA JWTZ ASHUHUDIA ZOEZI LA AMPHIBIOUS LANDING BAGAMOYO

Picha
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na meza kuu wakipiga saluti wakati wa wimbo wa Taifa wakati wa kufunga Zoezi la medani katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba 30, 2016. Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akipiga ngoma za bendi ya jeshi ya Mwenge Jazzz wana Paselepa wakati wa kufunga Zoezi la medani katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba 30, 2016 Ndege vita zikipita angani katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba 30, 2016 Vifaru vinavyopita baharini na nchi kavu vikiwa katika zoezi la "Ambhibious Landing" katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baat...

MAPOKEZI ya Maalim Seif Buguruni yaota mbawa

Picha
Mapokezi makubwa yaliyopangwa kufanyika leo  jijini Dar es salaam ya kuwapokea Wajumbe wa Baraza Kuu la CUF na  Kamati ya Uongozi ya chama na Katibu Mkuu Maalim Seif yameota mbawa kufuatia kusitishwa  kwa hofu ya kutokuwepo usalama. Mapema jana, ilitangazwa kwamba Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, wajumbe wa baraza kuu la CUF na kamati ya uongozi ya chama wangefanyiwa mapokezi makubwa katika ofisi hizo lakini yaliahirishwa ghafla baadaye usiku kwa kuhofia kuwapo vurugu. Kiongozi wa wabunge wa CUF waliokuwa wameandaa mapokezi hayo, Riziki Shahari alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa wameahirisha mapokezi hayo baada ya kujiridhisha kuwa hali ya usalama siyo nzuri. “Tunazo taarifa kuwa yapo makundi hatari ya watu yanayoishi ndani ya ofisi huku yakilindwa na vyombo vya dola tangu ofisi hiyo iporwe na aliyewahi kuwa mwanachama na kiongozi wa juu wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akishirikiana na watu wanaomuunga mkono.  ...

Mbowe ‘Awachana’ Twaweza na Lipumba

Picha
FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amewataka wanachama wa chama hicho na watanzania kwa ujumla kupuuza taarifa za utafiti za wa taasisi ya Twaweza, anaandika Pendo Omary. Tamko la Mbowe limekuja ikiwa ni siku moja tu baada ya Twaweza, kutangaza matokeo ya utafiti wake uliopewa jina la ‘Demokrasia, udikteta na maandamano.’ Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mbowe amesema Twaweza ni wapiga zumari wanaochaguliwa wimbo na watawala wa kiimla ili kujaribu kufunika aibu inayolikabili taifa letu kwa sasa. “Hatua zinazochukuliwa na Rais John Magufuli zimeporomosha uchumi wa nchi yetu kwa kiasi cha kutisha. Mapato ya wananchi yameanguka. Uwekezaji wa ndani na nje ya nchi umepungua. Ajira zimepungua kwa kiasi kikubwa na umasikini umeongezeka,” amesema Mbowe. Ripoti ya utafiti wa Twaweza iliyokusanywa kutokana na wahojiwa 1,602 kati ya tarehe 23 na 29 Agosti, mwaka huu kwa njia ya simu Tanzania Bara, imese...

VIONGOZI WA DUNIA WAHUDHURIA MAZISHI YA WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA ISRAEL, SHIMON PERES

Picha
Askari wakiwa wamelibeba jeneza la mwili wa Shimon Peres  Viongozi mbalimbali duniani wanajiandaa kutoa heshima zao za mwisho wakati wa mazishi ya kiongozi shupavu wa Israeli marehemu, Shimon Peres, aliyefariki Jumatano wiki hii. Rais Barack Obama akizungumza jambo Kuna ulinzi mkali katika eneo ambalo litatumika kwa mazishi yake, katika maeneo ya makaburi ya kitaifa mlimani Herzl mjini Jerusalem. Waombolezaji watajumuisha Rais wa sasa wa Marekani Barack Obama na Rais wa zamani Bill Clinton, aliyefanya kazi na Bw Peres katika mkutano wa mwafaka wa amani wa Oslo mwaka wa 1993. Viongozi kadhaa wa Kipalestina pia watahudhuria mazishi hayo akiwepo Rais Mahmoud Abbas na mpatanishi mkuu wa zamani Saeb Erekat. Itakuwa mara ya kwanza kwa Bw Abbas kuzuru Israel tangu 2010. Rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton alikuwepo kutoa heshima zake kwa Peres Maelfu ya Waisraeli walitoa heshima zao za mwisho kwa hayati Peres, ambaye maiti yake imekuwa nje ya majengo ya Bunge la Israeli, K...

DALILI ZA MVUA NI MAWINGU UWEZEKANO WA HASHEEM THABEET KURUDI NBA WAANZA KUJIONYESHA LIVE SOMA HAPA!!

Picha

Winnie Mandela aibiwa dola 6000 kutoka nyumbani kwake

Picha
Winnie  anasema alipewa pesa hizo wakati wa sherehe ya siku yake ya kuzaliwa alipohitimu miaka 80 Polisi nchini Afrika kusini wanasema wanachunguza kesi ambapo aliyekuwa mke wa rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela, Winnie Madikizela Mandela aliibiwa pesa kutoka nyumbani kwake. Msemaji wa polisi anasema kuwa hawajamkamata mshukiwa yeyote lakini wanaendelea na uchunguzi. Mtandao wa News24 ulisema kuwa Winnie Mandela aligundua kuwa dola 6,000 ambazo alikuwa amepewa kama zawadi wakati ya sherehe ya siku ya kuzaliwa kwake zilikuwa zimetoweka Mtandao huo unasema aligundua kuwa hazikuwepo wakati alienda kutafuta pesa kumtuma mtu anunue mkate. Ripoti zinasema kuwa alikuwa na mipango ya kuzipeleka pesa hizo kwenye benki.

GSM FOUNDATION WAFANIKISHA UPASUAJI WA WATOTO WENYE VICHWA VIKUBWA MKOA WA MARA

Picha
Dkt. Othman Kiloloma akizungumza na waandishi wa habari katika Hospitali ya Rufaa Musoma wakati wa kufunga awamu ya tatu ya kambi tiba ya @GSMFoundationTz

Mahakama yabariki urais wa Nkurunziza

Picha
Uamuzi  huo ulitolewa jana na Mahakama ya Katiba ya Afika Mashariki (EACJ) kutokana na kesi iliyofunguliwa dhidi yake na asasi tatu za kiraia za Burundi, ambazo zilidai amejiongezea muda wa uongozi kinyume cha katiba. Kupingwa kwa Rais Nkurunziza kuendelea kuwa rais kwa awamu tatu, kulisababisha kuibuka jaribio la kumpindua Mei, mwaka jana, chini ya Meja Jenerali Godefroid Niyombane. Kutokana na kuongoza jaribio hilo, Meja Jenerali Niyombane alitimuliwa ukuu wa usalama, ikiwa miezi mitatu baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo. Mapema nchini humo, Mahakama ya Katiba ilimthibitisha Nkurunziza baada ya uteuzi wa chama chake cha CNDD FDD kumpitisha kupeperusha bendera katika uchaguzi mkuu. Hukumuiliyosomwa jana na Jaji Isack Lenaola, ilithibitisha uhalali wa Rais Nkurunziza kuendelea kuongoza nchi hiyo kwa awamu ya tatu kwa mujibu wa Katiba. Jaji Lenaola alisema walalamikaji hao, ambao ni Jukwaa la Asasi za Vyama vya Kiraia katika nchi za Afrika Mashariki (EACSOF), Chama cha Wan...

Chadema Waahirisha Tena Maandamano ya Oparesheni UKUTA

Picha
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Mbowe ametangaza kuwa Operesheni UKUTA iliyokuwa ifanyike Oktoba Mosi haitofanyika tena. Mbowe amesema hayo leo baada ya kimya cha muda mrefu tangu kuahirishwa kwa maandamano Septemba Mosi. Aidha, Mbowe amesema kuwa hawatataja tarehe ya kufanya maandamano ili kutompa adui nafasi ya kujipanga. Amesisitiza kuwa maandamano yapo, ila tarehe hawataweka hadharani. Operesheni hii ilikuwa ifanyike Septemba Mosi mwaka huu lakini iliahirishwa ili kuwapa nafasi viongozi wa dini kuweza kukutana na kujadiliana na Rais Dkt Magufuli juu ya mustakabali wa hali ya kisiasa nchini kufuatia kuzuiwa kwa shughuli mbalimbali za kisiasa. Hadi leo viongozi wa dini bado hawajakutana na Rais Magufuli licha ya wao kueleza kuwa Rais Magufuli hajakataa kukutana nao kama inavyoelezwa na baadhi ya vyombo vya habari

Jicho la 3: Wanachofanya Mbao FC VPL, kinashangaza…

Picha
Na Baraka Mbolembole WAKATI kikosi cha Mbao FC kitakaposhuka uwanjani kupambana na JKT Ruvu katika uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza siku ya Jumapili, mafanikio ya klabu hiyo katika michezo 7 ya mwanzo katika ligi kuu Tanzania Bara msimu huu huenda yakawashtua wengi. Miezi 6 iliyopita, Mbao ilikuwa ikisuasua katika ligi daraja la kwanza huku JKT Ruvu ikiwa katika mashaka ya kubaki VPL. Kwa kipindi hicho mashabiki wengi wa kandanda nchini wangepinga kwamba klabu hizo zinaweza kukutana katika ligi kuu Bara, tena Mbao ikiwa juu ya JKT Ruvu katika msimamo wa ligi. Kitu ambacho kilikuwa kigumu kukifikiria, sasa kimetokea na Mbao inaamini kwamba inaweza kuwachapa mabingwa hao wa FA Cup 2002. Ingawa ilipewa ‘kipigo kikali’ na Mbeya City FC, Septemba 3 kwa kuchapwa 4-1 katika uwanja wao wa nyumbani (Kirumba,) Mbao FC ambayo inashika nafasi ya 7 kwa sasa itakuwa na hamu ya kuonyesha uwezo zaidi kuzingatia kwamba wamefanikiwa kuchukua pointi muhimu kutoka mikononi mwa timu kama...

Uchambuzi na dondoo uelekea Oktoba 1 Yanga vs Simba

Picha
“Si siku ya kukosa kabisa nchi itakuwa kwenye matukio mawili ya kihistoria lile la upandaji miti kisha tunaelekea pale taifa kwenye “Dar Derby” ni mechi ya watani wa jadi Yanga vs Simba, tunaanza kudondoa ndogondogo kuelekea mtanange huo. MSIMAMO:                                             YANGA:   Tayari wamejikusanyia pointi 10, Wakishinda michezo mitatu, kufungwa mchezo mmoja na kutoka sare mchezo mmoja, ikiwa na magoli manane ya kufungwa na moja la kufungwa hivyo GD ni magoli 7, ikiwa nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi.  (Yanga ina mchezo mmoja mkononi) SIMBA:  Hawa ndio vinara wa ligi, Mara baada ya kucheza mechi sita na kujikusanyia pointi 16, ikishinda mechi 5 na kutoka sare mchezo 1. Ikifunga magoli 12 na kufungwa mawili. GD...

Taarifa Ya Kanusho Kuhusu Tangazo La Ajira Serikalini

Picha
Kuna tangazo ambalo linasambazwa kupitia baadhi ya mitandao ya kijamii lenye kichwa cha habari ‘’Sekretarieti ya Ajira yatangaza zaidi ya nafasi za kazi 1,000’’. Likionyesha kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia watanzania wenye sifa na uwezo kujaza jumla ya nafasi wazi za kazi 1,101 kwa niaba ya waajiri mbalimbali Serikalini. Katibu wa Sekretarieti ya Ajira anapenda kuwataafu wadau na wananchi wote kwa ujumla kuwa taarifa hiyo haina ukweli wowote na inalenga kuupotosha Umma, hivyo wananchi wote wanapaswa kuzipuuza.  Matangazo yote ambayo hutolewa na Serikali kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni lazima yaonekane kwenye Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira www.ajira.go.tz  au portal ya Ajira ambayo ni  portal.ajira.go.tz . Kama mnavyofahamu hivi karibuni Serikali ilitoa taarifa ya kusitisha Ajira mpya Serikalini kwa ajili ya zoezi la uhakiki wa Watumishi hewa kama ambavyo t...

Mwimbaji Ray Vanny Adai Ilifika Wakati Akawa Anaichukia Sauti yake...Afunguka Haya Kuhusu Diamond Platnumz

Picha
Mwimbaji Raymond Amefunguka ya moyoni kuhusu boss wake aliyemtoa Kimuziki Diamond Platnumz: Rayvanny Mengi yako Moyoni Mwangu.lakini kiukweli siamini hapa nilipo.nilikata tamaa,sikujiamini tena kama ntaweza kufika.kuna muda nilijiona sina bahati hadi nikaanza kuichukia sauti yangu.lakini wewe ulinishika mkono nakunionyesha njia mengi umenielekeza haukuishia hapo ukaona unipe nafasi tufanye kazi moja mimi na wewe #SALOME . Am so proud of you @diamondplatnumz

Shabiki wa Simba aeleza alivyopelekwa polisi kwa kushangilia kufungwa kwa Yanga

Picha
Bi Halima ambaye ni mwanachama wa klabu ya Simba kwa sasa anamiaka 76 alipiga story na Sports Extra ya Clouds FM na kuelezea baadhi ya mambo ya kishabiki enzi hizo kuelekea game ya Simba na Yanga. “Mimi nilikuwa napata furaha tu na nilikuwa najiamni na timu yangu ya Sunderland, Yanga tulishaifunga mara nyingi mapa ikawa inaitwa ‘four, four’ kwasababu ya vipigo vya magoli manne mfululizo.” Kitu gani kigumu ambacho umewahi kupitia katika mechi za Simba na Yanga? “Nilishapelekwa polisi kwasababu ya kushangilia kufungwa kwa Yanga mwaka 1976 walivyocheza na Inugu Rangers, mimi nikawa nashangilia Inugu Rangers kwa nguvu zangu zote, wakaja kunichukua wakanipeleka polisi wakati huo nilikuwa nakaa mtaa wa Udowe.” “Tulipofika kituoni, yule mzee aliyenikamata kunipeleka polisi kumbe si mwanachama wa Yanga, tulikuwa tumekaa na mkuu wa kituo kwenye baraza la usuluhishi akaniuliza wewe ni mwanachama wa Simba nikasema ndiyo nikaonesha kadi yangu ya Simba,...

Mourinho mpe Pogba watu sahihi wa kucheza nao authibitishie umma thamani yake

Picha
Manchester United jana walikuwa na kibarua kingine Europa League dhidi ya Zorya Luhansk na kushinda bao 1-0, mchezo ambao kocha wa United Jose Mourinho alisema ni lazima ushindi upatikane. Katika mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Old Trafford, United walionekana kukosa ubunifu hasa kwa baadhi ya wachezaji wao akiwemo Marouane Fellaini. Paul Pogba ni mchezaji ghali zaidi duniani kwa sasa ambaye United wamemnunua dirisha la usajili la kiangazi, lakini bado wanashindwa kujua ni wapi hasa mahali sahihi wamchezeshe staa ili aweze kung’aa kama alivyokuwa akifanya Juventus. Kwenye michezo kadhaa aliyocheza pamoja na Fellaini, Pogba alionekana kucheza tofauti na wakati ambapo Fellaini hayupo. Vilevile jana kwenye mchezo dhidi ya Zorya hadhithi ilikuwa ileile. United walikosa kabisa njaa ya kulisakama lango la wapinzani wao. Watu wanajiuliza je, kama angecheza Michael Carrick hali ingekuwa vilevile kama ambavyo alicheza Fellaini? Wakati ambapo ama Carrick au Ander Herrera wameche...

Mke wa Mtu Amponza Mwanamuziki Tunda Man

Picha
Msanii wa Tip Top Connection, Tunda Man ameshindwa kuachia video ya wimbo wake mpya ‘Mwanaume Suruali’ baada ya kumtumia mke wa mtu kama video queen. Muimbaji huyo ambaye bado anafanya vizuri na wimbo ‘Mama Kijacho’, ameiambia Bongo5 kuwa ameshindwa kuachia kazi hiyo kutokana na mume wa mwanamke huyo kuzuia video hiyo sitoke. “Kuna video ya wimbo wangu mpya ‘Mwanaume Suruali’ ambayo ilikuwa itoke hivi karibuni lakini kwa bahati mbaya mume wa video queen ambaye ametumika kwenye video amezuia video isitoke,” alisema Tunda. “Kwa hiyo bado tupo kwenye mazungumzo, kama akiruhusu itoke video itatoka hivi karibuni,” Akifafanua zaidi kilichotokea Tunda alisema “Mimi nilikuwa nipo Dar nilimwachia mtu kazi Zanzibar ya kutafuta location na mambo mengine, kwa hiyo kwa bahati mbaya au nzuri akampata mwanamke ambaye na mimi nilipenda aonekane kwenye video. Kweli tukafanya naye video na pesa yake akalipwa, lakini mwanamke hakusema k...

UTAFITI Twaweza ‘Wambeba’ Tena Magufuli

Picha
RIPOTI ya utafiti mpya wa taasisi ya Twaweza imeeleza kuwa watanzania wengi wanaunga mkono, hatua ya Rais John Magufuli kupiga marufuku mikutano na maandamano ya kisiasa hapa nchini, anaandika Aisha Amran. Matokeo hayo yanatokana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,602 kati ya tarehe 23 na 29 Agosti, mwaka huu kwa njia ya simu. Utafiti huo ulihusisha wananchi wa Tanzania Bara pekee na kwamba watu 6 kati ya 10 wamepinga kuwa nchi inaongozwa kidikteta. Watu hao ni sawa na asilimia 58, walipinga kuwa nchi inaongozwa kidikteta huku asilimia 31 wakieleza kutokuwa na uhakika juu ya suala hilo. Katika utafiti huo unaopewa jina la, “Demokrasia, udikteta na maandamano” unaripoti kwamba  asilimia 80 ya watanzania waliohojiwa, wanasema  baada ya uchaguzi, vyama vya upinzani vikubali kushindwa na visaidiane na serikali kuijenga nchi. Huku asilimia 20 pekee ndiyo wananchi wakisema wapinzani waifuatilie na kuiwajibisha serikali iliyopo madarakani. Katika hatua...

Serikali Yaridhia Utekelezaji Wa Ujenzi Wa Mradi Wa Bomba La Mafuta

Picha
SERIKALI ya Tanzania imeridhia rasmi utekelezaji wa mradi ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Kabaale katika Wilaya ya Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania.    Uamuzi huo umefikiwa katika Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika  tarehe 29 Septemba, 2016  Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.    Taarifa ya kuridhiwa rasmi kwa mradi huo imetolewa naWaziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ambaye amesema ujenzi wa mradi huo utakaoanza wakati wowote kuanzia sasa unatarajiwa kukamilika mwaka 2020.    Amesema ujenzi wa bomba hilo unatarajiwa kugharimu dola za Marekani Bilioni 3.5 ambapo kati yake Dola Bilioni 3 zitatumika kujenga bomba upande wa Tanzania.    Mradi huo mkubwa utatekelezwa kwa ubia wa ujenzi na uendeshaji kwa kushirikishaka mpuni za Total ya Ufaransa, CNOOC ya China, Tullow ya Uingereza na Serikaliza Tanzania na Uganda.  ...

SABABU ZA WEMA SEPETU KUTOFANYA BIRTHDAY PARTY MWAKA HUU

Picha
Jana September 28 ilikuwa ni siku ya kuzaliwa ya Tz Sweetheart Wema Sepetu, kama ilivyozoeleka katika siku ya kuzaliwa ya mwanadada huyo huwa party ya kujipongeza inahusika lakini mwaka huu imekuwa tofauti. Wema Sepetu amefunguka kuwa hawezi kufanya party kwa mwaka huu na mwaka ujao na hivyo anajipanga kufanya bonge la party mwaka 2018 ambapo atakuwa anatimiza umri wa miaka 30. Mwaka jana tulishuhudia mwanadada huyo akijizawadia gari aina ya Range Rover kama kujipongeza katika kusherehekea siku yake hiyo ya kuzaliwa, hatujui mwaka 2018 kipi kitatokea maana amedai kufanya bonge la party.

Ndege BInafsi ya Cristiano Ronaldo Yaanguka, Hakuwemo Ndani

Picha
Ndege binafsi ya mchezaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ilianguka wakati ikitua kwenye uwanja wa ndege wa El Prat jijini Barcelona, Jumatatu. Hakuna majeruhi walioripotiwa. Kwa mujibu wa ESPN, Ronaldo, aliyekuwa Dortmund kipindi hicho wakati Real Madrid ilikuwa ikijiandaa kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa waliotoka sare ya 2-2 katika hatua ya makundi dhidi ya Borussia Dortmund, hakuwa ndani ya ndege hiyo wakati inaanguka. Mshambuliaji huyo huikodisha ndege hiyo, Gulfstream G200, aliyoinunua kwa €19m kufanya kazi zingine wakati asipokuwa akiitumia. Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vya Hispania, matairi ya magari hayo yalivunjika wakati ikitua na hivyo kutoka nje ya njia.

Waziri Mkuu kuhamia Dodoma leo

Picha
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, anatarajia  kuhamia rasmi Dodoma leo. Majaliwa anahamia mjini hapa ikiwa ni sehemu ya kutekeleza ahadi ya Serikali ya awamu ya tano ya kuhamia Dodoma ambako ndiko yaliko makao makuu ya nchi. Julai 25 mwaka huu, katika kilele cha siku ya mashujaa kilichofanyika mkoani hapa, Waziri Mkuu Majaliwa alisema ifikapo Septemba mwaka huu, Serikali itakuwa imehamia mjini hapa. Hatua hiyo ya  waziri mkuu   ilitangazwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alipozungumza  na waandishi wa habari. Alisema   Waziri Mkuu anatarajiwa kuwasili leo mchana akitokea   Dar es Salaam alikokuwa akiishi. “Baada ya kuwasili hapa  atafanya ziara ya siku mbili katika Manispaa ya Dodoma Oktoba mosi na Oktoba 2 mwaka huu   kukagua hatua mbalimbali za maandalizi ya kupokea   Serikali mkoani hapa. “Wakati wa ziara hiyo, atakagua majengo ya Serikali, maeneo ya kutolea huduma za afya, kituo cha...

Tibaijuka Ahofia ESCROW.....Akataa Zawadi ya Milioni 200

Picha
MBUNGE wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka (CCM), amepata tuzo ya Umoja wa Mataifa (UN) ikiwa ni mchango wa kuthamini kazi aliyoifanya, huku akikataa kupokea zawadi ya Dola 100, 000 za Marekani, ambazo ni zaidi ya Sh milioni 200. Profesa Tibaijuka alitoa taarifa hiyo jana jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo alisema tuzo hiyo ya Maendeleo Endelevu ilidhaminiwa na mwana Mfalme wa Bahrain, Khalifa bin Salman Al Khalifa. Alisema, hatua ya kuzikataa fedha hizo, ni njia ya kukwepa mtego kama uliomkuta mwaka juzi baada ya kupokea fedha za Escrow Sh bilioni 1.6 kutoka kwa mfanyabiashara,  James Rugemalira. Tuzo hiyo ambayo ni heshima kwa Tanzania, alikabidhiwa Septemba 24, mwaka huu na inajulikana kama ‘His Royal Highness Prince Khalifa bin Salman Al Khalifa Award  for Sustainable Development’. Profesa Tibaijuka alisema, alikabidhiwa tuzo hiyo kwa kutambua mchango wake katika kuhamasisha maendeleo duniani. Alisema tuzo  h...

Mkwasa ametoa mtazamo wake  kuelekea Yanga vs Simba

Picha
Siku moja kuelekea pambano la Simba na Yanga, Charles Boniface Mkwasa mchezaji wa zamani wa Yanga ambaye kwa sasa ni kocha Mkuu wa timu ya taifa ametoa mtazamo wake kuelekea mchezo huo wa Jumamosi. “Timu hizi mbili zinapokutana inakuwa ni mechi ambayo inagusa watanzania wengi sana, lakini ukitazama sana hii mechi inakuwa na maneno mengi, presha kubwa, tension kubwa si tu kwa mashabiki lakini tension inaingia hadi kwenye timu na wachezaji wakashindwa ku-perform au timu ikashindwa kucheza kiufundi kwasababu wanataka kucheza kwa haraka kutafuta ushindi au kukamiana.” “Ladha ya mpira ikakosekana lakini kwasababu ni mechi ya wakubwa basi kunakuwa na mpambano lakini ukiangalia standard ya namna gani mipango inatoka upande mmoja kweda mwingine, huwezi kuiona kwasababu wachezaji hawachezi kwa lengo la kuonesha standard ya mpira ila lengo ni ushindi kama unavyojua timu moja inapofungwa kizaa-zaa huwa kinaanzia hapo na migogoro inaanzia kwenye mechi kama hizi.” “...

Waziri Mkuu apokea misaada zaidi ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko Kagera

Picha
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea zaidi ya sh. milioni 760 zikiwa ni misaada kwa wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Septemba 10, mwaka huu.   Amepokea misaada hiyo kutoka kwa taasisi na wadau mbalimbali likiwemo kundi la wanawake New Millennium linaloundwa na wake wa viongozi wa Serikali walio madarakani na waliostaafu.   Makabidhiano ya michango hiyo, yamefanyika jana jioni (Alhamis, Septemba 29, 2016) kwa nyakati tofauti kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam pamoja na makazi ya Waziri.   Miongoni mwa waliokabidhi misaada hiyo ni pamoja Meya wa jiji la Dar es Salaam Mhe. Isaya Mwita sh. milioni 10, Kampuni ya mabati ya ALFA imekabidhi mabati yenye thamani ya sh. milioni 50 na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) sh.milioni 100.    Wengine ni Ofisa Mtendaji Mkuu kampuni ya vinywani baridi ya Pepsi Cola, Bw. Avinash Jha amekabidhi sh.milioni 50, kampuni ya Round Table pamoja na wadau wao sh. m...

Taarifa kuhusu kesi ya viongozi waliofungua akaunti bandia ya maafa Kagera

Picha
Watumishi  watatu wa Serikali akiwamo Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Bukoba, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba wakituhumiwa kutaka kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu. Watumishi hao wanadaiwa kutaka kujipatia fedha hizo baada ya kufungua akaunti feki iitwayo kamati ya maafa Kagera kwa ajili ya kukusanya fedha za kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Septemba 10 mwaka huu. Watumishi waliofikishwa mahakamani hapo jana ni aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Amantus Msole, Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba, Kelvin Makonda, Mhasibu wa Mkoa wa Kagera, Simbaufoo Swai na Meneja wa CRDB tawi la Bukoba, Carlo Sendwa. Akisoma mashtaka hayo, Wakili wa Serikali, Hashimu Ngole, alidai watuhumiwa hao wanashtakiwa kwa makosa mawili. Alilitaja shtaka la kwanza kuwa ni kula njama za kutenda kosa la kufungua akaunti feki yenye jina linalofanana na jina la akaunti iliyofunguliwa na Serikali kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la...

Chadema kutoa msimamo wa Oparesheni UKUTA Leo

Picha
Mwezi mmoja baada ya Chadema kusitisha Operesheni Ukuta kupinga inachokiita ukiukwaji wa haki za binadamu na ukandamizaji wa demokrasia, leo inatarajia kutoa mwelekeo wa mkakati huo. Operesheni hiyo ilipangwa kuzinduliwa Septemba mosi nchini kwa maandamano na mikutano ya hadhara kama maazimio ya Kamati Kuu ya Chadema, baada ya chama hicho kukumbwa na vikwazo kadhaa kuendesha shughuli zake, ikiwa ni pamoja na kuzuiwa kufanya mikutano ya hadhara. Siku moja kabla ya kufanyika kwa operesheni hiyo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alitangaza kuisitisha kwa mwezi hadi kesho, ili kutoa fursa kwa viongozi wa dini kusemezana na Rais John Magufuli na Serikali yake. Jana, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alisema:  “Kuhusu Ukuta, kesho (leo) tutatoa msimamo wetu juu ya kitu tutakachofanya.” Alisema operesheni hiyo ilisitishwa kutokana na sababu za msingi zilizoelezwa, hivyo kauli ya chama hicho leo itafafanua kwa kina kuhusu mambo yote yaliyojitokeza katika kipindi...