SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 28 Septemba 2016

T media news

Wafuasi wataka Maalim aitishe mkutano kumtambua Lipumba

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad 

Baadhi ya wafuasi wa aliyekuwa mwenyekiti wa CUF wamesema ili Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad aweze kuingia katika ofisi za makao ya CUF Buguruni ni lazima aitishe mkutano na wanahabari kumtambua Profesa Lipumba.

Baadhi ya wafuasi hapo wamekusanyika eneo la ofisi hiyo wakiwa na nia ya kumpokea Profesa Lipumba na kumzuia Maalim Seif endapo atafika.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake Juma Yassin amesema Maalim Seif ataendelea kubaki Zanzibar iwapo  hatataka kumtambua Profesa Lipumba ambaye ni mwenyekiti halali Kikatiba.
"Tumesikia leo huenda akaja lakini ofisi  na asijisumbue tupo tayari kwa lolote hadi amtambue Profesa Lipumba," amesema Yassin ambaye ni mwenyekiti wa Tawi la Kosovo Manzese.