SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 28 Septemba 2016

T media news

AUNTEZEKEL AFUNGUKA KUHUSU : WEMA SEPETU ATAJIJUA KISA KUWA KARIBU NA ZARI

KAMA ni noma na iwe noma! Mwigizaji Aunt Ezekiel amesema kama kitendo cha yeye kuwa karibu na mpenzi wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kama kitapokelewa vibaya na shosti wake muigizaji Wema Sepetu ‘Madam’, hatajali, atajijua mwenyewe maana hana jinsi. Kauli hiyo imekuja ikiwa ni baada ya Aunt kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa ya mpenzi huyo wa Diamond, iliyofanyika visiwani Zanzibar na picha za Aunt akiwa ameshikilia tumbo la Zari kuvuja mitandaoni.

Baada ya picha hizo kuvuja, watu mbalimbali walianza kuchangia kwenye mitandao ya kijamii kwa kusema kitendo hicho hakitamfurahisha Madam huku wengine wakimpongeza Aunt kwa kuonesha anamsapoti kwanza ‘ubavu’ wake halafu marafiki baadaye.

Mara baada ya kuona maoni hayo mitandaoni, R i s a s i Mchanganyiko, lilimvutia waya Aunt na kutaka k u m u u l i z a k w a m b a haoni kitendo hicho kinaweza k u p o k e l e w a tofauti na

Madam ndipo mrembo huyo alipofunguka: “Mimi sioni kama ni tatizo, kupiga picha na Zari na kuwa naye karibu maana anapaswa pia atambue mimi kuwa karibu na yule au Diamond kuna sababu. Mtu wangu mimi (Moses Iyobo) anafanya kazi chini ya Diamond, Zari ni mtu wa karibu wa Diamond sasa wakinialika shughuli yao lazima niende. “Kwanza namuunga mkono mume wangu mtarajiwa Iyobo, lakini pia si vibaya mimi nikiwa karibu na Zari maana namuunga mkono Diamond ambaye ni bosi wa Iyobo.

Naanzaje kumchukia mtu anayesababisha sisi tupate mkate wa kila siku? Kama yeye (Wema) atanichukia kwa hili kwa kweli atajiju maana sina jinsi lakini naamini hawezi kufanya hivyo maana hata yeye ni muelewa,” alisema Aunt. Urafiki wa Wema na Aunt ulikuwa mkubwa sana kipindi cha nyuma lakini katika kipindi cha hivi karibuni, u n a o n e k a n a k u l e g a l e g a hivyo kitendo cha Aunt kuonekana yupo karibu na Zari, k i m e z u a gumzo na kuongeza hisia za watu kuamini kwamba ushosti wao umekufa kabisa!