SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 28 Septemba 2016

T media news

Ndalichako apingwa na walimu

Maswa. Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wilayani hapa, Mkoa wa Simiyu, kimemjia juu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako kuwa anaupotosha umma juu ya madai yao.

Kimesema walimu wanadai madeni mengi, hivyo kauli ya Ndalichako kwamba hawana wanachodai inalenga kuleta uchonganishi kati yao na Serikali.

Mwenyekiti wa CWT wilayani hapa, Onesmo Makota amesema wao wanaidai Serikali zaidi ya Sh500 milioni kutokana na malimbikizo na mapunjo ya mishahara.