SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 27 Septemba 2016

T media news

BREAKIN NEWZZ!!:- PROFESSOR LIPUMBA AZIDI KUIPASUA CUF VIPANDE VIPANDE ONA MKUTANO WAKE WA LEO LIVE!!


Vikundi vya wafuasi wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Profesa Ibrahim Haruna Lipumba wamekusanyika katika Ofisi za CUF Makao Makuu, Buguruni, Jijini Dar es Salaam wakisubiri kumpokea na kumuingiza ofisini.

Wanachama hao wanadai ya kuwa wana barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa inayomtambua Lipumba aliyetangaza kujiuzulu nafasi hiyo mwaka jana kama Mwenyekiti halali wa CUF.

Kwa mujibu wa shuhuda eneo la tukio, inadaiwa kuwa geti la ofisi za chama hicho limefungwa kwa ndani ambapo hakuna kiongozi yeyote aliyepo ndani.

Wafuasi hao wa Lipumba wamesikika wakiimba na kucheza huku wakidai kuwa wanasubiri msafara wa Lipumba ambao upo njiani kuelekea Makao Makuu ya CUF hapo Buguruni.

Awali hapo jana Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF, Julius Mtatiro alikanusha taarifa zilizokuwa zinaenea katika mitandao ya jamii kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa ametoa barua inayoagiza Profesa Lipumba arudi katika nyadhifa yake ya Uenyekiti na kuwataka wanachama wa CUF wasubiri taarifa rasmi kutoka kwa viongozi wao.

Hatahivyo, leo alipoulizwa kuhusiana na sakata hilo alikiri CUF kupokea barua kutoka kwa Msajili na kudai bado hawajaisoma ili kujua maudhui yaliyomo ndani.

Ameongeza kuwa pamoja na hayo Msajili wa Vyama vya Siasa hana mamlaka ya kuingilia maamuzi ya vikao vya chama chochote cha siasa.

Chanzo:Jamiiforums