Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif
Wakati Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akijiandaa kuzungumza na wafuasi wake leo jijini hapa, Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif naye yupo kwenye kikao maalum kinachoendelea hivi sasa Vuga, Unguja.
Juzi, Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi juzi aliandika barua inayomtambua Profesa Lipumba kuwa Mwenyekiti wa chama hicho hali iliyowakusanya wafuasi wake katika ofisi za chama hicho Buguruni na baadaye mwanasiasa huyo kuingia katika ofisi yake.
Mwandishi wetu aliyeko eneo la tukio sasa hivi anaendelea kutujuza yanayojiri.