Jinsi ya kuhifadhi mboga za majani kama mchicha, maboga, matembele n.k.



Hatua 👇👇👇.
1. Chuma mboga zako zilizo tayari.

2. Zichambue kuondoa yasiyohitajika.

3. Safisha kwa maji.

4. Kisha tafuta mfuko mzuri wa kitambaa kisha funga mboga zako humo.

5. Chemsha maji hadi yachemke.

6. Weka mboga zako kwenye kitambaa kwenye hayo maji yaliyo jikoni yamechemka kwa dakika 5.

7. Zitoe kisha ziache zichuruzike maji.

8. Kaanike juani kwenye kichanja ila juu funika kwa kitambaa cheusi.

9. Ikikauka tafuta chombo kisichoingiza hewa ihifadhi vizuri, hakikisha haipati unyevu wa maji.

10. Mboga hiyo inaweza kudumu kwa miezi 6.

Nawasilisha.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: UTAMU WA MADAM JESCA

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU

SIMULIZI FUPI: UCHI WANGU UMENIPONZA