SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 27 Septemba 2016

T media news

Wafuasi 22 wa CUF kutoka Zanzibar wametiwa mbaroni na Jeshi la polisi kanda Maalum Dsm

Wafuasi 22 wa chama cha wananchi Cuf kutoka zanzibar wametiwa mbaroni na Jeshi la polisi kanda Maalum dsm baada ya kudaiwa kupanga njama za kuhujumu makao makuu ya Cuf Buguruni ambapo jeshi hilo wamesema wakamata na vifaa vya milipuko,Visu,majambia pamoja na spray ambazo zinadhaniwa kuwa tindikali.

Kamishna wa Polisi kanda maalum dsm Simon siro amesema vijana hao ambao wanashikiliwa na kuhojiwa wamekamatwa eneo la mwananyamala wakati wakiwa katika gari namba T.857 CHE ambapo wengine wanane walifanikiwa kutoroka.

Katika matukio mengine ya uhalifu jeshi hilo limemtia mbaron Bakari Abdallah na a mkewe kwa tuhuma za ujambazi wa kutumia silaha ambapo katika upekuzi walifanikiwa kukamata bastora pamoja na risasi tano ambapo pia wanawashikilia watuhumiwa wengine 12 na bunduki 2 kwa tuhuma za ujambazi.

Aidha jeshi hilo limefanikiwa kuyanasa magari mawili yalisheni magunia ya bangi yaliyokuwa yakiingizwa  dsm kutoka mkoani Iringa .