Baraza Kuu la Uongozi CUF lamfuta uanachama Profesa Lipumba

Baraza Kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF) Taifa lililokutana Zanzibar leo limemfukuza uanachama Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Prof. Ibrahim Lipumba.

Taarifa kutoka katika mkutano chama hicho unaeleza kuwa, wajumbe wote waliohudhuria wamepiga kura ya kuridhia kufukuzwa uanachama kwa Prof. Lipumba.

Hatua hii imekuja ikiwa ni siku chache tangu Prof. Lipumba kurejea na kusema kuwa yeye ni mwenyekiti halali wa chama hicho kufuatia maamuzi yaliyotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Mutungi.

Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF limefikia uamuzi huo kwa mujibu wa Katiba ya Chama, Ibara ya 10 (1)(c).

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: UTAMU WA MADAM JESCA

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU

SIMULIZI FUPI: UCHI WANGU UMENIPONZA