Real Madrid leo wana kibarua kigumu ugenini nchini Ujerumani kucheza na Borussia Dortmund kwenye mchezo wa raundi ya pili ya Kundi F wa UEFA Champions League utakaochezwa kwenye Uwanja wa Signal Iduna Park.
Wakati Real Madrid wametoka kuvutwa na shati kwenye La Liga kwa kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na Las Palmas wikiendi iliyopita, Borussia Dortmund kwa upande wao walikuwa na furaha baada ya kuwafunga Freiburg 3-1.
*Borussia wakiwa katika kiwango bora mpaka sasa wameshinda michezo yao yote minne iliyopita katika michuano yote, wakiwa wamefunga magoli 20. Madrid, kwa upande wa wamekosa njaa ya magoli katika safu yao ya ushambuliaji na kushuhudia wakipoteza pointi katika michezo kadhaa iliyopita.
Lakini kocha wa Madrid Zinedine Zidane, ambaye alishinda kila kitu akiwa mchezaji, anaweza kufanya mabadiliko machache kuelekea mchezo huu katika dimba la Sigbal Iduna Park, sehemu ambayo timu imekuwa na historia mbovu kabisa
Kimsingi kwenye mechi zao za mwisho katika uwanja huo kwenye misimu ya 2012, 2013 na 2014, Real hawajashinda mchezo wowote zaidi ya kuambulia vipigo vitatu na sare moja.
Michezo ya hivi karibuni imewapa Madrid matokea ambayo hawakuwa wametarajia. Kiungo mkabaji Casemiro amethibitisha umuhimu wake kwenye timu hiyo na kukosekana kwake katika michezo kadhaa ukiwepo hu wa leo ni pigo kubwa kwa Real kutokana na kukosa muhimili muhimu katika eneo la kiungo mkabaji.
Kutokuwa katika kiwango bora mchezaji Cristiano Ronaldo ni changamoto kubwa kwa ‘BBC’, na hata katika mchezo dhidi ya Las Palmas alitolewa nje kutokana na kushindwa kucheza vyema.
Luka Modric na Toni Kroos watakuwa na kibarua kizito kuhakikisha wanacheza vyema eneo la kiungo, na kuondoa mapungufu yaliyoonekana kwenye baadhi ya michezo iliyopita hasa eneo la kiungo mkabaji ambalo linamkosa Casemiro.
Vilevile, ni vigumu sana kwa James Rodriguez au Isco kupata nafasi ya kuanza kwenye mchezo wa leo kutokana aina ya mchezo wa Dortmund. Dortmund chini ya kocha wao Thomas Tuchel wanacheza soka la kasi ambalo litahitaji umakini mkubwa kwa Madrid katika kuzuia mashambulizi.
Dortmund wanajivunia uwepo wan straika wao aliye kwenye kiwango bora Pierre-Emerick Aubameyang bila kusahau Shinji Kagawa na Mario Gotze ambao lwa pamoja wote watauwasha moto kuhakikisha Dortmund wanapata matokeo.
Wengine ni Ousmane Dembele na Emre Mor ambao pia ni msaada mkubwa kwa wakali hao wa Signal Iduna Park.
Madri wanapaswa kuwa makini zaidi ukizingatia kwamba mpaka sasa Dortmund ndio timu yenye magoli mengi zaidi kwenye Bundesliga, wakiwazidi hata Bayern. Hii inaonesha namna gani walivyokuwa na safu hatari ya ushambuliaji.
Head-to-head statistics
Katika jumla ya michezo yote 10 waliyokutana na Dortmund, Real Madrid wameshinda mara 4, sare mara 3 na wamefungwa mara 3.Katika michezo mitano waliyokutana na Real Madrid Signal Iduna Park, Dortmund hawajafungwa hata mchezo mmoja kati ya mitano, wameshinda mara 3 na kutoka sare mara 2.Mara ya mwisho kukutana ilikuwa ni kwenye robo fainali ya Champions League msimu wa 2013/14. Real walishinda kwa wastani wa mabao 3-2 margin. Mchezo wa kwanza Dortmund walifungwa mabao 3-0 na wao kulipiza nyumbani kwa kushinda mabao 2-0.Real Madrid hawana rekodi nzuri kwa timu za Ujermani wakiwa ugenini kufuatia kufungwa magoli 2-0 na Wolfsburg kwenye robo fainali ya Champions League msimu uliopita. Hata hivyo Real walifuzu baada ya kushinda mabao 3-0 katika mchezo wa marudiano.