SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 29 Septemba 2016

T media news

MFAHAMU RUBANI WA KIKE MDOGO KULIKO WOTE DUNIANI

Kate McWilliams ndiye mwanadada kutoka Uingereza anaetajwa kuwa binti mdogo zaidi kuweza kuwa rubani wa ndege za kibiashara.
Taarifa kutoka mjini Carlisle zimesema kuwa binti huyo alianza kupanda ndege na kuongozana na marubani wengine akiwa na umri wa miaka 13 kabla ya kwenda kwenye mafunzo akiwa na umri wa miaka 19 katika kituo cha mafunzo cha ‘CTC Aviation’huko mjini Southampton na baada ya hapo amejiunga na kampuni ya ‘EASYJET’ kama Afisa tangu mwezi Mei 2011.


Kate McWilliams anaiongoza ‘Airbus A319’ pamoja na ‘A320’ zinazokwenda kwenye vituo takribani 100 ikiwemo miji maarufu duniani kama Reykjavik, Tel Aviv na Marrakech.