Arsenal wameshinda mchezo wao Kundi A wa Champions League katika Uwanja wa Emirates usiku wa kuamkia leo.
Theo Walcott ndiyo alikuwa shujaa wa mchezo, akifunga mabao mawili kwenye kipindi cha kwanza yalidumu muda wote wa mchezo. Mpaka sasa Walcott amefunga mabao 4 katika michezo 3 iliyopita.
Ndugu wawili Granit na Taulant wadhihirisha mapenzi ya dhati kati yao kwa kubadilishana jezi
Ikumbukwe wawili hawa walishawahi pia kukutana kwenye Michuano ya Euro mwaka 2016 akati Granit akiichezea Switzerland huku Taulant akichezea Albania.
Jana walikutana tena Granit akiwa upande wa Arsenal na Taulant akiwa upande wa Basel na baada ya mchezo walikutana na kubadilishana jezi ikiwa ni ishara ya upendo mkubwa uliopo kati yao.
Video