Balozi wa Malawi afurahishwa na jitihada za Mkuu wa mkoa kuimarisha uhusiano wa nchi mbili Malawi yaomba ushirikiano katika biashara, kilimo, utalii na Elimu Mkuu mkoa asema kupitia Mkoa wa Mbeya serikali inajenga meli Tatu aomba meli hizo zifike mpaka malawi kukamilika kwa meli , uwanja wa ndege kutarahisisha biashara, utalii na usafiri
MKUU WA MKOA WA MBEYA Amos Makalla leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Malawi nchini Tanzania Hon Hawa Ndilowe mkoani Mbeya kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kukuza uhusiano wa nchi mbili
Kwa upande wa Balozi wa malawi amesifu jitihada za Mkuu wa mkoa wa Mbeya kwa kufanya mikutano YA hadhara mpaka wa kasumulu unaotenganisha Malawi na Tanzania na kupitia kauli zake za kuhubiri amani na ushirikiano zimemfanya balozi kuja Mbeya
Ameomba ushirikiano zaidi na amehaidi kushirikiana na Tanzania ktk sekta YA kilimo, biashara , utalii na Elimu
Kwa upande wa Mkuu wa mkoa wa Mbeya amemwakikishia Balozi wa Malawi ushirikiano na anaomba kuwepo kwa ziara na vikao vya kubadilishana uzoefu na fursa mbalimbali zilizopo ktk nchi mbili
Amesema Tanzania kupitia Bandari YA Itungi inajenga Meli mbili za mizigo na meli moja YA abiria zitakazokamilka mwaka huu na hivyo kurahisisha usafirishaji wa mizigo na abiria na kumuomba Balozi awajulishe watu wa malawi juu YA fursa hiyo na kuitumia
Aidha kukamilika kwa uwanja wa ndege wa songwe pia ni fursa YA kukuza utalii katika mhifadhi za Kitulo na Ruaha