Wajua kuwa Salama wa Eatv ana mkopy swaga mtangazaji huyu?
Anaitwa Ellen Lee DeGeneres amezaliwa tar. 26 Januari 1958 ni mwigizaji wa filamu na mchekeshaji kutoka nchini Marekani, amezaliwa na kukulia Metairie, Louisiana .
Ni mtangazaji wa kipindi maarufu sana duniani ChaThe Ellen Show kikitazamwa na watu wengu zaidi pia kupitia mtandao wa Youtube.
Ellen alionekana kwenye Tv kwa mara ya kwanza kupitia show iliyo fahamika kama Open House ambamo alicheza kama Margo Van Meter.
Mwaka 1992 muandaaji wa vipindi anae fahamika kama Neal Marlens akiwa na mwenzie Carol walimpa tena nafasi Ellen katika show nyingine ya Laurie Hill.
Kabla ya hapo Ellen alianzia katika uchekeshaji jukwaani katika sehemu tu wanazo uza kahawa hii ilikuwa mwanzoni mwa miaka ya 1980, alibahatika kuwa msema chochote (MC) mwanzoni mwa 1981 katika moja ya majumba ya maonesho lijulikanalo kama Clyde's ComedyClub huko New Orleans marekani.
Kwanini anafananishwa na Salama?
Achilia mbari kufanana sura kwa mbalii lakini pia wawili hawa wote wana mienendo inayo fanana ikiwemo kupendelea kuvaa mavazi ya kiume
Pia wawili hawa wote ni watangazaji wa Tv achilia mbari kufanana kwao pia kwa namna wanavoongea hata viyuko vyao wanapo ongoza vipindi vyao.







Maoni
Chapisha Maoni