Rais Magufuli Amteua Thobias Andengenye Kuwa Kamishna Mkuu Wa Jeshi La Zimamoto Nchini


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye kuwa Kamishna Mkuu wa Jeshi la Zimamoto nchini.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 25 Aprili, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Kamishna Andengenye umeanzia leo tarehe 25 Aprili, 2016.

Kamishna wa Polisi Andengenye anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Pius Makuru Nyambacha ambaye amestaafu.

Kabla ya uteuzi huo Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye alikuwa Kamishna wa Utawala na Utumishi, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.

Wakati huo huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Donan Mmbando kuwa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Benjamin Mkapa ya Dodoma.

Uteuzi wa Dkt. Donan Mmbando umeanza tarehe 24 Aprili, 2016.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam-25 Aprili, 2016

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: UTAMU WA MADAM JESCA

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU

SIMULIZI FUPI: UCHI WANGU UMENIPONZA