NDOTO ZA AZAM FC ZAYEYUSHWA NA ESPERANCE

TUNIS

KLABU ya Esperance ya Tunisia usiku wa jana imeweza kudhihirisha kuwa wawao ni bora zaidi ya Azam na inastahili kuwa katika nafasi ya 342 kwa ubora duniani mara baada kuirarua Azam Fc kwa jumla ya magoli 3-0.

Katika Mchezo huo uliokuwa mkali na wa aina yake uliochezwa mjini Tunis wenyeji walianza kulisakama lako la Azam mapema tu mara baada ya kipyenga kupulizwa,hali iliyowasaidia kupata goli katika dakika ya 16 ambalo hata hivyo lilikataliwa.

Magoli ya wenyeji jana yalifungwa na Saad Bguir,Haythem Jouini na Fakhreddine Ben Youssef, Aidha katika mchezo huo Azam walikosa huduma za mshambualiji wake hatari Kipre Tchetche,Pascal Wawa na Shimari Kapombe ambao ni majeruhi.

Katika mchezo wa Kwanza Azam waliibuka na ushindi wa 2-1,hivyo kuwafanya watolewe kwa jumal ya magoli 4-2

Kwa matokeo hayo ndoto za Azam za kufika katika hatua ya makundi ya michuano ya kombe la shirikisho Afrika zimeota mbawa huku wakiiacha Yanga kuwa mwakilishi pekee kutoka ukanda huu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika michuano ya kimataifa.

Yanga itashuka dimbani leo hii kuumana na National Al Ahly ya Misri katika mchezo wa pili wa hatua ya 16 bora ya michuano ya ligi ya mabingwa Afrika huko Misri.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: UTAMU WA MADAM JESCA

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU

SIMULIZI FUPI: UCHI WANGU UMENIPONZA