Mwanzo wa kutengeneza gari

Motokaa

Ford Mondeo ni motokaa ndogo ya kubeba abiria wachache, kwa mfanofamilia ndogo.

Magari kama Toyota Landcruiser hujengwa juu ya fremu ya lori dogo kwa kusudi la kubeba watu kwenye njia mbaya.

Motokaa (kutoka Kiingereza "motor car"[1], mara nyingi huitwa tu gari) ni chombo chausafiri kinachotembea kwenye nchi kavu kikitumia nguvu ya injini au mota yake.

Kuna aina nyingi za motokaa; magari madogo hubeba abiria tu na gari dogo la kawaida hubeba dereva pamoja na abiria hadi wanne. Magari makubwa kidogo hubeba hadi watu 8.

Mengine ya kubeba abiria ni mabasi ambayo ni pia aina ya motokaa lakini mara nyingi hutajwa kama kundi la pekee, sawa na malori ambayo ni motokaa kubwa za kubeba mizigo. Kuna kila aina ya mchanganyiko kati ya aina hizi.

Fremu ya motokaa pamoja na magurudumu, bila injini wala bodi

.

Muundo

Historia ya motokaaEdit

Kwa karne nyingi watu walitumia magari yaliyovutwa na wanyama kwa mfano farasi,punda au maksai. Waroma wa kale walifanya majaribio na magari yaliyosukumwa na watumwa. Maendeleo ya uhandisi yalisababisha majaribio ya kutengeneza magari yaliyosogezwa kwa nguvu ya upepo yakitumia tanga kuanzia mwaka 1600 hukoUholanzi.

Injini za mvukeEdit

Baada ya kugunduliwa kwa injini ya mvukenguvu yake ilitumiwa pia kwa vyombo vya usafiri. Kutokana na uzito wa injini pamoja na magari yaliyoweza kuvumilia uzito mkubwa wa injini pamoja na maji na kuni iliyohitajika kuchemsha maji vyombo hivi havikufaa barabara za kawaida vikatumia njia ya reli za chuma. Nusu ya pili ya karne ya 19 iliona maendeleao ya kutengenezwa kwa motokaa za mvuke madogo yaliyotembea barabara za kawaida katika nchi za Ulaya na Marekani.

Injini za umemeEdit

Sehemu ya pili ya karne ya 19 iliona pia magari yaliyoendeshwa kwa nguvu ya umeme. Magari haya yana faida nyingi; muundo wa gari ni rahisi zaidi kwa sababu haihitaji giaboksi wala gia na gari halina makelele pia hautoi harufu baya ya eksozi. Lakini magari haya yalikuwa na tatizo ya kwamba yalitegemea kupata nishati kwa njia ya beteri nzito zilizochukua muda mrefu kuchajiwa. Hata hivyo hadi mwanzo wa karne ya 20 magari ya umeme yalikuwa mengi katika miji mikubwa.

Basi ya umeme mjini San Franciscoinapokea nishati kupitia waya juu ya barabara inapopita

Mwaka 1900 asilimia 40 za motokaa zote nchini Marekani zilikuwa na injini za mvuke, 38 % za umeme na 22% za petroli. Mjini New York nusu ya motokaa zote zilikuwa na injini ya umeme.

Baadaye magari ya petroli yalisogea mbele kwa sababu yaliweza kutembea mbali kwa kujaza mafuta kuliko magari ya umeme kwa beteri zao. Pia beteri zilichukua masaa mengi hadi kujazwa upya wakati mafuta hujazwa mara moja.

Katika nchi kadhaa mabasi ya umeme yameendelea kutumiwa katika miji mikubwa yakipokea nishati si kwa beteri bali kwa nyaya za umeme zinazopangwa juu ya barabara ambako basi inapita.

Katika karne ya 21 teknolojia ya beteri ilisogea mbele kutokana na upanuzi wa matumzi ya simu za mkononi. Beteri ziliendelea kuwa ndogo zaidi na pia kushika umeme kwa muda mrefu zaidi. Maendeleo haya yametumiwa kwa kubuni motokaa mpya za umeme. (tazama chini)

Injini za mwako ndani (petroli na diseli)Edit

Injini mwako ndani imekuwa hadi leo njia kuu ya kusogeza magari na kwa kawaida tukiongelea motokaa tunamaanisha gari lenye injini mwako ndani inayochoma petroli au diseli.

Motokaa ya kwanza ya Benz ya 1885

Katika karne ya 19 wahandisi mbalimbali walianza kutengeneza injini za mwako wa ndani zilizochoma gesi au petroli ndani yake. Injini ya kwanza iliyofaulu kuanzia 1876 na kutengenezwa kwa wingi ilikuwa ni ile ya Mjerumani Nikolaus Otto aliyeshirikiana naGottlieb Daimler na Wilhelm Maybach. Ilikuwa na mapigo manne petroli ikichomwa kwa msaada wa mwasho wa umeme na hadi leo sehemu kubwa ya injini zote inafuata kielelezo wa Otto. 1879 Karl Benz alitengeneza injini ya mapigo mawili kwa mfano wa Otto akaitumia kwa gari lake na tangu 1885 akatoa aina ya kwanza ya motokaa yenye magurudumu matatu iliyoendelea kujengwa mfululizo yaani kibiashara.

Maendeleo ya motokaa zilizotumia injini mwako ndani yalikuwa haraka. Mwanzoni yalikuwa na matatizo mengi hasa uhaba wa petroli. Benz alinunua mafuta kwa gari lake kwenye duka la dawa.

1892 mhandisi Mjerumani Rudolf Diesel alitunga injini inayochoma mafuta kwa kuikandamiza vikali na kutumia joto la hewa ndani ya injini kutokana na mshtuko wa kukandamizwa. Mashine hizi zina uwezo kutumia aina mbalimbali za mafuta na ile ya kawaida ilikuwa nzito kuliko petroli ikaitwa "diseli". Injini za diseli zamani hazikupendwa kwa magari madogo kutokana na sauti kubwa zaidi ya injini lakini zikawa kawaida kwa malori, mabasi na injini za meli kwa sababu zinatumia mafuta kidogo kuliko injini za petroli.

Gari la Ford T ya 1926

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: UTAMU WA MADAM JESCA

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU

SIMULIZI FUPI: UCHI WANGU UMENIPONZA