MUSSA SWEDI ASHINDA UNAIBU MEYA JIJI LA DAR ES SALAAM


Na Moshi Shaban

Machi 22, Mwaka huu alipatikana Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita (CHADEMA) kupitia Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) , baada ya  kuishinda CCM iliyopata kura 67, huku UKAWA wakipata kura 84, ambapo kura 7 ziliharibika, ambapo nafasi ya Naibu Meya wa Jiji hilo ilibaki wazi.

Mapema leo zoezi la Uchaguzi wa kumpata Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, ambapo katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee Mussa Swedi Kaffana (Diwani wa CUF Kata ya Kiwalani) ametangazwa mshindi wa nafasi ya Unaibu Meya wa Jiji hilo baada ya kuchaguliwa kwa kura 10, dhidi ya Mpinzani wake Mariam Luginda (CCM) kuambulia kura 6, na wala hakuna iliyoharibika.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: UTAMU WA MADAM JESCA

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU

SIMULIZI FUPI: UCHI WANGU UMENIPONZA