Mpenzi wa Kala Jeremiah ajifungua mtoto wa kiume, anaitwa ‘Alama’

Mpenzi wa msanii wa muziki wa Hip Hop, Kala Jeremiah amejifungua mtoto wa kiume Jumamosi hii, nakupewa jina, ‘Alama’.

Akizungumza na Bongo5 Jumatatu hii, Kala amesema jina Alama limetokana na jina lake la zamadi, ‘Mark’.

“Kusema kweli nafuraha sana kupata mtoto wa kwanza wakiume,” alisema Kala. “Mama yake nipo naye sema sikainaye ila ni mtu wangu wa muhimu sana kwa sababu ameniletea kiumbe,”

Aliongeza, “Mwanangu anaitwa Alama, vyovyote unavyotaka kumuita, ukitaka umwite alama ya kuuliza, sijui nini wewe tu. Nimempa jina hilo kwa sababu ni jana langu ambao nilikuwa natumia wakati nauza mtumba, hata marafiki zangu wanajua nilikuwa naitwa Mark, sema nikalibadili na kuliweka Alama, kwa kiswahili,”

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: UTAMU WA MADAM JESCA

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU

SIMULIZI FUPI: UCHI WANGU UMENIPONZA