Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2016

Ma Producer wa Muziki Bongo Wana Hali Mbaya Sana – Master J

Picha
Mtayarishaji mkongwe wa muziki nchini Tanzania, Master J amesema watayarishaji wa muziki wa Bongo wana hali mbaya sana kwa sasa.  Master J amejiwekea heshima kubwa kwenye;muziki wa Bongo Fleva, pia amefanikiwa kuwatambulisha wakongwe kibao wa muziki wa Bongo Fleva na Hip Hop ambao wamejiwekea heshima kubwa kwa sasa nchini.  Akiongea kwenye kipindi cha FNL, kinachoruka kupitia EATV, Master J alisema ‘watayarishaji wa muziki Bongo wanahalimbaya sana’.  “Unajua maproducer wanahali mbaya sana sasa, madirector ndiyo wanamiliki magari na majumba. Kama inawezekana wasanii waende kufanya show mikoani na video zao halafu waone itakuwaje,” aliongezea.

Idris Sultan Aeleza Jinsi Watu Walivyofuja Pesa zake na Kumsababishia Hasara

Picha
Mshindi wa shindano la Big Brother Africa 2014, Hotshots Idris Sultan, amevunja ukimya na kuzungumzia tetesi ambazo zilikuwa zinazagaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba kuna mtu alimpatia pesa zake kwa ajili ya biashara lakini akazitumia vibaya kinyume na makubaliano.  Ikumbukwe mshindi huyo wa Big Brother Africa 2014, alipata zaidi ya milioni 500. Pesa ambayo alidai aliitumia kuwekeza katika biashara mbalimbali, na baadae aliweka wazi kwamba pesa hizo zilishaisha.  Akizungumza na Bongo5 Ijumaa hii, Idris amesema ni kweli kuna mtu alikuwa anafanye naye biashara lakini akamwingiza mkenge.  “Kuna watu ambao nimeweza kufanya nao kazi, lakini wakaaribu baadhi ya mambo, nisingependa kuliongelea kwa sababu kuna baadhi ya vitu ambavyo wameviharibu sana, na hawakuweza kuviweka sawa,” alisema Idris. Aliongeza, “Yaani kama kupunyua, hivi vitu vinatokeaga katika sehemu yoyote, kwenye kampuni, kwenye nini. Kuna watu wanaweza wakafuja mali zako au wakafanya ...

Cheapest Hosting Services in Tanzania

Picha

Ben Carson NI NANI?

Picha
Benjamin S.Carson(Kushoto)Katika ikulu ya Marekani 19/06/2008 Daktari Benjamin S. Carson  (amezaliwa tar. 18 Septemba   1951 ) ni daktari na mtaalamu wa Nyurolojia, na pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Nyurolojia kwa watoto katika hospitali ya Johns Hopkins huko nchini  Marekani . Alitunukiwa na raisi medali ya uhuru mwaka 2008 Historia ya elimu Edit Benjamin Solomon Carso alizaliwa katika eneo la  Detroit  katika jimbo la  Michigan . Mama yake, Sonya Carson, aliacha shule akiwa katika daraja la tatu na kuolewa na Robert Solomon Carson, aliyekuwa mchungaji mzee zaidi katika eneo la Tennesee, wakati mama yake Ben akiwa na umri wa miaka kumi na tatu tu. Wakati Carson akiwa na umri wa miaka nane tu, wazazi wake waliachana. Mama Carson aliachwa kuwalea Benjamin na kaka yake Curtis, yeye mwenyewe. Alifanya kazi katika sehemu mbaili au hata tatu kwa mara moja ili aweze kuwatosheleza watoto wake wawili. . [1]  Mwanzoni Carson alikuwa na maisha magumu shuleni...

Tume ya uchaguzi DRC yataka muda zaidi kujitayarisha kwa ajili ya uchaguzi

Picha
Tume Huru ya Uchaguzi Katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (CENI) imeomba muda zaidi wa kujitayarisha kwa ajili ya kuandaa zoezi la uchaguzi wa rais. Mkuu wa CENI Corneille Nangaa amesema anahitaji takribani miezi 16 ili kuandaa kwa njia sahihi uchaguzi ujao wa rais nchini humo. Akizungumza mjini Kinshasa, Nangaa amesema tume hiyo inapaswa kuandikisha wapiga kura na kutayarisha daftari jipya la wapiga kura na kwamba zoezi hilo linahitaji miezi 16. Aidha mkuu wa Tume Huru ya Uchaguzi DRC amesema tume hiyo imewasilisha ombi hilo kwa Umoja wa Mataifa na kwamba azimio 2277 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilihusu ombi hilo. Azimio hilo lilitaka serikali ya DRC iandae uchaguzi wa rais kwa mujibu wa katiba ya nchi. Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo anakamilisha duru yake ya urais tarehe 19 Desemba mwaka 2016. Pamoja na hayo tume ya uchaguzi nchini humo inasema inahitajia zaidi ya dola bilioni moja ili kuandaa uchaguzi wa rais kwa mafanikio. Tangazo hilo...

Mapigano yaanza tena Kordofan Kusini nchini Sudan

Picha
Mapigano yameanza tena kati ya jeshi la Sudan na waasi katika eneo la Kordofan Kusini. Arnu Lodi, msemaji wa waasi wa eneo la Kordofan Kusini ametangaza leo kuwa wapiganaji saba wa kundi hilo la waasi wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika mapigano hayo. Mwezi mmoja umepita tangu yalipotokea mapigano kwa mara ya mwisho baina ya jeshi la serikali ya Khartoum na waasi wa eneo la Kordofan Kusini. Kwa mujibu wa jeshi, mapigano baina ya pande hizo mbili yalianza siku ya Jumatano katika mji wa Oum Sediba. Tangu mwaka 2011 hadi sasa waasi katika majimbo ya Kordofan Kusini na Blue Nile wanapambana na jeshi la serikali ya Khartoum katika majimbo hayo. Mwishoni mwa mwaka jana Rais Omar al-Bashir alitangaza dikrii ya kusitishwa vita katika maeneo hayo na akarefusha muda wa dikrii hiyo kwa muda wa mwezi mmoja. Watu zaidi ya milioni mbili wamebaki bila ya makaazi katika eneo la kusini mwa Sudan kutokana na mapigano na machafuko yaliyolikumba eneo hilo..

Iran: Ulaya itoe ushirikiano katika kupambana na ugaidi na utekelezaji wa JCPOA

Picha
Rais Hassan Rouhani ameutaka Umoja wa Ulaya utoe ushirikiano katika mapambano dhidi ya ugaidi na kusisitizia ulazima wa kutekelezwa ipasavyo makubaliano ya nyuklia (JCPOA). Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa wito huo leo katika mazungumzo na Rais wa Baraza la Seneti la Ubelgiji Bi Christine Defraigne ambaye yuko safarini hapa nchini. Rais Rouhani ameashiria mchango chanya wa Umoja wa Ulaya katika makubaliano ya nyuklia baina ya Iran na nchi zinazounda kundi la 5+1 na kueleza kwamba: makubaliano ya nyuklia ni mwanzo tu wa safari na si mwisho wake; na kitu pekee cha kuifanya mihimili ya makubaliano hayo iwe imara zaidi ni kutekelezwa kwa wakati na kama inavyopasa makubaliano na ahadi zilizotolewa. Rais Rouhani amebainisha kuwa ugaidi ni tatizo kubwa na sugu linaloukabili ulimwengu; na mbali na kubainisha sababu na chanzo chake amesisitiza kuwa pamoja na sababu za kiuchumi na kiutamaduni kama umasikini, ujinga, ubaguzi na kukata tamaa vijana juu ya mustakabali, lakini malalam...

Kiongozi wa upinzani nchini Bahrain aachiliwa huru baada ya kutumikia kifungo cha miaka mitano jela

Picha
Sheikh Mohammed Ali Mahfoudh, Katibu Mkuu wa Chama cha Amalul-Islami nchini Bahrain ameachiliwa huru baada ya kutumikia kifungo cha miaka mitano jela. Mahakama moja ya utawala wa kifalme wa ukoo wa Aal -Khalifa ilikuwa imemhukumu Sheikh Mahfoudh kifungo cha miaka kumi jela, lakini mnamo mwezi Novemba mwaka 2012 mahakama ya rufaa ilitoa uamuzi wa kupunguza adhabu ya kifungo hicho kutoka miaka kumi hadi mitano. Katibu Mkuu huyo wa Chama cha Amalul-Islami alifungwa jela kutokana na malalamiko yaliyotolewa na Waziri wa Sheria wa Bahrain dhidi ya chama hicho. Tangu mwezi Februari mwaka 2011, wananchi wa Bahrain wamekuwa wakifanya maandamano ya amani nchini kote kupinga utawala wa kidikteta wa kifalme wa ukoo wa Aal Khalifa na kuutaka ung'atuke madarakani. Utawala huo umekuwa ukitumia mkono wa chuma kukabiliana na maandamano hayo sambamba na kutekeleza sera za kibaguzi dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia ambao ndio wanaounda asilimia kubwa ya wananchi wa Bahrain. Mamia ya watu ...

Wapinzani Chad wataka kubatilishwa matokeo ya uchaguzi wa Rais

Picha
Wapinzani nchini Chad wamelitaka Baraza la Katiba la nchi hiyo kubatilishwa matokeo ya uchaguzi wa Rais yaliyomrejesha tena madarakani Rais Idriss Deby. Wapinzani sita waliowania kiti cha Urais katika uchaguzi wa hivi karibuni nchini Chad wametangaza kuwa, wamelitaka Baraza la Katiba litengue matokeo ya uchaguzi huo kwani zoezi zima la uchaguzi huo lilitawaliwa na wizi wa kura na udanganyifu. Joseph Djimrangar Dadnadji, Waziri Mkuu wa zamani wa Chad ametangaza kuwa, suala la kukiukwa sheria katika kipindi cha kufanyika uchaguzi na wakati wa zoezi la kuhesabu kura linatosha kubatilisha matokeo ya uchaguzi. Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi ya Chad, Rais Deby alipata asilimia 61.56 ya kura katika uchaguzi uliofanyika tarehe 10 ya mwezi huu na hivyo kupata fursa ya kuiongoza tena nchi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitano. Wakati wapinzani wakitoa malalamiko hayo, wiki iliyopita waangalizi wa Umoja wa Afrika kwenye uchaguzi huo walinukuliwa wakisema k...

Mpenzi wa zamani anavyoweza kukutibulia penzi lako la sasa

Picha
T MEDIA NEWS Mahusiano KATIKA safari ya mapenzi kuna uwezekano mkubwa mtu akawa ameshawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na watu wengi kabla ya kumpata yule sahihi wa kuishi naye kama mke na mume. Rekodi zinaweza kutofautiana kutoka kwa mtu na mtu ila kama wewe umewahi kuwa na uhusiano na zaidi ya mtu mmoja huko nyuma, unatakiwa kuwa makini katika maisha yako ya sasa ili huyo mpenzi wako wa zamani asije akakutibulia. Tumekuwa tukishuhudia mikwaruzano ya hapa na pale kati ya wapenzi chanzo kikiwa ni mmoja kukuta aidha meseji isiyoeleweka kwenye simu ya mwenzake ikitoka kwa mpenzi wake wa zamani au unaweza kusikia mwanaume kamshushia kipigo mpenzi wake baada ya kumkuta akiwa katika mazingira tata na ‘mtu’ wake wa zamani. Hayo yamekuwa yakitokea kila siku lakini chanzo ni wengi kutojua jinsi wanavyoweza ‘kuwahendo’ wapenzi wao wa zamani na kuhisi hata wakiwa karibu nao hawawezi kuwa na madhara. Yawezekana ni kweli huyo mpenzi wako wa zamani hamkuachana kwa sha...

Kabla ya ndoa jiulize, kwa nini umempenda

T MEDIA NEWS Mahusiano Uamuzi wa ndoa si wa kujaribu. Unatakiwa kujihakikishia kwamba ni kweli umevutiwa na kila kitu cha mwenzako, kwamba utakuwa naye katika shida na raha. Hayo ndiyo mambo ya kuzingatia. Nimeshaandika mengi kuhusu sifa za anayetakiwa kuoa au kuolewa, lakini nasogea mbele zaidi na kuangalia sababu za kumpenda mtarajiwa wako katika ndoa.Zipo sababu za msingi sana ambazo unatakiwa kuwa nazo kabla ya kuingia kwenye ndoa KWA NINI UJIULIZE Lazima nifafanue hili kwanza kabla ya kuendelea. Hivi unafikiri ni kwa nini ni lazima kujiuliza sababu za kumpenda mwenzi wako? Yes! Ni kwa lengo la kujiwekea usalama katika ndoa yako ijayo. Kujiandalia amani na pumziko la kweli. Kwenye mapenzi ya dhati pekee ndipo vinapopatikana vitu nilivyotaja hapo juu. Kwa maneno mengine kuwa na majibu ya swali linalosomeka kwenye kichwa cha mada hii ni kujihakikishia ndoa bora. Tuendelee kujifunza. NI MWENZI WA NDOTO ZAKO? Jambo kubwa kuliko yote ambalo unatakiwa kuliangalia kwa jicho la tat...

LE MAJANGAZ BABA WA FAMILIA AJIFUNGUA MTOTO

Picha
Familia inayoundwa na wanandoa Bianca na Nick Bowser, ni familia yenye furaha lakini iliyowashangaza wengi baada ya Nick ( baba wa familia) kupata ujauzito na kujifungua.  Iko hivi; Nick ambaye ana umri wa miaka 27 hivi sasa, alizaliwa na jinsia ya kike na kupewa jina la Nicole na wazazi wake, lakini aliamua kubadilika na kuishi kama mwanaume (transgender/jike dume) tangu miaka saba iliyopita. Na hii ilichangiwa pia na sura na umbo la kiume alilokuwa nalo.  Hali ilikuwa hivyo pia kwa Bianca ambaye ana umri wa miaka 32 hivi sasa, yeye alizaliwa mwanaume na kuitwa jina la Jason, lakini kutokana na kuwa na sura nzuri na umbo la kike, na hisia zake za kutaka kuishi kama mwanamke, alibadili aina ya maisha na kuishi kama mwanamke kamili.  Wawili hao walikutana na kuamua kufunga ndoa huku wakiyabadilisha kabisa maisha ya wana ndoa, Nick akiwa baba wa familia anaevaa na kuishi kama mwanaume. Mkewe Bianca (ambaye ni mwanaume) yeye alibadili na kuishi kama mwanamke kamili akii...

Wananchi Wamelielewa Soma la TCRA...Simu Feki Nchini zazidi Kupungua....

Picha
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema idadi ya namba tambulishi ambazo zilikuwa hazina viwango zimeendelea kupungua kutoka asilimia 30 mwezi Desemba hadi kufikia asilimia 13, Machi mwaka huu.  Kutokana na kupungua huko, inamaanisha kwamba simu feki nchini zinazidi kupungua.  Akizungumza na vyombo vya habari leo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TCRA James Kiraba amesema katika uchambuzi na matokeo ya awali ambacho pia kilishirikisha kampuni za mawasiliano kimeonyesha kuwa mwezi Februari ilishuka mpaka asilimia 18.  Amesema uchambuzi wa Februari ulionyesha idadi ya namba tambulishi ambazo hazikuwa na viwango zilikuwa asilimia tatu, vilevile idadi ya namba tambulishi ambazo zimenakiliwa zilikuwa na asilimia 18, huku simu halisi zikiwa asilimia 79.  "Uchambuzi wa Machi unaonyesha idadi ya namba tambulishi ambazo hazina viwango zilikuwa sawa na asilimia mme, huku idadi ya namba tambulishi ambazo zimenakiliwa zilikuwa asilimia 13. Uchambuzi huu unahusisha kampu...

YANGA VS TOTO,PLUIJM ANENA HAYA...!!!

Picha
KOCHA wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga, Hans Pluijm ametamba timu yake leo kuibuka na ushindi dhidi ya Toto Africans ili kuzidi kukaribia kutetea taji hilo. Akizungumza  wakati wa mazoezi ya timu hiyo jijini hapa, Pluijm alisema kuwa licha ya uzuri wa Toto Africans, lakini wataibuka na ushindi katika mchezo huo wa leo CCM Kirumba. Alisema wachezaji wake mwanzo mwisho watacheza kwa kujituma huku wakilishambulia kwa nguvu lango la Toto African wakisaka pointi tatu muhimu. “Toto African ni timu iliyojaa wachezaji wadogo wanaojituma na wanacheza mpira mzuri sana. Jambo muhimu kwetu ni kuhakikisha tunashinda kila mechi ili tuweze kubaki kileleni mwa Ligi Kuu na kutwaa taji,“ alisema Pluijm. Hata hivyo, Pluijm alithibitisha kikosi chake kuwa na majeruhi, lakini amesema wameziba mapengo hayo. “Golikipa wetu Barthez na Godfrey Mwashiuya ni majeruhi ila nina imani mapengo yao yatazibwa na wachezaji waliopo,” alisema Pluijm. Kwa upande wake kocha mkuu wa...

Mapendekezo Ya Sheria Ya Wazee Kuwasilishwa Bungeni

Picha
NAIBU WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla amesema Serikali imekamilisha mapendekezo ya uundwaji wa Sheria ya Wazee ambayo yatawasilishwa katika mkutano wa Bunge wa Septemba. Dk. Kigwangalla aliyasema hayo jana (Ijumaa, Aprili 29, 2016) wakati akitoa ufafanuzi kwa Viongozi wa Mtandao wa Wazee waliomtembelea Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ofisini kwake mjini Dodoma. Dk. Kigwangalla alisema kuwepo kwa Sheria ya Wazee kutawezesha mambo mbalimbali yanayohusu wazee kutekelezwa kwa mujibu wa sheria hiyo likiwemo suala la pensheni. “Mimi pamoja na Waziri wangu, Ummy Mwalimu baada ya kupewa jukumu la kuongoza wizara tuliunda kikundi cha wazee kwa ajili ya kuamua mambo makubwa mawili ambayo tutayatekeleza likiwemo la pensheni kwa wazee wote,” alisema. Naibu Waziri huyo alisema suala jingine ambalo wamepanga kulitekeleza ni utoaji wa huduma ya bure kwa wazee, ambapo watawapatia bima ya afya ili wasiendelee kusumbuka. Kwa upande wake ...

Abiria Wanusurika Kufa Katika Ajali ya Ndege Mjini Bukoba Leo

Picha
Watu kadhaa wamenusurika  kufa baada ya ndege ya Shirika la Ndege la Auric Air waliyokuwa wakisafiria kupata ajali katika Uwanja wa Ndege wa Manispaa ya Bukoba ilipokuwa ikitua na rubani kupoteza uelekeo  kama inavyo onekana pichani. Ndege hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka Jijini Mwanza ,tukio limetokea majira ya saa nne asuhuhi ya leo Jumamosi April 30,2016.

Aliyejifanya Ofisa usalama wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Atupwa jela Miaka 12

Picha
Mahakama ya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, imemhukumu kwenda jela miaka 12, Qasama Machibya aliyejifanya ofisa usalama wa Taifa kwenye ziara ya Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete mwaka 2013. Kabla ya hukumu, mshtakiwa alijitetea mahakamani hapo kuwa kitambulisho alichokutwa nacho siyo chake na anashangaa kuona kuna picha yake na jina lake. Alidai kuwa hizo ni mbinu za polisi kumminya, hivyo aliiomba Mahakama kumpunguzia adhabu na kwamba ana ugonjwa wa Ukimwi. Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Gabriel Kurwijila alisema utetezi wa mshtakiwa hauifanyi mahakama kutomtia hatiani kwa kuwa hana cheti cha ugonjwa. Alisema kutokana na mahakama kuridhishwa na ushahidi wa upande wa mashtaka uliowasilishwa inamtia hatiani kwa makosa matatu. Kurwijila alisema kosa la kwanza ni kughushi nyaraka ya Serikali hivyo, atakwenda jela miaka mitano na kosa la pili la kujifanya ofisa usalama wa Taifa kifungo chake ni miaka miwili. Alisema katika kosa la tatu la kuudanganya umma kwa kutoa nya...

Makonda Asema hataki kuwaona wasanii nyumbani kwake.......Ni Baada ya Kumtosa kwenye uzinduzi wa kampeni ya usafi

Picha
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema hataki kuwaona nyumbani kwake wasanii ambao wamekacha kuhudhuria kampeni yake ya usafi ambayo imezinduliwa Jumamosi hii katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam. Akizungumza katika uzinduzi huo, Paul Makonda ameonesha kusikitishwa na idadi ndogo ya wasanii waliojitokeza kuunga mkogo kampeni hiyo. “Lakini nashukuru wasanii wote ambao wamejumuika nasi, na kwa kweli hiki ni kipimo cha kuwatambua marafiki zangu wa kweli ni wapi. Na mimi niwaambie tu, sitaki kuona msanii yoyote nyumbani kwangu ambaye hawezi kuniunga mkono kwenye mambo yangu ya maendeleo,” alisema Makonda. “Sitaki hiyo tabia, nimemuona Steve Nyerere hapa amekuja akiwa amechelewa hilo ni onyo, ukirudia tena nakushughulikia. Huwezi kuwa rafiki yangu alafu kwenye mambo kama haya huhangaiki, wengine wanataka waombwe, eti mbona hujanipigia simu kuniomba nipost, we nani?. Swala la usafi siyo la serikali ni swala la kila mtu,”  aliongez...

Rais mstaafu Jakaya Kikwete ametaja mali alizochuma alipokuwa madarakani kwa miaka 10.

Picha
RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE. Kamishna wa Tume ya Maadili, Jaji mstaafu Salome Kaganda ameiambia Nipashe katika mahojiano maalumu katikati ya wiki kuwa Kikwete ameshawasilisha tamko la mali zake tangu aondoke madarakani Novemba 5, mwaka jana. Jaji Kaganda alisema Kikwete aliwasilisha fomu inayoonyesha mali alizozipata wakati akiwa madarakani kati ya 2005-2015, na alizozipata kabla hajangia madarakani kwa Sekretarieti yake. Nipashe ilizungumza na Jaji Kaganda kujua kama Kikwete alishatoa tamko kama Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya mwaka 1995 na kanuni zake zinavyoelekeza, lakini pia kufahamu idadi ya mali anazomiliki Rais huyo mstaafu na thamani yake. Kaganda alisema ni kweli Kikwete aliorodhesha mali zake zote kwa tume lakini Jaji huyo alikataa katakata kumwonyesha mwandishi wa habari hizi tamko hilo. Jaji Kaganda alisema sheria inazuia kumwonyesha mtu mwingine tamko la mali la mtu mwingine hadi kuwe na sababu ya maana ya anayehitaji, na pia kuwe na ulazima wa ku...

CCM Yawataka Wafanyabiashara Kupuuza kauli za Wanasiasa kuwa Rais Magufuli Analengo la Kuwakomoa.

Picha
Chama cha Mapinduzi kimewataka watanzania kupuuza kauli za baadhi ya wanasiasa zinazodai kuwa rais Magufuli analengo la kuwakomoa wafanyabiashara na kinazieleza kauli hizo kuwa ni za uchochezi kwakuwa serikali ya awamu ya tano haina tatizo na wafanyabiashara na watumishi waadilifu bali wanaolihujumu taifa kwa manufaaa binafsi.   Kauli hiyo ya chama imetolewa na msemaji mkuu wa CCM Christopher Ole Sendeka wilayani Simanjiro alipokuwa akizungumza na wananchi wanachama wafuasi wa CCM na viongozi wa mila katika kata ya Shambarai. Kwa upande katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Arusha Shabani Mdoe amewataka wananchi kuwa makini na viongozi wasio waadilifu huku mkuu wa wilaya ya Simaniro Mahamoud Kambona akiwata viongozi wa mila kushirikiana na serikali katika kuleta maendeleo. Katika mkutano huo viongozi wa mila kutoka jamii ya wafugaji pia walipata nafasi ya kupaza sauti na kutaka serikali na jamii iheshimu maamuzi wanayoyatoa kama viongozi katika jamii.

Watu 4 na wengine 29 Wajeruhiwa Baada ya Basi la HBS Walilokuwa Wakisafiria Kupinduka Jijini Mbeya

Picha
Watu wanne wamekufa papo  hapo na wengine 29 kujeruhiwa baada ya basi la HBS linalodaiwa kuwa ni mali ya kampuni ya Sabena walilokuwa wakisafiria kutoka jijini Mbeya kwenda Tabora kuacha njia na kupinduka katika eneo la maji mazuri, barabara kuu ya Mbeya – Chunya wilayani Mbeya.   Basi hilo likiwa limebeba abiria wengi kuliko uwezo wake, lilianza safari yake ya kuelekea Tabora likitokea jijini Mbeya, lakini inadaiwa kuwa likiwa kwenye mtelemko na kona kali za mlima Mbeya likafeli breki na ndipo dereva wake akaamua kuruka na kuliacha likijiendesha lenyewe hali ambayo ilisababisha lipoteze mwelekeo na kuanguka mtaroni. Muuguzi wa zamu katika hospitali ya rufaa ya kanda ya nyanda za juu kusini, Jesca Kahangwa amethibitisha kupokea miili ya watu wanne na majeruhi 29 wa ajali hiyo, huku akidai kuwa hali za majeruhi wengi bado ni mbaya. Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amewahi katika eneo la ajali na baada ya kupata maelezo ya chanzo cha...

WAARABU WAONYESHA KUFURU YA PESA, UNAAMBIWA WANAMILIKI RANGE HII ILIYOPABWA KWA SARAFU ZA DHAHABU.

Picha

Yanga Sasa Haikamatiki...Haya hapa Matokeo ya Leo Dhidi ya Toto Africans

Yanga imeendelea kushinda mechi zake za ligi kuu Tanzania bara baada ya kuifunga Toto Africans ya jijini Mwanza kwa magoli 2-1 kwenye uwanja wa CMM Kirumba, Mwanza.  Toto walianza kupata goli la kwenye mchezo huo lililofungwa na William Kimanzi dakika ya 39 kipindi cha kwanza lakini goli hilo likasawazishwa na Amis Tambwe dakika ya 50 kipindi cha pili.  Yanga walijihakikishia pointi tatu kwenye mchezo huo kupitia beki wao wa kulia Juma Abdul dakika ya 78 na kifanya Yanga kufikisha pointi 65 baada ya kucheza michezo 26 ya VPL.

MR. BLUE: SUGU AMEHATARISHA NDOA YANGU!

Picha
MKALI wa Muziki wa Hip Hop, Bongo Kheri Sameer ‘Mr Blue’ ameendelea kumporomoshea lawama Mbunge wa Mbeya Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambaye pia ni msanii wa Muziki wa Hip Hop, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kuwa usumbufu aliokuwa anampa ili kuiachia ngoma yake ya Freedom ulimsababishia ‘rabsha’ ndani ya ndoa yake.    Shutuma hizo anazozitoa Blue ni mwendelezo wa ‘drama’ inayoendelea kati yake na Sugu ambayo kwa sasa ndiyo habari ya mjini kufuatia madai ya Blue kuwa mheshimiwa huyo alimzunguka kwa kuuchukua wimbo wake huo ambao mwanzo yeye alimshirikisha, akaurekodi upya huku akifuta mashairi yake lakini kama haitoshi ‘akashuti’ video, jambo ambalo Blue analiona kuwa ni uonevu.   “Kwanza Sugu alinisababishia matatizo ndani ya ndoa yangu mpaka nikawa sipokei simu zake. Alikuwa ananipigia simu kila muda na kila siku akiuliza ‘project’ inatoka lini hadi mke wangu akawa a...

Lishe Bora kwa Maisha Yote

Picha
Inajulikana kabisa kuwa nyumba imara hujengwa kwa mchanganyiko wa vitu vingi. Nyumba hii huonekana nzuri na yenye kupendeza wakati wote na pia haimomonyoki kirahisi wakati wa mvua au upepo mkali. Nyumba imara hujengwa kwa mchanganyiko kama wa cementi, mchanga, kokoto, nondo n.k. mchanganyiko huu huwa katika kiwango sahihi, hii ni kwamba kuna kiasi au uwiano sahihi katika mchanganyiko huu. Kimojawapo kati ya hivi kikipelea au kuwa katika kiasi pungufu basi nyumba haitakuwa imara, vilevile kimojawapo kikizidi basi nyumba haitakuwa imara pia. Hivyo nyumba ili iwe imara ni lazima mchanganyiko huu uwe katika uwiano ulio sahihi. Mpaka hapo swali linakujia, je mwili wako unajengwa na nini? je kuna uhitaji wa uwiano sahihi? Mwili wa binadamu hujengwa kwa chakula. Chakula hicho ni lazima kiwe chakula bora au mlo kamili. Mlo kamili unajumuisha makundi matano ya vyakula ambayo ni:  nafaka, mizizi na ndizi , kundi la pili:  vyakula vyenye jamii ya kunde   na vyenye asili ya wanya...

Mtu mkubwa kuliko wote duniani aingizwa kwenye kitabu cha kumbukumbu

Picha
Mtu anayesadikiwa kuwa na umri mkubwa kuliko wote duniani YISRAEL KRISTAL mwenye miaka 112 na siku 178 amepewa cheti na kitabu YISRAEL KRISTAL Mtu anayesadikiwa kuwa na umri mkubwa kuliko wote duniani YISRAEL KRISTAL mwenye miaka 112 na siku 178 amepewa cheti na kitabu cha kumbukumbu cha dunia.(Guiness World Reports) KRISTAL alizaliwa nchini POLAND mwaka 1903 na ameshuhudia vita ya kwanza na ya pili ya dunia kabla ya kuhamia nchini ISRAEL kwenye mji wa HAIFA. Kumbukumbu zilizopita zinaonyesha  kuwa mtu aliyekuwa na umri mkubwa kabisa duniani alikua ni YASUTARO KOIDE wa Japan aliyefariki dunia akiwa na miaka 112 na siku 312. Wakati akipokea cheti hicho Kristal amesema kuwa haelewi siri ya kuishi miaka mingi duniani ila anaamini kuwa yote yanapangwa na MUNGU aliye juu kwani kulikuwa na watu wazuri na wenye nguvu tu lakini leo hii hawapo.  

MBUNGE MWENYE MVUTO ZAIDI KULIKO WENGINE UNAOWAJUA WEWE

Picha

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ( TPDC ) Lakanusha Kufungua Akaunti za ESCROW katika Benki ya Stanbic

Picha
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, linapenda kutoa taarifa sahihi juu ya taarifa ambazo zimekuwa zikiandikwa na vyombo mbalimbali vya habari, pamoja na mitandao ya kijamii kuhusu TPDC kufungua Akaunti za ESCROW katika Benki ya Stanbic. Ni vyema ikaeleweka kwamba, Akaunti ya  ESCROW  ni Akaunti  maalumu inayoweza kufunguliwa  baina ya  Kampuni, Taasisi,  au Mashirika mbalimbali ya binafsi na yale ya umma kwa matumizi maalumu.  Lengo la Akaunti ya ESCROW ni kuhifadhi fedha au kupitisha malipo kwa ajili ya shughuli maalum ikiwemo miradi au kazi yoyote maalumu na malipo haya hufanyika baada ya pande mbili kuridhia. TPDC ilifungua Akaunti tatu za Esrow baada ya Serikali  ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BOT)  kutoa idhini kufunguliwa kwa akaunti kwenye Benki ya Stanbic, ikiwa ni moja ya masharti yaliyowekwa na mkopeshaji ili  kutoa mkopo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mipya ya gesi asilia, kut...

Shirika La Umeme Tanzania Tanesco Lazindua ”Tanesco Huduma";

Picha
Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco), limezindua huduma mpya inayotoa nafasi kwa wateja kutoa na kupata taarifa kupitia mfumo wa mawasiliano uliounganishwa kwenye simu za kiganjani unaoanza kwa majaribio katika mkoa wa kihuduma wa Kinondoni Kaskazini. Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba alisema jana jijini Dar es salaam kuwa, mfumo huo ambao uko kwenye programu maalumu, utasaidia kuboresha utendaji kazi wa shirika. “Mfumo huu utaongeza kasi ya uwajibikaji wa watendaji kuwahudumia wananchi, lakini kwa sasa tumeuanza kwa majaribio katika mkoa wetu wa Kinondoni Kaskazini, wateja wetu watatoa taarifa za matukio yanayowakabili hata wale wanaoomba rushwa, watujulishe tupate ushahidi tuchukue hatua,”  alisema Mramba. Alisema mfumo huo umeundwa kutokana na ushirikiano kati ya Tanesco na Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (Costech) na alisema itawapunguzia usumbufu wateja wa kupiga simu kwenye vituo vya huduma wanapokuwa na malalamiko binafsi a...

Nay Aliachwa na Shamsa Ford Sababu ya Vibomu-Niva

Picha
Msanii wa filamu nchini Niva Super Mariyoo, ambaye alionja joto ya jiwe kwa muda fulani baada ya kutajwa kwenye wimbo wa Nay wa Mitego 'Shika adabu yako' na kusema "Huyo msanii huyo hana hata chumba cha kupanga ila anaishi kwenye gari".  Niva amefunguka na kusema kuwa Nay wa Mitego siku zote huwa anaimba watu maarufu ili apate kiki na kusema msanii huyo kutokana na kufanya nyimbo mbovu mbovu ndiyo maana hata siku moja hajawahi kupata tuzo.  Akizungumza kwenye kipindi cha eNEWS Niva Super Marioo amedai kuwa ni kweli kwa sasa wanawake wengi wanafanya kazi na kutafuta riziki na wanakuwa wanawasaidia baadhi ya wanaume ambao kazi yao kukaa nyumbani kama Imma Chogo ambaye ni (Nay wa Mitego).  "Kimaisha mimi Imma Chogo hajanifikia sema sisi wengine huwa hatupendi kujiweka wazi sana, kama kweli mtu unamiliki nyumba, una kwako kwanini hutulii na familia? kama kweli wewe unajiona ni Gentle Man kwanini wanawake wanakukimbia? Star anakimbiwa? mimi najua Star anakimbiliw...

NAMBA 1 HADI 62 NA MAANA ZAKE KATIKA VPL 2015-16

Picha
Na Baraka Mbolembole Mechi sita za ligi kuu ya kandanda Tanzania bara zitachezwa leo Jumamosi na siku ya kesho Jumapili katika miji tofauti. Kama ilivyo kawaida ya mtandao wako huu wa tawfiqmassin.blogspot.com leo tena tunakuja tofauti. Kumbuka ni timu sita tu kati ya 16 za msimu huu zimewahi kushinda ubingwa VPL. Yanga, Simba, Mtibwa, Coastal, African Sports na Azam FC. Nimekuchambulia ligi yote na kukuwekea katika mtindo wa namba kuanzi namba moja (1) hadi 62. Ni timu moja tu kati ya 16 zinazocheza Ligi kuu ndiyo itapata tiketi ya kuiwakilisha Tanzania Bara katika michuano ya Afrika hapo mwakani. Kwa mara ya kwanza katika historia bingwa pekee wa ligi ndiye atapaa kimataifa.Namba hii inamuwakilisha mlinzi namba mbili wa Azam FC, Shomari Kapombe ambaye amefunga magoli 8 katika VPL hadi sasa na kuwa kinara wa ufungaji upande wa wachezaji wa nafasi za ulinzi. Mlinzi huyo wa Taifa Stars amekosa michezo miwili iliyopita ya timu yake na atakosa pia michezo mitano ya mwisho ku...