MTUNZI : SEIF JABU.
NAMBA : + 258 845018401 wasap.
Sehemu ya tatu.
Baada ya ya kujikabidhi kwa mwenyezimungu nilipiga hatua kuelekea walipokuwa mlango.
" Asalam aleykum."
" Waleykumsalam."
Wote Waliitika na Mama Yasini aliitika na aliitika kwa furaha iliyo sindikizwa na tabasamu.
" Mwanangu Seif ulipoondoka pale kulitokea taflani ya kuibiwa kuni Wanangu wakasema ni wewe ila nimepinga huwezi kuwa wewe."
Nilimuangalia Mama Yasini kisha nikamwambia kwa upole na utulivu.
" Huwezi juwa huwenda ni kawa mimi kwa hiyo Usije enda kushika koo mtu mwingine ili hali huna ushahidi."
" Seif nimekumbuka kuni hizo niliziwasha jana wala Usiwe na hofu."
""Sawa Mama Yasini."
Waliaga wakaondoka ila nilibaki na maumivu moyoni kwani mwizi nilikuwa mimi.
""Ehhhh mwenyezimungu nisamehe kwa wizi ule ila naahidi mbele yako kuwa nitalilipa deni hili la wizi."
Mana aliniangalia kisha akaniuuliza.
" Mwanangu ni kweli umeiba?"
" Hapana mama yangu."
" Mbona una mawazo kiasi hicho ili hali unajua hujaiba?"
" Nina fikilia kwanini wanihisi mimi?"
" Basi tuyaache hayo ingia ndani."
" Mama nimeleta samaki pamoja na unga sijui Kuna mkaa wa kutumia?"
" Mkaa upo."
"Mungu ni mkubwa."
Mama aliwasha jiko akamchemsha yule samaki akatia chumvi kidogo kisha akasonga na ugali akatukaribisha wanawe kula.
"Wanangu mvumilie kwani nimekosa nyanya, kitungu na mafuta."
"Usijali mama yetu."
Tulikula baada ya kula tukaelekea madrasa' nilipoingia darasani kuangalia mbele yangu nilimuona Shemsa aliponiona tu alinyanyuka akanifuata huku akitabasamu.
" Asalam aleykum."
" Waleykumsalam hujambo?"
"Nilikuwa siko sawa ila kwa kuwa nimekuona nadhubutu kusema sijambo."
"Na mimi nimefurahi kukuona karibu sana madrasa."
" Asante nimeisha fika' pale kuna nafasi nimekuwekea twende tukakae pamoja."
" Sawa twende."
Nilimuangalia Shemsa nikafikilia kwanini ametoakea kunipenda kiasi kike ili hanijui kiundani ila katika kuwaza kote nilikosa jibu nikaenda tukakaa akafungua juzuu akaanza kusoma ila kabla hajafika mbali akaniuuliza.
" Seif umeshika udhu?"
" Ndio "
" Tuendelee kusoma na ni naomba tuanzie surat fatiha mpaka Ama."
" Sawa.:
Tulisoma hatimae tukamaliza kusoma tulipo maliza mpaka dakika hiyo mwalimu alikuwa hajafika nilichofanya nilisimama mbele nikatoa salamu baada ya salamu nikaongoza darasa kusoma baadhi ya Dua nilizokuwa najua' nashukuru wanafunzi wengi walikuwa wananipenda na kusikiliza hata niliposimama mbele yao walinisikiliza ilipotimu saa kumi niligonga kengelele wanafunzi wote tukakutana tulipokuwa kuwa tukakutana kila kengelele ilipokuwa inagongwa (mstarini).
Nilisimama mbele nikatoa salamu kisha nikawaambia kuwa kila mmoja aende kwao tutaona kesho saa mbili asubuhi.
" Sawa mwalimu."
Madarasa yote ya chini walikuwa wanapenda kuniita mwalimu kutokana na kuwafundisha sana kwani nilikuwa nimepangiwa kuwafundisha kila siku asubuhi.
Wanafunzi wote Walitoka ila mimi nilirudi darasani nikaendelea kujisomea huku nikisubili kuswali swala ya magharibi kwani ndio ilikuwa kawaida yangu.
Nikiwa darasani nilishituka kuona mtu anakaa pembeni yangu.
" Seif mbona umerudi darasani? "
" Ni kawaida yangu kubaki mpaka niswali swala ya magharibi na siku nyingi huwa natoka baada ya swala ya ishai."
" Alhamdulillah kupata rafiki niliyemhitaji siku zote."
Shemsa aliposema hivyo nilimuangalia ila nikakosa la kumwambia kwani kwa kifupi mimi nilikuwa mtu wa aibu sana.
"Seif fungua kitabu tusome kitakatifu tudurusu (tufanye masahihisho)."
Nilifanya kama alivyosema tukaanza kusoma na Namshukuru mungu kuwa sote tulikutana tukiwa ni wasitaarabu na Vijana tunaomuogopa mwenyezimungu kwani na kukaa kote tukisoma hakuna aliye ingiwa na hisia za kipuuzi.
" Shemsa."
"Abeee."
" Twende nikusindikize masaa yamekwenda na jinsia yako si vizuri ukachelewa nyumbani."
" Sawa."
Nilimsindikiza Shemsa mpaka kwa tulipo fika mlango nilimuaga.
"Shemsa nikutakie usiku mwema wacha niwahi swala ya magharibi msikitini."
" Siyo vizuri ukiishia hapa."
" Naelewa ila utaniswamehe na unisalimie mama."
" Basi nisubili kidogo nije."
" Sawa."
Nilimsubilia kama alivyo niomba ila kabla Shemsa hajarudi Humudu alinikuta balazani akaanza kunishambulia kwa maneno.
" Wewe kapuku umefuata nini hapa? "
"Namsubili Shemsa kaniambia nimngoje hapa."
" Hivi ukijiagalia unaona una hadhi ya kukanyaga katika kibalaza chetu?"
" Nisamehe nimekosea."
Nilimtaka msamaha kisha nikatoka sakafuni nikasimama chini.
Akiwa anaendelea kunitukana Shemsa alitokea na yeye alishuhudia na kusikia baadhi ya matusi.
" Humudu unamtukana Seif kakukosea kitu gani? "
"Hivi dada yangu Shemsa wewe ni kuvutana na huyu fukala ukamleta hapa? Sitaki kumuona hapa tena asije tuletea kunguni na chawa hapa tukaikimbia nyumba."
"Humudu funga demo lako inatosha kama nidharau imetosha na kuanzia leo labda nikwambie kitu kimoja ni kuwa nimekukana toka moyoni mwangu kuwa wewe siyo ndugu yangu tena."
Shemsa aliongea mpaka akaanza kulia nikamshika nikamfumbata mikononi mwangu kisha nikamwambia.
"Shemsa usiitese nafsi yako kwa ajiri ya mambo ya Dunia bali itese kwa kumuhofu mwenyezimungu na kujilinda kumkosea."
Shemsa alilia kwa hisia za kweli mpaka na mimi chozi lilinidondoka ila nikalifuta ili asibaini hilo.
" Shemsa kapumzike wacha nikaswali."
" Sawa ila nisamehe"
" Yameisha wala usihofu."
""Chukua kuna zawadi yako humu."
" Asante."
Nilielekea msikitini nilipomaliza ibada nilirudi nyumbani ila nilipo fika nilikuta mama kazunguuka na wanawake wa Mtaa ule wanamtukana huku wanamsukuma sukuma.
"Masikini usiye na mbele wala nyuma wewe ni wa kutudhurau sisi tunakwambia fanya hivi hufanyi?"
Niliwasogelea kisha nikatoa salamu.
"Asalam aleykum."
" Ona na kindembile chake sijui kinamsalimia nani?"
"Mwanangu ingia ndani."
Mana alinitaka niingie ndani ili nisiendelee kusikiliza matusi wanayomtukana kwani yalikuwa ya nguoni na mazito.
Itaendelea........