SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 30 Novemba 2017

T media news

STORY : MKE MWEMA. SEHUMU YA 4



MTUNZI :  SEIF JABU

NAMBA : + 258 845018401 wasap.

Sehemu ya nne.

Like yako ndiyo inafanya hadithi hii ipostiwe hivyo basi like ili iendelee...

Hakika niliumia sana kuona yanayo mkuta mama yangu ili hali najua hana kosa lolote.

"Halima mama kafanya nini mpaka atukanwe kiasi hicho?"

" Alikuwa hayupo aliporudi akaitwa akaambiwa kuwa anatakiwa kuhamia nyumba ya nyuma ile ya chumba kimoja akahoji ataishi vipi na watoto katika chumba kimoja basi ndio wakaanza kumshambulia kwa maneno mpaka sasa."

" Bibi yupo?"

" Yupo na amenyamanza kimya."

Nilijuliza tunateswaje ndani ya nyumba ya bibi yetu ili anajua sisi hatuna ndugu zaidi yake hapa mwanza.

Nilitoka nikamuangalia mama yangu anavyo sukumwa huku akitukanwa nikaumia sana nikamfuta nikamshika mkono kisha nikatoa sauti kama kiume nikawauliza.

" Mnahitaji nini kwa mama yangu mpaka mumshambulie?"

"Ahame humu ahamie chumba cha nyuma."

" Kafanya kosa gani?"

" Anatuumiza mapua na vyakula vyake kijinga leo kutumia mawese kupika basi nyumba nzima inanuka mawese isitoshe jana kapika dagaa kwa kuzichemsha akasababisha mwanangu kaugua mafua yasiyo poa."

Nilimgeukia Mama yangu kisha nikapiga magoti mbele yake nitamwambia kwa unyenyekevu.

" Mama naomba tuhamie chumba kile cha nyuma ili tuache kusababisha maradhi kwa ndugu zetu hawa kutokana na vyakula tunavyokula kuwazuru."

"Mwanangu wewe umekuwa dada yako kakuwa tutachangia chumba kimoja itawezekana?"

"Mama yangu tuhame tusije tukawa sababu ya kwenda motoni kwa kuwakosesha amani viumbe wa mungu' kwani kila mmoja ataulizwa aliishi vipi jirani yake? Mama yangu tuhame tuwape amani ili waweze kutekeleza ibada bila kikwazo."

Mama aliniangalia kisha akaniambia basi anzeni kuhamisha vitu ili tuwapishe.

Hatukuwa na vitu vingi vya kuhamisha tulikuwa na vigodoro vilivyo kuwa vimeisha isha na na nguo chache na vyombo vichache visivyo jaa hata kwenye beseni.

Tulihamia upande wa nyuma ila hali ya chumba haikuwa salama kabisa kilikuwa chumba cha kilichojengwa kwa udongo na kilikuwa cha zamani sana mpaka kilikuwa tayari na nyufa nyingi sana na ukuta wa upande wa kushoto ulionekana ni kuanguka leo au kesho' chumba hicho kiilikuwaga kikitumiwa kama jicho kabla hakijachakaa na kuoneka hakifai.

Siku hiyo nililala nje kwani niliona kulala chumba kimoja tukiwa wote haitawezekana.

" Mwanangu Seif mbona Umekuja kulala nje."

"Haina shida mimi ni mtoto wa kiume."

"Sawa usiku mwema."

Mama alijiongeza akarudi ndani na mimi nikajiweka kwenye mkeka nikajifunika shuka nikaomba ulinzi kwa mwenyezimungu kisha nikalala.

Usiku ulienda vizuri saa kumi na moja nilikuwa msikitini nikifanya sunaa mbali huku nikisubili muda wa ibada.

Nikiwa msikitini nilikuwa nikimuomba mwenyezimungu anisemehe mazambi yangu na anisamehe kama niliwahi kumkwaza kiumbe yeyote yule.

Baada nilirudi nyumbani nilipofika nilimkuta Mama akiwa anafanya usafi nikamtolea salamu kisha nikakaa kwenye chini nikamuuliza mama.

"Hivi Mama yangu ikitokea nafasi uombe kitu kimoja kwa mwenyezimungu utaomba nini?"

Mama aliniangalia bila kupepesa maneno akaniambia.

" Nitaomba faraja ya moyo wangu na pepo iwe makazi yangu ya kudumu"

" mama unahisi hatuhitaji maisha mazuri?"

" Mwanangu kuna wenye magumu kuliko hata sisi hapa sasa kwanini tusimshukuru mwenyezimungu kwa Neema alizotupatia."

" Ni kweli mama."

Tulibadilishana mawazo kidogo na mama yangu mda wa kwenda madrasa ulipofika tulimuacha nyumbani sisi tukaelekea madirasa.

Nilipofika mlangoni kabla sijaingia nilishikwa na mkono na Vijana wawili niliokuwa nasoma nao madrasa wakanivutia pembeni' sikujua niya yao niliwafuata.

" Sikia wewe hebu tueleze wewe na yule binti wa kiarabu mko vipi?"

""Ni rafiki yangu tu kwani Kuna tatizo limemkuta?"

Si kupewa jibu la maneno bali nilipigwa makofi ya shavuni kama matatu kisha wakaniambia.

"Ole wako tukuone unakuwa karibu naye tena."

Waliondoka wakaingia madrasa nikabaki nashangaa' sikushangaa kupigwa makofi laah bali kilichonishangaza ni kufikilia kumbe na madrasa kuna Vijana wanamna hiyo? Nilitoka nikaingia darasa huku nikamshukuru mungu Kwa yaliyotokea.

Nilipoingia darasani tu Shemsa aliinuka akinifuata na kuni salimia kisha akaniomba tukakae pamoja kuna nafasi ila nilipowaangilia wale Vijana walininyoshea vidole kuashiria wataniadhibu.


Itaendelea.............