SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 30 Novemba 2017

T media news

Asante Umoja wa Ulaya. Serikali yetu imwajibishe kila anayejihusisha na rushwa.

Waraka toka Mlimani

Rais Dkt Magufuli ambaye mapema juma hili juhudi zake za kupambana na rushwa ambazo zimeanza kuzaa matunda zimepongezwa na Umoja wa Ulaya (EU)

Mapema juma hili, Umoja wa Ulaya (EU) umempongeza Rais Magufuli na mikakati yake katika kupambana na rushwa na kumuahidi kumuunga mkono zaidi.

Pamoja na pongezi hizo imetoa msaada wa shilingi bilioni 40 bilioni za Kitanzania katika kupambana na rushwa. Balozi wa EU nchini Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) amesema kuwa fedha hizo zitatumika katika mpango wa “Ongeza uwajibikaji kwa kupambana na rushwa na kuchukua hatua za kisheria.” Hakika, ni matumaini ya walio wengi kuwa serikali itahakikisha mkakati huo unatekelezwa kikamilifu.

Siku za hivi karibuni kumekuwa na idadi kubwa ya watu wakishtakiwa kwa makosa ya rushwa na uhujumu uchumi nchini. Mfano wa watuhumiwa wa kesi hizi za rushwa ni mfanyabishara Yusuf Manji na wengine ambao wana orodha ya makosa madogo na mashatka mengine makubwa yakihusishwa na majina yao lakini bado wapo uraiani, wakiwa huru. Watu wa namna hii na wengine kama “wazee wa Escrow” kina Harbinder Sighi Sethi na James Rugemalira wameliibia taifa mamilioni na hata mabilioni y fedha na serikali haipaswi kuwa na mswalie Mtume kwani ni aina hii ya watu ambao wamesababisha Watanzania kukosa huduma bora walizostahili kupata.

Wito kwa serikali ni kuwatizama kwa jicho la karibu zaidi watu hawa na pia ihoji uzalendo wa wale ambao mara kwa mara wanakamatwa kwa makossa ya kuhujumu uchumi wa Taifa letu.  Kwa mara nyingine tena pongezi ziende kwa serikali chini ya Rais Dkt Magufuli kwa kuelekeza fedha za EU katika kupambana na rushwa, na mafanikio ambayo sasa tafiti zinaonyesha rushwa inapungua nchini. Matarajio ya wananchi ni kuona kazi hii njema inaendeleea bila upendeleo wala kusita kwa namna yoyote katika kufuata sharia.

Mpaka wakati mwingine …