Ilikua ni wakati wa kuufungua Msikiti mpya uliojengwa katika jimbo la Mtama linaloongozwa na Mbunge Nape Nnauye ambapo waliohudhuria ni pamoja na Mufti wa Tanzania mwenyewe, Waziri wa zamani Benard Membe na wengine.
Kwenye ufunguzi huo Nape Nnauye alinukuliwa akisema “Sisi Wanasiasa wakati mwingine tunawasha moto mwingi mno tunashindwa kuuzima lakini kupitia Dini zetu hizi kama mambo yakiwekwa vizuri mioto mingi inazimika na mambo yanakwenda vizuri“
“Tumeanza kuona wakati mwingine tunafanya chaguzi zetu, watu wanakatana mapanga, watu wanapigana…. wanashutumiana, hili jambo sisi Wanasiasa tunaweza tukashindwa kulihimili lakini nyinyi viongozi wa dini mkisimama mkatusaidia inawezekana sababu watu hawa wanatoka miongoni mwetu humuhumu“