Aliyekuwa mgombea urais wa CHADEMA 2015 Edward Ngoyai Lowassa ambaye alihama CCM, ameweka wazi taarifa za kutaka kurudi CCM, na kusema kwamba hana mpango kabisa na wala hafikirii kurudi CCM.
Lowassa ameyasema hayo kufuatia kauli iliyotolea na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho ambo, kwamba Lowassa ana mpango wa kurudi CCM kama baadhi ya wananchama wengine wa CHADEMA walivyofanya, na kusema kwamba taarifa hizo hazina ukweli wowote na haitakuja tokea.
“Hizo habari ndio nazisikia kutoka kwenu, taarifa hizi si za ukweli na uongo mtupu, sijaomba kukutana na rais, nashangaa kwa nini mkuu wa mkoa mzima anasema uongo mkubwa kiasi hicho, na anaachiwa bila kuchukuliwa hatua”, amesema Edward Lowassa.
Edward Lowassa ameendelea kwa kusema kwamba kitendo cha Mrisho Gambo ambaye ni mkuu wa mkoa wa Arusha kusema hadharani kwamba Lowassa amemuomba amkutanishe na Rais Magufuli kwani anataka kurudi kwenye chama, ni kitendo kisichofaa kwa kiongozi mkubwa kama yeye, na kumtaka aache mara moja kwani yeye sio msemaji wake.
“Ni jambo la jabu sana, nataka kumwambia Mrisho Gambo aache uongo sina mpango wa kurudi CCM na siihitaji CCM, wananchi wapuuze maneno hayo, ni uongo, anastahili kuchukuliwa adhabu, nasikitika sana Gambo anataka kuchukua wajibu ambao sio wake, haihitaji kuwa msemaji wangu na wala simuhitaji kuwa msemaji wangu, naiheshimu sana ofisi ya mkuu wa mkoa nategemea atashughulika na ofisi ya mkuu wa mkoa inayomuhusu, badala ya kutoa maneno ya uongo mtaani”, amesema Edward Lowassa.
Hivi karibuni Mrisho Gambo alisikika akisema kwamba amefuatwa na baadhi ya watu ambao wametumwa na Lowassa, kumuomba amsaidie kukutana na Rais Magufuli ili aweze kurejea CCM, kwani uamuzi ambao aliufanya mwaka 2015 wa kuhama chama ulikuwa ni uamuzi wa hasira.
Chanzo: EATV