SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 26 Novemba 2017

T media news

Story: MKE MWEMA.

5
MTUNZI : SEIF JABU

NAMBA : + 258 845018401.

Sehemu ya pili.



Endelea nayo.

Nilimuinua Shemsa kutoka chini ila nilikuwa kwenye mfadhaiko furani ila baada ya kubaini hilo nilitaka mungu msamaha na kisha nikatubia kosa langu.

"Eee mwenyezimungu muumba wa mbigu na aridhi na vyote vilivyomo nisamehe kwa kuyaelekeza macho yangu kusiko faa kuelekeza."

Shemsa aliniangalia kisha akaniuuliza.

""Unaitwa nani?"

" Naitwa Seif."

" Seif tumlaani shetwani kwani nyoyo zetu zimeingia mchanga furani wa vumbi kama tusipo muweka mungu mbele basi tutajikuta tunakuwa wakosefu mbele ya mungu."

"Ni kweli kabisa."

Msemo wa Shemsa ulikuwa unamaana kubwa sana ila kwa mtu muelewa. Kwa kukufumbua macho ni kuwa sote mimi na Shemsa tulikuwa tumetokea kupendana kwani macho yetu yaliongea na nafsi zetu zikatafsili.

"Shemsa tushikamane katika mambo ya heli na masomo tuwe marafiki wa kudumu na mimi Nakuahidi nitakulinda na kukuheshimu mpaka pale mungu atakapo jalia kutuonesha njia iliyo sahihi kufikia wakati wa kuitana wachumba."

" Seif una matamu yakujenga na sio kubomoa ila naomba nikuulize jambo?"

" Uliza."

Tulijikuta tunakaa chini na kuanza kuongea na kusahau kama tulikuwa tunasubiliwa kupeleka jibu.

"Seif urafiki wetu utakuwa wa aina gani?"

" Utakuwa ni urafiki wa kutakiana mema na kushauriana mema ila pia utakuwa ni urafiki wa kusubili au utakao kuwa na ahadi ya ndoa ndani yake."

"Amina tuombe mungu atuongoze katika heli na tusije kumuasi kipindi chote cha urafiki wetu."

"Sawa inshaallah."

" Seif twende tusije chelewa nikamkasirisha Dada Najma."

" Sawa."

Tuliondoka tukaelekea tulipokuwa tumewaacha wenzetu ila tulipo fika tulishangaa kukuta hawapo hata tulipoenda kuangalia ofisini tulikuta hawapo.

"Seif wameenda wapi?"

" Sijui?labda watakuwa wameenda nyumbani."

"Kwani tumechelewa sana.?"

"Tumemaliza karibia dakika 30"

"Watakuwa wameendoka."

" Basi sawa Seif acha mimi niwahi nyumbani."

" Na mimi pia wacha nifike nyumbani maana saa nane inatakiwa niwe nimerudi madrasa."

" Sawa kwaheli."

" Sawa."

Tuliagana ila nikasimama nikajiuliza kwanini arudi peke yake? Nikaona siyo vizuri wacha nimsindikize.

""Shemsa wacha nikusindikize."

"Sawa twende."

Tuliondoka ila tulikuwa kimya sana hakuna aliyekuwa anaongea na kila mmoja alikuwa ana haibu ya kumuanza mwenziye.

"Seif nimefika ni pale."

"Sawa acha nirudie hapa."

"Twende mpaka nyumbani japo upate hata maji ya kunywa."

Sikupinga kweli nilimfikisha Shemsa kwao nikamkuta mama nijamsabahi akaitika vizuri akanikaribisha nikakaa kwenye kiti.

"Shemsa mletee juice mwenziyo."

Nilipewa juice nikanywa kisha nikaaga ila kabla ya kutoka mama Shemsa akamuita mwanaye wa kiume anaitwa Humudu.

"Humudu Humudu..?"

" Namuuuu..."

" Msindikize mwenziyo"

Humudu alitoka na mimi ndani kwa nia ya kunisindikiza ila tulipofika balabalani alianza kunitukana.

" Yaani mama ananisumbua kuja kusindikiza kapuku kama wewe?"

Sikumjibu nilinyamanza mpaka nikafika nyumbani nilipofika nilimkaribisha.

" Karibu tumefika mimi ninaishi hapa."

" Ndio unaishi hapa kwenye vichuguu?"

" Ndio "

"Aya kwaheli."

Umudu aliondoka ila nilibaki naumia moyoni na kujutia ni kwanini nilikubali anisindikize mpaka nyumbani.

Niliingia ila nilipofika nilikuta mama yangu analia akiwa peke yake nikashituka nikamuuliza.

" Mama mbona unalia"

" Hapana mwanangu."

" Mama usinifiche niambie ukweli."

"Mwanangu najua kuwa toka jana usiku hamjala kwa hiyo ninapo waona katika hali hiyo mimi naumia sana dada yako katoka chuo njaa inamuuma na mdogo wako naye hivyo hata wewe pia najua unahisi njaa."

" Mama usilie acha nitoke nikirudi huenda mambo yakawa mazuri."

" Mwanangu unakwenda wapi?"

" Vuta subira mama nakuja."

Nilitoka nje hakili yangu ikazuunguka niende wapi nifanye nini ili tupate chakula? Nikapata jibu huwa Mtaa wa pili kuna wakina mama wanakaanga samaki na ukiwapelekea kuni wana kupa samaki aina ya panki' kwa wakazi wa mwanza najua wanazijua samaki hizo.

Sikuwa na pa  kutoa kuni kutokana na kuwa tulikuwa tunaishi mjini ila nilichofanya nilikwenda nikapenyeza uchororo nikatokea  nyuma ya nyumba moja ya mama Yasini muuza samaki Nilichofanya nilitembea kwa tahadhari nikaenda nikaiba kuni kwenye store (stoo) kisha nikaondoka nikatokea upande wa pili balabalani nikapeleka kuuza kuni hapo hapo kwa Mama Yasini.

"Nimekuletea kuni mama"

" Asante kuni nzuri sana mwanangu nitakupa samaki ya mnofu."

" Nitashukuru mama yangu."

Alinipatia samaki ya mnofu moja na samaki aina ya mapanki vipande viwili ila nikamuomba samaki ya mnofu abaki nayo anipatie pesa kidogo na yeye akakubali bila kipingamiza nikaondoka mbio mbio nikaenda kununua unga na vinyanya kisha nikaanza kukimbia kuelekea nyumbani ili niwahishe mama apike tupate mulo maana ndugu zangu walikuwa hoi kwa njaa.

Niliishiwa nguvu nilipo fika nyumbani nilimuona Mama Yasini akiwa nyumbani pamoja na watoto wake wawili kiume na waliponiona wakanisota vidole wakioneshana nitajua tayari mambo yamehalibika nilicho sema nilisema *Eehh muumba wa mbigu na aridhi niliyomo nilinde na Sharii za viumbe wako hasira zao uzipoze wasije nidhuru wala kuniabisha*


Itaendelea....................