Ili uweze kufuga kuku Bora kuna mambo machache yafuatayo yanayohitajika:
Ujenzi wa banda bora kwa kuzingatia vipimo sahihi kitalamu, ingia fursa101.co.tz tutakuletea watalaamu.
Uchaguzi wa kuku wazazi wenye sifa na Afya nzuri.Udhibiti na tiba za magonjwa mbalimbali kwa kuzingatia ratiba sahihi za chanjoUlishaji bora kwa waakati na Chakula kiwe na viin lishe vyoteUzingatiaji Wa usafi Wa banda na vyombo
SIFA ZA BANDA BORA LA KUKU
Liingize mwanga na hewa muda woteLiwe Kavu daimaLiwe na nafasi ya kutosha kuanzia vipimo vya upana 3M na urefu 4/5M kuku wasibananeLiwe la Gharama Nafuu lakini la kudumu unaweza ukatumia Mabanzi, mbao, mianzi, matofali katika ukuta na paa tumia Vigae, Bati na nyasiLiielekeze kuzuia upepo na mvua pia kuzuia wanyam na wadudu hatari kwa KukuLiwe na nafasi ya kuweka vyombo vya Chakula na ndani kuwe na maranda, bembea, vichanjaKuwe na Uzio mpana angalau mita 10*12 ili wapate mahala paa kuota joto
Ukihitaji huduma ya kutengenezewa mabanda, karibu Fursa 101 ukutane na watalaamu.
EPUKA VIFO VYA KUKU KWA KUFANYA YAFUATAYO
Osha banda na vyombo kwa dawa kama V-RID kila baada ya miezi 3/6 ili kuua bacteria nkChanja kuku chanjo zifuatzo Mahepe (Mareks ) kuanzia siku Ya 1-3 ,Mdondo siku 3-7 utarudia siku Ya 21,Gumboro siku 14 na Ndui siku ya 28
NOTE: Chanjo ya kideri utarudia kila baada ya miezi 3.
Wape Vitamin Kama Multivitamin, vital stress au maji ya molasses ya ungaUsafi Wa banda ni muhimu epuka watu kuingia bandani ukiweza kuwe na mavazi maalumu kama Overall, magumu yatakayofuliwa kwa dawa maalumu kwa ajili ya mfanyakazi na wageni wanaotembelea
Kwa mahitaji ya dawa mbalimbali…Fursa 101 inakuja na soko la bidhaa za mifugo yote. Unaweza kununua vyakula, madawa mpaka kuku wa kufuga kupitia www.fursa101.co.tz
Endelea kutembelea kwa bidhaa mpya zinazokuja kila siku. Unaweza kununua kila kitu mtandaoni na ushauri bure…