Mtunzi: SEIF JABU.
Namba: + 258 845018401 wasap.
Sehemu ya 1.
Anza nayo.
Mama alikuwa anakawaida ya kuamka asubuhi na mapema kwa ajiri ya swala ya alfajiri na kila alipoamka alikuja kutuamusha wanawe kwa ajiri ya kwenda msikitini kuswali swala ya alfajiri.
" Seif mwanangu shikilia ibada Dunia siyo rafiki wa kudumu."
" Sawa mama ila Kwanini usiniache nikaswalia hapa nyumbani?"
" Mwanangu mtoto wa kiume huswalia msikitini."
" Mama kwenda msikitini peke yangu nakuwa na hofu Dunia imebadilika matendo ya ajabu kila siku yanatokea."
"Mwanangu Seif muamini mungu pekee na jua kuwa kila upigapo hatua kuelekea msikitini malaika wa mungu wanakuwa wamekuzunguuka na kukupa ulinzi usio na shaka."
" Sawa mama yangu basi wacha niwahi jamaa."
"Inshaallah.
Hayo ndiyo yalikuwa maisha ya nyumbani yalikuwa ni maisha ya kumtumainia mungu na yenye furaha japo tulikuwa mafukara.
Tulipitia mateso mengi sana katika jiji la mwanza ila tuliyavumilia mimi pamoja na familia.
Tuliitwa wakimbizi, mafukara, wezi, kifupi kila mmoja alituita alivyopenda ila mama yangu hakukata tamaa alisimama imala.
Nilikwenda msikitini nilipo fika nilishika udhu kisha nikaingia msikitini nikaswali rakaa mbili za sunah kisha nikasubili jamaa' baada ya swala sheikh alinifuata akaniambia.
" Asalam aleykum."
" Waleykumsalam."
"Napendezwa na kufanya kwako ibada kwani vipindi vyote unahudhulia tena unahudhulia kwa muda muafaka jina lako ni nani nataka nikuunge na wenzio uwe unasoma hapa madirasa."
Nilifurahi sana bila kipingamizi nikakubali na kweli baada ya siku mbili mbele nilianza kusoma madirasa.
Nilimshukuru mwenyezimungu kisha nikamwambia shida nyingine nikamuomba anisaidie niweze kupata Elimu ya Dunia.
" Ewe mungu nakuachia wewe kwani wewe ndiye mpaji na utampa umutakaye na unamnyima umtakae' mungu nitakubali jibu lolote kutoka kwako ikiwa ni kupata au kukosa vyote Nitashukuru na kusema Alhamdulillah."
Imani yangu kipindi hicho ilikuwa juu kabla ya kugeuza ukurasa wa maisha yangu na kafuata maisha Dunia.
Mungu aliitikia Dua yangu nikakutana na mzee mmoja msikitini akanilingania (akanihusia) kuhusu Dini kisha baada ya hapo akanipa hongera ya kuwa mtoto mdogo ninae swali vipindi vitano kwa siku, Baada ya hapo akaniambia chagua jambo ulilolikosa katika maisha yako na unatamani ulipate kama nikiwa na uwezo nalo nitalikupatia.
"Kila siku natamani nipate elimu ya Dunia pia kwani elimu zote ni muhimu kwetu binaadamu."
" Kama ni hilo umelipata kesho tukutane hapa twende ukapate vipimo vya nguo za shule kisha nitakupeleka kuanza kusoma shule ya msingi mwenge na pia na ndugu yako mmoja nitawasomesha nyote wawili."
" Asante sana."
Kweli malengo yalikamilika na bila kuchelewa nilianza kusoma shule ya msingi mwenge na dada yangu akapelekwa shule ya msingi makongoro.
Nilimshukuru mungu Kwa kujibu maombi yangu nikamshukuru mama yangu kwa kunipa matumaini ya ushindi.
**************
Siku zilikatika na maisha yakasonga mbele hatimae miaka minne ikapita na nijafanikiwa kuingia darasa la nne , na upande wa madirasa nilizidi kufanya vizuri napo nikasogezwa daraja mpaka darasa la pili.
Siku hiyo nikiwa nje ya madirasa naongea na dada yangu Halima walikuja mabinti watatu wa kiarabu wakatoa salamu kisha mmoja wao aliyekuwa mkubwa kati yao akaniuliza.
" Tunahitaji kujiunga na madirasa Kuna utaratibu gani?"
" Utaratibu ni kulipia 500 kwa wiki."
500 ya wakati huo ilikuwa na dhamani kubwa sana kwani kilo ya mchele ilikuwa sh.30 na soda ilikuwa tsh15.
" Sawa tuko tayari kulipia ofisi ziko wapi?"
"Ngoja niwaitie Ustadhi Hamisi kwake si mbali ni nyuma ya msikiti."
"Sawa' Shemsa msindikize."
Najima aliyekuwa mkubwa alimwambia mdogo wake wa kike aitwaye Shemsa anisindikize na yeye akafanya hivyo.
Tulienda pamoja mpaka kwa Ustadhi Hamisi nitamwambia kuhusu ugeni akadai turudi baada ya dakika chache atakuja.
Tulianza kurudi maeneo ya chuo na ila tukiwa njiani kwa bahati mbaya Shemsa alijikwaa akanguka akateguka.
"Mamaaa nimeumiaaa."
" Pole sana."
Nilimwambia huku nikimpa mkono ili nimnyanyue lakini akashindwa kutoka chini nilicho fanya nilishika mguu ili niunyoshe ila kwa bahati mbaya nikawa nimeona Sehemu ambayo hayikuwa na ruhusu kuyiona akili yangu ikahama mwili ukanisisimka nikabaki kama mtu aliyepingwa shoti.
" Niinue hapa."
Itaendelea...................