Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bi. Stella Tullo Chagi kuwa Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba wa Wilaya.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi huu umeanza tarehe 25 Novemba, 2017.
Kabla ya uteuzi huu Bi. Stella Tullo Chagi alikuwa Msajili Msaidizi wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
30 Novemba, 2017