SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 27 Novemba 2017

T media news

Nawashangaa Wanaonishangaa Mimi Kucheka Mahakamani Wakati Lulu Anaukumiwa Hata Mimi Nililia Wakati Wengine Wakila Bata- Mama Kanumba

MAMA wa aliyekuwa mwigizaji mahiri wa Bongo Movies, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amefungukia cheko alilolitoa mahakamani wakati wa hukumu ya mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Mama Kanumba aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, anawashangaa wanaomshangaa yeye kucheka, lakini akawataka wakumbuke kuwa hata yeye alilia mno wakati werngine wakila bata.
Mama Kanumba alisema kuwa, baada ya Lulu kuhukumiwa kifungo cha kwenda jela miaka miwili kwa kusababisha kifo cha Kanumba bila kukusudia, alijikuta akicheka, lakini hakumaanisha kuwa anafurahia Lulu kwenda jela kwa sababu yeye ni Mkristo hivyo hapaswi kushangilia mabaya ya mwanadamu mwenzake.
“Nawashangaa wanaoona nilivyocheka ilikuwa kosa, kwani mimi nililia mara ngapi?” alihoji mama Kanumba.