Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2017

Dar yaibuka kinara kwa fursa za kibiashara Afrika

Picha
Bara la Afrika limekuwa moja ya kitovu kikubwa cha uwekezaji duniani. Baadhi ya nchi barani Afrika zimekuwa na nafasi nyingi za uwekezaji zaidi ya nyingine. Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na ‘PricewaterhouseCoopers’ (PwC) imelijata Jiji la Dar es Salaam kuwa ndilo linaloongoza zaidi na kuyashinda Majiji mengine yalioendelea barani Afrika kwa kuwa na fursa nyingi za kibiashara na uwekezaji. Ripoti hiyo imeeleza pia kuwa Jiji la Lusaka nchini Zambia linashika nafasi ya pili huku Jiji la Nairobi- Kenya na Jiji la Lagos- Nigeria yakifungana katika nafasi ya tatu. Jiji la Accra- Ghana limeshika nafasi ya tano, Abidjan– Ivory Coast nafasi ya sita wakati Kigali ya Rwanda imeshika nafasi ya saba. Nafasi ya nane imeshikiliwa na Addis Ababa- Ethiopia, ikifuatiwa na Kapala- Uganda na nafasi ya kumi inashikiliwa na Jiji la Cairo- Misri. Sababu tano zilizotajwa kuwa chanzo cha Majiji haya kuwa na fursa mbalimbali za kibiashara zaidi ya mengine ni pamoja na uwepo wa soko kub...

Waliopanga Ratiba ya Ligi Kuu Kuwajibishwa na TFF

Picha
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Alfred Kidao amesema kuwa ameagizwa na rais wa Shrikisho hilo, Wallace Karia kumwandikia barua Mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi ili kuwaadhibu viongozi wa Bodi ya Ligi waliohusika na kupanga ratiba. Kumekuwa na malalamiko kutokana na Bodi hiyo kupanga ratiba ya ligi ambapo walishindwa kuzingatia kuwa kuna michezo ya kimataifa ambayo itahusisha timu za taifa jambo ambalo limesababisha baada tu ya mchezo mmoja tu, ligi hiyo ikapanguliwa tena. “Nimeagizwa na rais nimwandikie barua mtendaji mkuu wa bodi ya ligi ili aweze kuwachukulia hatua viongozi wa bodi hiyo waliohusika na kupanga ratiba hii pamoja na kwamba walikuwa na kalenda lakini bado wamekosea,” alisema Kidao. Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi ni Boniface Wambura ambaye sasa atakuwa na jukumu la kuchukua hatua kwa wasaidizi wake.

Fahamu wakati sahihi wa kumtambulisha mchumba wako kwa wazazi

Unakupokuwa na uhusiano na mtu, kila mmoja anatamani ifike siku wote wawili muweze kuishi pamoja, lakini siku hiyo huwa haiji hivi hivi, kuna hatua mnatakiwa kupitia tena kwa uwazi kufika hapo. Moja ya hatua kubwa ambazo zinawatatiza watu wengi ni kuwapeleka wenza wao kuwatambulisha nyumbani kwani hakika hilo huwa ni zoezi gumu. Suala hili hutofautiana kulingana na jamii ambazo wahusika wanatoka. Kwa upande wa jamii za Kiafrika mfano Tanzania, kwenda kumtambulisha mchumba sio kazi rahisi. Changamoto kubwa inayowakumba watu wengi ni namna ya kufahamu jinsi ya kufanya utambulisho huo lakini pia kufahamu wakati sahihi wa kufanya hivyo. Unaweza ukatamani uwekwe kwenye chumba uulizwe maswali ya kila namna kana kwamba unaomba kazi kuliko kutakiwa kumtambulisha mchumba kwa wazazi. Licha ya kuwa huenda mchumba wako alikuwa akija kwenu na mnakaa mnazungumza, lakini unapofika wakati wa kwenda kumtambulisha rasmi, changamoto huwa ni kubwa. Kuna vitu vya msingi, kote kwa mwanaume na mwanamke ...

Picha: Amiri Jeshi Mkuu, Rais Magufuli akutana na Wakuu wa Idara ya Usalama wa Taifa

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 31 Agosti, 2017 amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wastaafu na viongozi wa sasa wa vyombo vya ulinzi na usalama hapa nchini. Viongozi hao ni Wakuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ ), Wakuu wa Jeshi la Polisi, Wakuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Wakuu wa Idara ya Uhamiaji, Wakuu wa Jeshi la Magereza na Wakuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Baada ya mazungumzo hayo viongozi wastaafu wa vyombo vya ulinzi na usalama wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuwaita na kufanya nao mazungumzo, ambayo yamewawezesha kubadilishana mawazo na kuimarisha zaidi ushirikiano kati yao na viongozi wa sasa wa vyombo hivyo. “Tunamshukuru sana Mhe. Rais Magufuli na tunampongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya, sio jambo la kuficha amefanya kazi nzuri, na kila mmoja wetu amezungumza hilo na tunamtakia kila la heri ili aweze kuendeleza pale alipofika, kwa kweli tumefurahi sana”  amesema Bw. Co...

Kinachoendelea hivi sasa katika siku ya mwisho ya usajili barani Ulaya

Klabu ya Arsenal inasemekana tayari wamekubali ofa kutoka Manchester City kwa ajili ya kumnunua mshambuliaji Alexis Sanchez kutoka Arsenal, City walituma kiasi cha £60m na inaonekana Gunners wamekubali. Divock Origi amejiunga na klabu ya soka ya Wolfburg inayoshiriki ligi kuu soka ya Bundesliga, Origi amesaini mkataba wa kuichezea klabu hiyo kwa mkopo akitokea Liverpool. Klabu ya Chelsea baada ya kutoswa na Oxlade Chamberlain aliyesaini Arsenal sasa wamekubali kutoa pesa kwa Lazio kumnunua mlinzi Davide Zappacosta na dili hilo linaonekana tayari limeshakamilika. Hadi sasa haijaeleweka ni wapi winga Ryad Mahrez anaelekea, kwani ilisemekana yuko Hispania kukamilisha uhamisho wa kujiunga na Barcelona lakini klabu hiyo imesema haina mpango wa kumnunua, sasa Arsenal na Chelsea wanapewa nafasi kubwa kumnunua. Klabu za Paris Saint German na Monaco zimebadili makubaliano kuhusu usajili wa Mbappe, hapo mwanzo ilitakiwa Mbappe aende PSG kwa mkopo lakini sasa anauzwa kabisa kwa dili litak...

MADEE: Sikuwahi Kuwa na Ugomvi na Afande Sele Ila Tulikua Tunagongana Kimashairi

Picha
Msanii wa Bongo Flava kutoka Tip Top Connection, Madee amedai hakuwahi kuwa na tatizo na Afande Sele kama ilivyokuwa ikisemekana. Madee ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Sikila’ ambayo amemshirikisha Tekno kutoka Nigeria amesema kilichokuwa kinatokea kati yao ni kugongana kwa mashairi. “Hamna tatizo, kwani kulikuwa na tatizo, matatizo yalikuwa kwenye mashairi ndio yalikuwa yanasuguana. Hatujawahi kuwa na mataizo mashairi ndio yana mataizo yanapokutana huko redioni lakini tukikutana bro vipi na ni mtu muhimu sana kwangu,” amesema Madee. “Nimemuangalia kuna vitu vingi sana nimejifunza kupitia yeye. Hivi vitu vilikuwa vinazungumzwa na watu tu, watu ndio huwa wanatengeneza haya mambo,” ameiambia Bongo5. Kwenye wimbo wa Madee, ‘Nisikilize’ Madee aliwahikusema ‘yule mkulima alidai eti namgeza, alitamba zamani miaka hii hajaweza, anaumia kwanini mwanzo alicheza, hawezi kuosha nywele ana uhaba wa fedha’. Pia kat...

Kumbe Chid Benzi Alikua Anatania Collabo na 2Pac? Hivi Ndivyo Alivyofunguka Kwa Mashabiki Zake

Picha
Rapa Chid Benz ambaye sasa anafanya poa na wimbo wake 'Muda' akiwa ameshirikiana na mkongwe Q Chillah amefunguka na kuwataka mashabiki wake kutosikiliza maneno ya watu na kudai wapinzani wake wamekuwa wakimuongelea vibaya kwa lengo la kumchafua Chid Benz anasema muda mwingine kwenye maisha yake ya kila siku amekuwa ni mtu wa utani sana kiasi kwamba utani mwingine huwa hapendi hata ufike kwenye 'Camera' za watu kwa kudai unaweza kutafsiriwa ndivyo sivyo. Rapa huyo ameibuka na kusema hayo ikiwa ni siku moja imepita toka alipotoa kauli kwamba anataka kumleta marehemu 2Pac nchini na kusema msanii huyo wa Marekani ni mzima na wala hajafa na kudai tayari wameshafanya naye wimbo.

Waislamu Milioni Mbili Waanza Ibada ya Hajj Mecca

Picha
Mahujaji karibu milioni mbili kutoka nchi mbalimbali duniani wameanza kuwasili Saudi Arabia kwa ibada ya Hajj ambayo hufanyika kila mwaka. Walianza machweo Jumatano kwa kuzunguka Kaaba katika Msikiti Mkuu wa Mecca, eneo takatifu zaidi katika dini ya Kiislamu. Raia wa Iran kwa mara nyingine wanashiriki baada ya kukosa Hajj ya mwaka mmoja kutokana na mkanyagano uliotokea mwaka 2015. Kulikuwa na taarifa za kukinzana kuhusu idadi kamili ya mahujaji wanaohudhuria kutoka taifa jirani la Qatar, ambalo limekuwa kwenye mzozo mkali na Saudi Arabia. Kamati ya Taifa ya Haki za Binadamu, ambayo inafadhiliwa na serikali ya Qatar, imesema ni raia wachache sana wa Qatar ambao wamevuka mpaka, ambao ulifunguliwa wiki mbili zilizopita na serikali ya Saudia kuwawezesha Waislamu kuhiji. Lakini gavana wa Mecca amesema raia 1,564 wa Qatar wanashiriki ibada hiyo ya Hajj, idadi ambayo imeongezeka ukilinganisha na 1,210 mwaka jana. Kwa Waislamu, Hajj ndiyo nguzo ya tano na ya mwisho ya dini ya Kiislamu. ...

DAYNA NYANGE: Natamani Kungekua na Sheria Inayowabana Wanaume Wanaokataa Mimba

Picha
Msanii wa muziki wa bongo fleva Dayna Nyange amesema anatamani kungekuwa na sheria inayowabana wanaume ambao wana tabia ya kukataa ujauzito, kwani kitendo hicho hakifai kwenye jamii. Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, Dayna amesema yeye kama miongoni mwa wanawake ambao wanalea mtoto bila msaada wa mzazi mwenza, anaumizwa na tabia hiyo, hivyo anatamani nchi ingeweka sheria kuwabana watu hao. Akielezea suala hilo kwa hisia hadi machozi yakianza kumtoka, Dayna alisema "hicho kitu kinaniumiza sana, yani natamani kungekuwa na sheria fulani ikitokea tu umekataa tu mimba, bado hadi mtoto anazaliwa unakataa, upewe adhabu ambayo itakuumiza sana maishani mwako". Dayna ambaye ana mtoto ambaye yuko darasa la 5 sasa na anapambana mwenyewe kuhakikisha anapata mahitaji yote, amesema yeye alipitia wakati mgumu mpaka alikuwa na chuki juu ya mzazi mwenzake, hali ambayo ilimfanya afunge na kumuomba Mungu ili aweze kuondoa roho ya chuki dhidi ya m...

Mkuu wa Mkoa wa Zanzibar Awapost Ali Kiba na Diamond Awapa Ushauri Huu

Picha
Wakati kukiwa bado fukuto kwa mashabiki mitaani kuhusu ni Ngoma ya Nani kali kati ya Aliyoachia Alikiba 'Seduce Me' na Zilipendwa ya WCB, basi hata serikalini wasanii hao wameendelea kugawagawa viongozi, ambapo Imeonekana Posti hii ya Diamond na Alikiba kwenye ukurasa wa Instagram wa mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mahmoud iliyoambatana na ujumbe huu "Nimeuelewa sana wimbo wa vijana wetu #wcb wakiongozwa na ndugu @diamondplatnumz hakika nimewaelewa sana kwenye wimbo wao wa #ZILIPENDWA, hii na pia nathamini kazi kubwa iliofanywa na kijana wetu ndugu yangu @officialalikiba, hakika wimbo wako ni wimbo nilio tokea kukubali. kama kiongozi niko proud sana na kazi nzuri zinazofanywa na vijana wetu kwa kutuwakilisha vyema nje ya mipaka yetu Ushauri wangu kwenu ni kua,tofauti zenu ziwe za kibiashara na sio vyenginevyo, #seduceme #fire#song #teammzikimzuri" Aliandika RC Ayoub

Hospitali ya Muhimbili Yazindua Uduma ya Malipo Kwa Njia ya Kielectroniki

Picha
Uongozi wa hosptali ya Muhimbili kupitia kwa mkurugenzi mtendaji wa hosptali hiyo Profesa Lawrence Maseru, amezindua mfumo mpya wa malipo ya matibabu kwa njia ya kielektroniki mapema leo mchana katika hosptali hiyo. hosptali ya Muhimbili Akizungumza na waandishi wa habari, profesa Maseru amesema, lengo la kusimikwa kwa mfumo huo katika hosptali ya Muhimibili ni kuondoa adha kwa wagonjwa au ndugu mbalimbali wa wagonjwa kwa kukaa muda mrefu kwenye foleni za kulipia huduma mbalimbali zinazo tolewa na hosptali hiyo. hosptali ya Muhimbili “Dhumuni la kuja na mfumo huu kwanza kuondoa kadhia na lapsha zilizokuwepo wakati ndugu wa wagonjwa walipokuwa wakifanya malipo ya huduma mabalimbali zitolewazo na hosptali yetu. Vilevile ni kudhibiti mapato ya serilikali ambayo inawezekana kwa njia moja ama nyingine yalikuwa yakipotea,” alisema Masaju. hosptali ya Muhimbili Akitoa ufafanuzi namna wateja watakavyoweza kutumia mfumo huo, mkurugenzi wa fedha na mipango wa hosptali ya muhimb...

Mke wa Roma: Kama Roma Akitaka Kumuoa Mange Sina Shida Amuoe Tu

Picha
Kwenye mitandao ya kijamii August 30, 2017 gumzo lilikuwa post ya mke wa Roma Mkatoli, Mama Ivan kwenye Instagram yake baada ya kuelezea kipande cha wimbo mpya wa Roma ‘Zimbabwe’ akisema kila anapokisikia hupata wivu. Licha ya kudai kuwandika maneno hayo kama utani huku wengi wakiyachukulia serious hadi kupelekea Mange Kimambi kuyanasa na kisha kuya post kwenye Istagram na kumuomba Mke wa Roma amruhusu awe mke mwenza ili amsaidie kumlinda Roma asiibiwe na wanawake wangine. Mke aliandika Instagram...“Kiukweli kila nikisikiaga huu msatari napata sanaaa wivu, utani utani hivi hivi mwisho wa siku inakuwa kweli, mimi mwenyewe alinianza kiutani utani hivi hivi, yani nyie!! wanaume hawa!! Kuolewa na msanii kunahitaji moyo” – Mke wa Roma Mke wa Roma alihojiwa na kufunguka akisema hakuwa serious bali kama Roma ataamua kumuowa Mange hatakuwa na usemi kwa kuwa mwanaume ndio mwenye maamuzi ingawa amedai hategemei kuona akioa mke mwingine kwa sababu dini hairihusu. ...

Oxlade Chamberlain kwenda Liverpool ni usajili wa kisoka zaidi kuliko pesa

Picha
Neymar amekwenda PSG kwa rekodi ya dunia ya £220m, Osmane Dembele akaenda Barcelona waweka mzigo wa £160m,Morata Chelsea wakatoa £70m na United nao wakatoa £90 kumnunua Lukaku. Hilo ndio soka mwanangu, pesa mbele mapenzi baadaye. Wachezaji wote hao hapo juu na wengine wengi wamevutiwa sana na kiasi cha pesa ambacho wameahidiwa japo ukubwa na historia za klabu walizoenda pia ni sababu. Mpira wa sasa upo kibiashara zaidi na mwenye biashara nzuri ndio atafaidika, soka la sasa limekuwa na vijana ambao wanaangalia zaidi maslahi na ndio maana haikushangaza ligi kuu nchini China ilipoanza kuwatishia vigogo wa Ulaya, ndioo lazima wawatishe kwa sababu wana pesa. Nchini Uingereza inaonekana vijana wengi wadogo waliokulia Southampton wanapaona Anfield kama sehemu nzuri zaidi kutamani kwenda na ndio maana haikuwa ngumu kwa Ricky Lambert, Adam Lallana, Nathan Clyne na hata Sadio Mane kukubali kujiunga na Liverpool. Shabiki mmoja alifanya mzaha na kusema Liverpool walitaka k...

Azma ya Rais Magufuli kwa Kampuni ya IPTL yatimia

Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imekataa kuiongezea muda wa leseni Kampuni ya kufua umeme wa Independent Power Tanzania Limited (IPTL) baada ya leseni yake ya kuzalisha umeme kumalizika muda wake. Agosti 30 mwaka huu kupitia taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, Bodi ya Wakurugenzi wa EWURA ilisema kuwa kikao chake kilichofanyika kimefikia uamuzi wa kutiongezea kampuni hiyo leseni ya biashara. Machi 28 mwaka huu, IPTL iliwasilisha maombi EWURA ikiomba kuongezewa muda wa leseni yake ya kufanyakazi nchini kwa miezi 55 kuanzia Julai 16, 2017 hadi 15 Januari 2022. Bodi ya Wakurugenzi ya EWURA imesema kuwa imezingatia mambo mbalimbali katika kuikatalia IPTL maombi yake ambayo ni, athari hasi kwenye bei ya umeme kwa watumiaji endapo muda wa leseni ya IPTL ungeongezwa ikiwa ni pamoja na kuendelea kulipa malipo ya ‘capacity charge’ kwa kiasi cha dola 2.667 milioni kwa mwezi. Sababu nyingine iliyotajwa na EWURA ni ma...

Mkuu Wa Mkoa Mjini Magharibi Atoa Taarifa Kuhusu Sikukuu Ya Eid El Hajj Kesho

Picha
Ndugu wananchi wakaazi wa Mkoa wa Mjini Magharibi wasikilizaji na watazamaji. ASSALAMU ALAYKUM, Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyenzi Mungu kwa kutujaalia neema ya uhai, uzima, amani na utulivu katika Mkoa wetu wa mjini Magharibi. Ndugu wananchi kama mjuavyo kuwa siku ya Ijumaa ya tarehe 1/9/2017 tutasherehekea sikukuu ya Eid El Hajj ambapo waislamu wote duniani wataungana na mahujaji waliopo Makka Saudi Arabia baada ya kukamilisha nguzo ya tano ya kiislam kwa kutekeleza ibada ya Hijja ambayo ni lazima kwa mwenye uwezo. Ndugu wananchi pamoja na wakaazi wote wa Mkoa wa Mjini Magharibi  napenda nichukuwe fursa hii  kutoa taarifa inayolenga kuwanasihi na kukumbushana mambo muhimu ya kuzingatiwa  katika kipindi chote cha skukuu na  baada ya skukuu ndani ya Mkoa wa Mjini Magharibi ili kuendeleza na kudumisha amani iliyopo. Kwa mwaka huu wa 2017 swala ya eid itafanyika Wilaya ya Magharibi B katika kiwanja cha Dimani na Baraza la Eid litafanyika Bweleo katika ene...

Wanafunzi Ichini India Wafunzwa Kuhusu Njia za Kutoa Talaka

Picha
Shule moja nchini India itaanza kuwafunza wavulana wa Kiislamu njia za kutoa talaka kulingana na sheriza za Kiislamu. Shule ya Dargh-E-Ala Hazrat inayodhibiti madrassa 15,000 za Kiislamu ilitangaza hilo kufuatia agizo la mahakama lililopiga marufuku talaka za moja kwa moja. Wasomi wa Kiislamu wamedai kwamba talaka za moja kwa moja haziambatani na sheria ya kiislamu. Kiongozi mmoja wa dini kutoka shule hiyo amesema kuwa wataanzisha kifungu kitakachoangazia maswala ya talaka. Mtaala wa shule hiyo ambao unaangazia Koran na sheria za kiislamu unazungumzia kuhusu talaka lakini sio kwa maelezo ya kina. ''Tulifanya mkutano wa viongozi wa dini pamoja na wale wa Madrassa baada ya agaizo la mahakama kuu na tumewaelezea jamii kupitia wanafunzi na katika ibada za siku ya Ijumaa kuhusu njia bora za kutoa talaka'', Maulana Shanbudin Racvi kiongozi mkuu wa dini aliambia BBC Hindi. Aliongezea kuwa hatua hiyo itaelezea vyema kwamba talaka ya moja kwa moja zinazoetekelezwa nchini ...

Dkt. Makongoro Mahanga Akamatwa na Kufikishwa Mahakamani

Picha
Mbunge wa zamani wa Ukonga na Segerea, Dk Makongoro Mahanga amekamatwa na Polisi Mkoa wa Ilala kwa amri ya Mahakama Kuu na amefikishwa mahakamani. Mahakama iliamuru Dk Mahanga akamatwe na kufikishwa mahakamani kwa kushindwa kutekeleza uamuzi unaomtaka amlipe mdai Kainerugaba Msemakweli Sh14 milioni. Fedha hizo ni gharama za kesi alizozitumia Msemakweli baada ya kushinda kesi ya madai ya kashfa ambayo Dk Mahanga alimfungulia kwa kumtaja kwenye kitabu chake kinachoitwa: “Mafisadi wa Elimu”. Katika kitabu hicho anamtaja kuwa ni mmoja wa viongozi wenye shahada za udaktari wa kughushi. Kati ya kiwango hicho cha fedha, Dk Mahanga ameshalipa Sh6 milioni hivyo anadaiwa Sh8 milioni.

Ajira Lukuki Zamwangwa Kibiti na Serikali

Picha
HALMASHAURI ya Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani imetangaza nafasi 45 za ajira kwa wanaotaka kuwa watendaji wa vijiji wilayani humo. Imesema imetangaza ajira hizo, ili kupata watendaji wa vijiji watakaoziba mapengo ya waliofariki na walioachishwa kazi kutokana na kuwa na elimu ya darasa la saba. Kibiti ni miongoni mwa wilaya za mkoa wa Pwani ambazo kwa miaka miwili iliyopita, zimekumbwa na mauaji ya viongozi wa ngazi mbalimbali, wakiwamo watendaji na wenyeviti wa vijiji. Mauaji hayo yalikuwa yakitekelezwa na watu wasiofahamika, waliokuwa wakivamia nyumba za watendaji hao na kuwaua kwa kuwapiga risasi. Wilaya nyingine za mkoa huo zilizokumbwa na mauaji hayo ni Rufiji na Mkuranga. Aidha, kutokana na kushamiri kwa mauaji hayo na vitisho vilivyokuwa vikitolewa na wauaji, baadhi ya watendaji wa vijiji waliripotiwa kukimbia makazi yao wakihofu kuuawa. Akizungumza na Nipashe kwa simu jana, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti, Alvera Ndabagoye, alisema hali ya wilaya yake kwa sasa...

CHADEMA Yatangaza Mgomo Kushindikiza Kutolewa kwa Mbunge wa Tunduma

Picha
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza mgogoro na mkuu wa wilaya ya Momba, Juma Irando kwa kuagiza jeshi la polisi wilayani humo kumuweka ndani kwa saa 48 mbunge wa Jimbo la Tunduma, Frank Mwakajoka kwa madai ya uchochezi. Katika kikao alichofanya na wanahabari, Mwenyekiti wa CHADEMA, Halmashauri ya mji wa Tunduma, Ali Mwafongo ameleezea kusikitishwa na amri hiyo ya mkuu wa wilaya na kusema kuwa kamwe hawatarudi nyuma huku akiahidi kutompa ushirikiano mkuu wa wilaya huyo. "Uchungu tunaopata sasa hivi tunajua ipo siku itakuwa furaha kwetu kwani ushindi unakaribia. Kinachofanywa sasa hivi wakumbuke ipo siku watawala watakuwa wapinzani na haya yanayofanywa hayataweza kuturudisha sisi nyuma. Viongozi wetu wamekuwa wakipelekeshwa sana lakini katu hatutokata tamaa kwa sababu ni kazi yetu kusema ukweli na kuwatumikia wananchi wetu" alisema Mbali na hayo mkuu huyo wa wilaya pia ametuhumiwa kutoa amri ya kushusha bendera za chama hicho hali ambayo imeonesha kuwake...

Kweli Pesa Inatakatisha, Huu Ndio Muonekano wa Sasa wa STEVE YANGA (Shabiki wa Yanga wa Kulia lia)

Picha
Huyu kijana alijizolea umaarufu miaka ya nyuma kutokana na tabia yake ya kulia lia sana pale timu yake ya Yanga ilipokuwa ikipokea kichapo alikuwa anashindwa kabisa kujizuia vile vile alihangaika kushiriki kwenye mashindano ya bongo star search lakini hakupata nafasi. Hii picha kipindi analia baada ya yanga kupokea kichapo hapa kipindi anatafuta nafasi Bongo  Star Search  Hapa kipindi anatafuta nafasi Bongo  Star Search Huu sasa ndio muonekano wa sasa baada ya kula kitengo pale AZAM na yanga kawahama kabisa NB:jamaa mwanzoni alionekana kama kituko sasa hivi kala kitengo hata harmorapa akiendeleza janja janja za kiki atatusua tu siku moja.

Nandy Afunguka Vitu Ambavyo Anavutiwa Navyo kwa Dogo Janja na Bill Nass

Picha
HIT maker wa ngoma ya Wasikudanganye, Faustina Charles ‘Nandy’ amesema kuwa anavutiwa na kila kitu ambacho wasanii wenzake wawili; Dogo Janja na Billnas hivyo kwake yeye, hao ndiyo chaguo lake. Akizungumza na Showbiz Extra, Nandy alisema, mbali na kwamba wasanii hao kuwa washkaji zake wa karibu na kuhusishwa nao na skendo za mapenzi lakini uwezo wao katika kazi unamfanya kuwa shabiki namba moja wa waimbaji hao. “Kwa Billnas na Dogo Janja huniambii chochote, kwa hapa Bongo hao ndiyo wasanii wangu bora, napenda kile wanachofanya cheki wanavyovaa, cheki muziki wao, cheki wanavyojua kwenda na wakati, kwa kweli sina sababu ya kutowashabikia ingawa nimekuwa nikihusishwa kutoka nao kimapenzi lakini hakuna ukweli wowote,” alisema Nandy.

Odama Afunguka Sababu ya Kutofanya Sherehe Kubwa Siku Yake ya Kuzaliwa

Picha
STAA wa filamu Bongo, Jennifer Kyaka ‘Odama’ amefunguka kuwa hakuweza kufanya sherehe kubwa kwenye siku yake ya kuzaliwa kwa sababu anaona kufanya hivyo ni kama utoto. Akizungumza na Amani, Odama alisema ameamua kutofanya kitu kubwa mpaka atakapokuwa mzee, itakuwa na maana kubwa kuliko kufanya kila mwaka. “Huwezi amini yaani hata kama zamani nilikuwa nafanya hivyo basi nilikuwa bado akili yangu haijachangamaa kabisa lakini mambo ya sherehe kubwa nitafanya nikiwa mzee kwa sasa tena hapana,” alisema Odama ambaye bethidei yake ni Agosti 26. Stori zinazo husiana na ulizosoma

Aliyekuwa Daktari wa Rais Kikwete amtetea Manji kesi ya dawa za kulevya

Daktari, Mohammed Janabi (51) kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu namna walivyouchunguza moyo wa mfanyabiashara Yusuf Manji alipopelekwa hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu. Prof. Janabi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI alisema kuwa, alichunguza moyo wa Manji ambaye pia ni Diwani wa Mbagala kwa tiketi ya CCM ili kuweza kutambua kama vyuma vilivyopo kwenye moyo wake kama vimeziba au la ambapo walibaini kwamba havijaziba. Janabi ambaye amewahi kuhudumu pia kama Daktari wa Rais wa awamu ya nne, Dkt Jakaya Kikwete aliyasema hayo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakati akiongozwa na wakili Hajra Mungula kutoa ushahidi mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha. Akijibu swali la wakili kuhusu athari za kutumia dawa za kulevya aina ya heroine na kuvuta sigara kwa wagonjwa wa moyo, Prof. Janabi alisema kwamba, matumizi ya vitu hivyo hupelekea vyuma kwenye moyo wa mgonjwa kuziba na kufanyiwa u...

Dereva Aliyegonga Treni Morogoro Afikishwa Mahakamani

Picha
Dereva wa daladala aliyesababisha ajali iliyoua wanafunzi watatu na abiria wengine 27 kujeruhiwa mkoani Morogoro amefikishwa mahakamani kujibu mashtaka 30, likiwemo la kuendesha gari kwa uzembe na kugonga treni ya abiria ya Shirika la Reli Tanzania (TRL). Katika Mahakama ya Wilaya ya Morogoro, Charles Petro ambaye alipata majeraha kwenye ajali hiyo amesomewa mashtaka mbele ya Hakimu Joyce Mkoi. Wakili wa Serikali, Caristus Kapinga amedai Agosti 24 asubuhi, kwenye makutano ya reli na barabara eneo la Tanesco, Manispaa ya Morogoro mshtakiwa alitenda makosa hayo. Kapinga amedai kwa makusudi, huku akijua kufanya hivyo ni kosa mshtakiwa aliendesha gari aina ya Nissan kwa uzembe na kugonga treni ya abiria iliyokuwa ikitokea Dodoma kwenda Dar es Salaam. Kutokana na ajali hiyo, wanafunzi watatu walifariki dunia na abiria 30 walijeruhiwa wakiwemo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari zilizoko Kihonda na Msamvu katika Manispaa ya Morogoro.  Mshtakiwa amekana mashtaka yote na  ...

Urusi yatia mguu mgogoro wa Korea Kaskazini, yaitahadharisha Marekani

Picha
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Urusi, Sergei Lavrov amemwambia waziri wa Ulinzi wa Marekani, Rex Tillerson kuwa kuiwekea vikwazo vingi Korea Kaskazini hakutasaidia chochote kutatua mgogoro uliopo kuhusu mpango wake wa nyuklia. Katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje nchini Urusi imesema kuwa viongozi hao wamezungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio yanayofanywa na Korea Kaskazini. Lavrov amesema kuwa diplomasia ndio njia pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Hata hivyo, Waziri wa ulinzi wa Marekani amesema kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini ili iweze kuachana na mpango wake wa majaribio ya silaha za nyuklia huku Rais Trump akisema mazungumzo sio suluhisho

Marekani: Tutaendelea na mazungumzo na Korea Kaskazini

Picha
Waziri wa ulinzi nchini Marekani James Mattis amesema kuwa Marekani itaendelea na mazungumzo ya kidiplomasia na Korea Kaskazini. Matamshi hayo yanajiri baada ya rais Donald Trump kusema katika mtandao wake wa Twitter kwamba mazungumzo sio suluhu kwa mipango ya kijeshi ya Korea Kaskazini. Urusi pia imeionya Marekani dhidi ya kuchukua hatua za kijeshi akisema madhara yake yatakuwa makubwa. Korea Kaskazini ilizua wasiwasi baada ya kurusha kombora kupitia anga ya Japan siku ya Jumanne. Kombora hilo ambalo Japan limelitaja kuwa tishio lisilo la kawaida , lilivuka katika anga ya kaskazini ya kisiwa cha Japana cha Hokkaido mapema siku ya Jumanne, na kusababisha raia kujificha kabla ya kombora hilo kuanguka baharini yapata kilomita 1,180 . Korea Kaskzini baadaye ilisema kuwa ni hatua mojawapo ya operesheni zake za kijeshi katika eneo la pacific na kurejelea tishio lake la kushambulia kisiwa cha pacific cha Guam. Siku chache zilizopita, bwana Trump alikuwa amenukuliwa akisema anaamini ki...

Mh Rais Chapa Kazi, Ukicheka na Kima Utavuna Mabuwa, Usigeuke Nyuma...Kipindi cha Mpito Maumivu Lazima...Asichomoke Mtu

Picha
Kuna watanzania wengine wana akina za ki-zwazwa sana. Kila siku wanalalamika, ooh mara Rais hivi...ooh mara kafanya vile. Mnataka afanyeje? Afanye kama kila mtu anavyotaka amekuwa malaika?Ukiulizwa wewe umefanya nini utajibuje? Tanzania ilishakuwa ya watu wachache walewale wanaojuana, watu maarufu. 1. Watu walikuwa wamehodhi maeneo makubwa nchi nzima, wakati hawayafanyii kazi 2. Wafanyabiashara wengi walikuwa hawalipi kodi 3. Wafanyakazi hewa, dawa hewa, mishahara hewa, pembejeo hewa,vyeo hewa 4. Wakubwa walikuwaga wanajitanua sana, walikuwa wanatunyanyasa sana. Utafikiri sisi ni wakimbizi 5. Mamikutano ya hadhara yalikuwaga kila siku makelele, wanakusanya watu ambao wanatakiwa wafanye kazi 6. Viongozi wa Serikali walikuwaga wanajilipa double payments, wanasafiri nje ya nchi kutanua tu makundi kwa makundi 7. Vimemo tu ndo vilikuwa mpango mzima. Undugu tu kila kona 8. Mafuta hewa, posho hewa, safari hewa, maiti hewa, kodi hewa Ingekuwa ni wewe, 1. Vijana wote walioko mtaani ...

Taarifa muhimu kwa waombaji wote wa mikopo ya vyuo vikuu 2017/18

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeongeza muda wa siku saba wa kutuma maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2017/2018 ili kutoa nafasi kwa waombaji mikopo ambao hawajakamilisha baadhi ya hatua za kujaza fomu za maombi kukamilisha na kutuma. Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Bodi ya Mikopo zilizopo Mwenge jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji Bw. Abdul-Razaq Badru amesema kuwa maombi ya mikopo yaliyokuwa yafungwe Septemba 4, yataendelea hadi Septemba 11, 2017. Aidha, Badru amewasisitiza waombaji wa mikopo kuzingatia mwongozo uliotolewa na Bodi unaowataka kuambatanisha nyaraka zote zilizothibitishwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamimi (RITA), makamishina wa viapo, mawakili na serikali za mtaa na kuziwasilisha kwenye mtandao wa Bodi. Maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2017/2018, yanayofanyika kwa njia ya mtandao olas.heslb.go.tz  yalifunguliwa Agosti 6, 2017. Mpaka kufikia Agosti 29, 2017, maombi ya mkopo zaidi ya 50,000 yalikuwa yam...

Vibaka wa mitandaoni almanusra wawaingize Cr7 na Romelu Lukaku katika mzozo

Picha
Teknolojia imekuwa kubwa siku za usoni na watu wanatumia mitandao ya kijamii kurahisisha mawasiliano yao, lakini mitandao hiyo hiyo wapo wanaoitumia vibaya na kuleta machafuko. Wahalifu wa mitandao walifanikiwa kuiba account ya mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku, hawakuishia hapo tu bali walienda mbali zaidi na kufanya jambo linaloweza kuleta ugomvi kati ya Lukaku na Cristiano Ronaldo. Baada ya tukio la Ronaldo kumsukuma muamuzi katika mchezo wa El Classico na kupewa adhabu ya kukaa nje michezo mitano, Ronaldo aliandika mtandaoni kutovutiwa kwakwe na maamuzi ya tukio hilo. Sasa wakati Cristiano akijitetea kupitia Instagram account yake kati ya watoa maoni wa tukio hilo mmoja wapo alikuwa ni Lukaku ambaye aliandika Lioneil Messi ni bora kuliko Cristiano Ronaldo. Baada ya muda comment hiyo ilifutwa lakini watu walishaiona, ilibainika kwamba hakuwa Lukaku aliyeandika hivyo bali account yake iliibiwa japokuwa hadi sasa Lukaku mwenyewe hajaongea lolote kuhusiana na tukio h...

SOMA Nafasi za Ajira Mbali Mbali Zilizotangazwa Siku ya Leo

Picha
Bonyeza link zifuatazo kusoma zaidi na kuapply nafasi hizi: Job Opportunity at Palladium, Monitoring & Evaluation Officer Job Opportunity at Estim Construction Co. Ltd, Contracts Manager 3 Job Opportunities at RAO Hospital 560 Job Opportunities at The National Bureau of Statistics (NBS) 11 Job Opportunities at TANROADS Job Opportunity at Tanzania Teachers Union, Registry Job Opportunity at CVPeople Africa, Administration Officer 4 Job Opportunity at CVPeople Africa, Assistant Health Inform Officers Job Opportunity at KP Recruiters, Chief Accountant 5 Job Opportunities at TPC Ltd Job Opportunity at WHO, Medical Officer 2 Job Opportunities at Acacia Mining, Environmental Officers Job Opportunity at I-TECH Tanzania, Operations Manager Job Opportunity at Laborex Tanzania, Human Resources Officer Nafasi zingine ingia  www.ajirayako.co.tz

NIYONZIMA Kafunguka: Ni Kuhusu Uhusiano Wake na Jini Kabula Uliotaka Kuvunja Ndoa yake

Picha
Kabla ya Jini Kabula kuwa katika matatizo aliwahi kunukuliwa akisema aliwahi kuwa mapenzini na staa wa soka wa Simba SC, Haruna Niyonzima na kuzua mzozo kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwa Niyonzima kwenye ndoa hivyo kumsababishia matatizo ndani ya familia yake. Ayo TV na millardayo.com zimempata Haruna Niyonzima kwenye EXCLUSIVE na kufunguka kila kitu akisema hakuwahi kuwa mapenzini na msichana huyo licha ya kwamba kuzungumza kwenye vyombo vya habari. Aidha, kuhusu mkewe kulisikia hilo alisema haikuwa rahisi kuchukulia kawaida ingawa ni muelewa na alijaribu kuelewa jambo hilo. Bonyeza Play hapa chini kumsikia Niyonzima 

Dogo Janja Anyoosha Maneno Kuhusu Irene Uwoya, ‘Nampenda Sana’

Picha
Msanii wa Bongo Flava, Dogo Janja amezungumzia taarifa zilizokuwa zikidai kuwa anatoka kimapenzi na Muigizaji wa filamu Irene Uwoya. Rapper huyo ambaye ameachia ngoma mpya leo ‘Ngarenaro’ amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds Fm kuwa ukaribu wao ulikuwa wa kawaida tu na hakuna kilichokuwa kinaendelea kati yao ingawa watu waliwachukulia vinginevyo. “Nampenda sana yule dada lakini kuwa na mazoea naye kidogo kumezua maneno mengi,” amesema Dogo Janja. July mwaka huu zilienea taarifa katika mitandao ya kijamii kuwa wawili hao wameonakana jijini Mwanza katika matanuzi  ya nguvu kitu kilichozua minong’ono kuwa wapo mapenzini.

Tanzania Yatajwa Kwenye Orodha ya Nchi Zenye Mishahara Mikubwa Afrika

Picha
Shirika la Numbeo limetoa orodha ya nchi kumi zenye mishahara mikubwa zaidi barani Afrika. Hili ni shirika kubwa zaidi duniani la ukusanyaji wa taarifa za majiji na nchi. Shirika hili linatoa taarifa za mara kwa mara kuhusu hali za maisha duniani ikiwemo gharama za maisha, upatikanaji wa nyumba za kupanga, huduma za afya, foleni za barabarani, uhalifu na kiwango cha uchafuzi wa mazingira. Zifuatazo ni nchi kumi za kiafrika zenye viwango vya juu zaidi vya mshahara: 1. Libya Libya ndiyo nchi inayoongoza barani Afrika kwa kuwa na viwango vikubwa vya mishahara. Nchi hii yenye utajiri wa mafuta imejulikana kwa zaidi ya miongo minne ya utawala wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Hayati Muammar Gaddafi na machafuko yaliyofata baada ya kifo chake. Na pamoja kwa machafuko ya kisiasa yanayoendelea nchini humo mpaka sasa yanayosababisha hali ya usalama kuwa tete, kiwango cha kawaida cha mshahara kwa mwezi baada ya makato ya kodi ni shilingi milioni tatu na laki nane (3,800,000) Ingawa machafuko ...

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamis ya August31

Picha