SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 28 Agosti 2017

T media news

Watu Wawili Wa Familia Moja Wamefariki Dunia Kwenye Ajari

Watu saba wamefariki katika ajali mbili tofauti ambapo ajali ya kwanza watu wawili wa familia moja wamepoteza maisha na wengine sita kujeruhiwa katika ajali ya gari dogo aina ya Kluger iliyotokea eneo la Masaki mkoani Pwani leo.

Majeruhi sita wa ajali ya gari ndogo iliyotokea mkoani Pwani wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani na taratibu zinafanyika ili kupelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi kutokana na hali zao kuwa mbaya.

Aidha watu wengine watano wamefariki dunia na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha lori la mzigo lililokuwa limebeba abiria mkoani Singida.
Ajali zote mbili zimesababisha vifo vya watu saba huku wengine 26 wakiwa ni majeruhi Tundu Lissu apingwa