SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 30 Agosti 2017

T media news

Picha za Ngao ya Jamii ya Simba baada ya kurekebishwa na TFF

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limefanya marekebisho katika Ngao ya Jamii waliyoshinda Simba.

Simba walikabidhiwa Ngao ya Jamii baada ya kuifunga Yanga kwa mikwaju 5-4 ya penalti, lakini ikawa na makosa katika maandishi.

Ngao hiyo ilikuwa imeandikwa, Community Sheild badala ya Community Shield.

Baada ya malalamiko kuwa makubwa, TFF iliomba Simba kuirudisha ngao hiyo kwa ajili ya marekebisho na sasa hilo, limefanyika.