SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 30 Agosti 2017

T media news

Sijawahi Kumuhonga Mwanamke Pesa Ili Anipende - Mwana FA


RAPA asiyechuja kwenye muziki wa Hip Hop Bongo, Hamis Mwijuma ‘Mwana FA’ ametoa kali ya mwaka baada ya kusema kuwa katika maisha yake yote ya ujana, hajawahi kumhonga mwanamke pesa ili apendwe.

Akichonga na Risasi Vibes, Mwana FA alisema tabia ya kuhonga honga wanawake pesa na vitu vingine vya thamani ili kupendwa hilo kwake halijawahi kutokea tangu alipopata akili mpaka alipo sasa kwenye ndoa.

“Nihonge ili nipate nini, sijawahi kuhonga hata siku moja najua wengi wanaweza wasiamini lakini ndiyo hivyo, tabia hizo naishia kuziona kwa washkaji zangu huku mtaani lakini kwangu hazijawahi kuwepo maana kitendo hicho nakichukulia kama biashara ya kikahaba ambayo binafsi naichukia” alisema Mwana FA